Watu wengi siku hizi wamekuwa wakijihusisha na upandaji miti katika mashamba binafsi, miti hii ina matumizi mbali mbali ikitumika kama mipaka, chanzo cha kuni, mbao, chakula cha mifugo, urembo n.k.
Miti ya mitiki ni moja ya miti inayotoa mbao ngumu na aghali zaidi duniani, vitu kama boti na mashua, vitako vya bunduki, fimbo za askari, milango na samani mbalimbali za majumbani hutengenezwa kutokana na miti hii.
Mti hii inasifika kwa uimara wa kutoliwa na wadudu kama mchwa na kuoza kutokana na maji kwa sababu ina hali ya mafuta mafuta. Mbao zake zina rangi nyekundu iliyokolea na kama mti litunzwa vituri kwa kupunguziwa matawi mapema, mbao zinakuwa hazina vidoda vidonda.
Kwa hapa nchni mashamba makubwa yanapatikana Kilombero, mtibwa na longuza (Lushoto) pia kuna wakulima wadogo wadogo katika mikoa ya Tanga, Morogoro na Pwani.
Kwa kawaida miti hii hustawi zaidi katika ukanda wa pwani wenye joto na mvua nyingi, hustawi katika udongo wa kitifu tifu wenye mbolea ya kutosha na usio tuamisha maji kabisa. Miti inayopandwa mabondeni inakuwa haaraka sana kuliko iliyopandwa sehemu za miinuko, ingawa miti ilipondwa kwenye miinuko inatoa mbao bora zaidi kutokana na kukua taratibu kidogo.
Uvunaji unaanza baada ya miaka 6-7 kwa kutoa miti ya kujengea ambayo hupatikana kwa kupunguza miti ya kati ili ile inayobaki iweze kukua zaidi. Mbao huanza kuvunwa baada ya miaka 12 - 15, ikifuatiwa na miaka 18. 20, 25, kumbuka uvunaji huu unafanywa kwa kupunguza nusu ya miti (kati ya mti na mti) na kuacha inayobaki iendelee kukua zaidi.
6 comments:
Asante sana kwa hii elimu Benet. unatusaidia sana. hizi ndo zile tunaita urithi ambazo mtu anauacha duniani na kukumbukwa kwa mchango wake. Unatoa mchango mkubwa sana hapa Bro. bila kujua Mungu akutie nguvu uendelee bila kuchoka.
nimefurahi sana kuona habari habari za mitiki .mwaka huu nimejikita kwenye kilimo cha mitiki kisarawe na mkuranga .naamini hii blog itakuwa ya msaada .tunashukuru sana kazi nzuri
Asante Kwa darasa
Nashukuru sana kwa elimu,Mimi nipo ngara mkoani kagera naweza kupanda na ikasitawi vizuri ndugu zangu.
Nice darasa
Shukran kwa Darsa
Post a Comment