Jana nilipata mgeni ambaye ameomba jina lake nilifiche, mgeni huyu aliomba tukatembelee shamba langu dogo la miti ya mitiki lililopo Kiluvya umbali wa kama km 30 kutoka jijini Dar es salaam. Shamba hili dogo (la mfano) lina ukubwa wa ekari mbili ambazo ziko bondeni, ni bonde lenye rutuba sana na sehemu ya bonde hili hutuamisha maji wakati wa mvua nyingi.
MGENI WANGU
CHINI YA MITIKI KUNA MPUNGA, HII NDIYO SEHEMU INAYOTUAMA MAJI NA HAINA MITI MINGI
Eneo la shamba hili kama likipandwa lote linauwezo wa kuchukua miti 1000 ila kwa sababu sehemu ya bonde hutuamisha maji basi kuna miti 800 tu, kwa sababu mitiki haiwezi kuota sehemu yenye kutuama maji (rejea makala zangu za mwanzo) Msimu huu wakati mvua zitakapokuwa zinaishia na bonde halituamishi maji, nitajaribu kurudishia hiyo miti 200 iliyobaki ili nione kama itashika, kwa sababu nina imani kama itashika mpaka mvua zijazo hata kama maji yatatuama haitakufa.
CHINI YA MITIKI KUMEPANDWA MIHOGO
Huyu mgeni wangu ni mkulima ambaye ana shamba lake kiasi cha ekari 50 sehemu za vigwaza unaingia ndani kulia kuufuata mto Ruvu. Hili shamba lake ni jipya na anategemea kuanza kupanda miti ya mitiki wakati wa mvua zamwezi wa 11, kwa sasa hivi anaanda shamba lake kwa kukata miti michache iliyopo pamoja na kulima vichaka na majani
CHINI YA MITIKI KUMEPANDWA MAHINDI
Ameniambia ataanza na ekari kumi kwa msimu wa kwanza kwa hiyo anahitaji kiasi cha miche 5000, kwa hiyo nina kibarua cha kuanza kuandaa kitalu cha kuoteshea mbegu hizo. Kitalu changu nitakiandaa kule kluvya kwa sababu ya urahisi wa kupitia miche wakati wa kupanda, yaani unangoa miche na kwenda kuipanda siku hiyo hiyo, nilimwomba tukatembelee shamba hilo ili niweze kujua vitu kama udongo unarutuba kiasi gani na je unatuamisha maji au la na kwa kaisi gani? Pili kujua kiasi cha mvua cha eneo husika kwa kuangalia uoto wa asili. Pia alikuwa anataka kujua kama anaweza kuchimba kisima cha asili na kukilinda kwa miti ya mikuyu.
9 comments:
Kaka Bennet kumbe we mtaalam sana wa mambo haya. Hongera SANA. Mi nina swali neno MITIKI linamaanisha nini?
Neno mitiki linatokana na jina la kiingereza la huo mti yaani TEAK (tectona grandis), kwa hiyo na sisi tukaiita hiyo miti mitiki, lakini sasa hivi baraza la Kiswahili wametoa jina la kibantu na kuiita hii miti MISOJI kwa hiyo TEAK (mitiki) = MISOJI
Oh kumbe Asante sana halafu nilipokuwa nyumbani nilliipanda hiyo mitiki/Teak = misoji mingi tu natumaini haijafa.
Hello Kaka,
Nimefurahi na nimekubali, kazi nzuri naamini nami nikija nitakuwa mgeni wako.
Hiyo miti ina miaka mingapi?
Naomba kujua
hongera kwa blog nzuri.Mimi nimepanda mitiki kama heka moja hivi maeneo ya zinga kule Bagamoyo,sasa nauliza hii miti huwa inakuwapruned au vipi maana mingine naona inatoa watoto pepeni je niitolee! mimi sina utaalaum wowote na ni binti aged 28yrs!!
Anonymous mitiki ni lazima ipunguziwe ili ubakie mti mmoja unaofaa kwa mbao ambao lazima unyooke, punguzia matawi yote kasoro yale ya juu juu tu
Nashukuru kwa ushauri wako,nategemea kwenda shamba kesho jumamosi nitajitahidi kufanya shughuli ya kutoe maoteo yote kwene mitiki kama ulivyonishauri! Thanks a lot!!
Kaka Bennet asante sana kwa darasa ngoja na mie nijapange vizuri mwakani nitakutafuta, bado naendelea kula shule hapa, ninaprint na kuzisomea home. Endelea na moyo huu.
Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe
nimekuwa nafuatilia threads zinazohusu kilimo na kuvutiwa na jinsi mnavyochangia-mfano Elnino na Malila na members wengine. naomba kuuliza kama nitaamua kulima MITIKI (teak wood). Sasa naomba mwenye utaalamu anisaidie kunielewesha yafuatayo:
1. Je unapotaka kupanda mitiki je mbegu zinauzwa wapi?
2. Je mbegu unazipanda kwenye vimfuko vidogovidogo na udongo wake (i.e kitalu). je mche unapotolewa kwenye kitalu unaupanda moja kwa moja shambani au kuna process nyingine?- i.e. yaani namaanisha hatua (steps) za kutoa kwenye kitalu kwenda shambani
3. Je unatakiwa kuweka umbali gani kati ya mtiki/mche mmoja na mwingine kama unataka ikue kwa ajili ya mbao.. na je spacing ni kiasi gani kama unataka ikue na uvune kama milingoti
4. Je kwenye ekari moja unaweza kupanda miche mingapi?
5. Je KIWASTANI inachukua miaka mingapi mpaka uvune kupata mbao na pili kupata milingoti
6. Je kuna paper au website ninayoweza kupata maelezo zaidi?
nitashukuru sana kwa mwenye kufahamu kunipa maelezo!
Post a Comment