Hii ni hatua muhimu sana kwa ukuaji wa miti ya mitiki, na mara nyingi hufanyika ili kupunguza upotevu wa maji toka kwenye mmea. Mara nyingi kipindi cha jua miche midogo huwa ipata tabu sana kupambana na hali ya ukame, na kama ilivyozoeleka ukanda wa pwani ambako ndio miti hii inastawi zaidi huwa na jua kali sana mpaka kufikia kiasi cha nyuzi joto za sentigredi 33 - 34.
Miti ya mitiki huwa inapoteza maji mengi sana kupitia majani yake kwa sababu ina majani mapana sana ambayo yanapoteza maji mengi sana kipindi cha jua (evaporation). Kipindi cha kupunguzia majani ni kipindi ambacho ardhi inakuwa wazi kwa sababu hatua hii hufanyika mara baada ya kupalilia miti yako
Wakati wa kupunguzia majani inabidi kuwe na umakini ili kuepuka kuvunja sehemu ya juu ya mti (kikonyo) na unapopunguzia majani ni lazima utoe jani moja kila upande. Unaweza kutumia mikono lakini ili kuepuka madhara nashauri visu vidogo vitumike kupunguza majani ya chini.

2 comments:
Sijaelewa kitu mkuu. Kwa nini tupunguze majani wakati tunaambiwa kwenye majani ndimo kuna chanikiwiti ya kusadisia chakula? Sio kwamba mmea utapata 'kwashiakoo' kwa kushindwa kujitengenezea chakula chake?
Asente
Miche ikiwa midogo wakati wa jua kali kama haijapandwa sehemu yenye unyevuunyevu huwa inapata tabu sana na unaiona inavyo nyauka, nitatuma picha, ukiruhusu hali hii mmea utapukutisha majani yote na mwisho ncha ya juu kabisa ya mti huanza kukauka
madahara yake ni kwamba mvua zikirudi utatoa matawi kwa sababu pale juu nchani palikufa, matokeo mbao zako hazitakuwa zimenyooka na zina vidonda vidonda sababu ya matawi
Post a Comment