BWAWA LA KUCHIMBA KWA AJILI YA SAMAKI WA CHAKULA
Ufugaji wa samaki ni kama ufugaji mwingine wowote wa wanyama, kwa sababu wanahitaji uangalizi kama wanyama wengine mfano vitu kama kula, usafi, tiba na mengineyo yote yanahitajika kwa ajili ya ufugaji wa samaki
VITU MUHIMU
Baada ya kuamua kufuga samaki ili kuchagua sehemu ya kufugia ni lazima uzingatie mambo yafuatayo
(a)MAJI- Ufugaji wa samaki unahitaji maji mengi ya kutosha kwa hiyo sehemu ya kufugia lazima iwe na chanzo cha uhakika cha maji kwa mwak a mzima, vyanzo kama ziwa, bwawa, mto, kisima ni vyanzo vizuri sana lakini maji ya bomba hayawezi kutumika moja kwa moja kwa sababu huwa yanatiwa dawa ya chlorine ambayo huua samaki. Ukitaka kutumia maji ya bomba ni lazima uyakinge kwanza sehemu kama kwenye matanki yakikaa kwa masaa kama 12 chlorine huondoka. Tatizo la maji ya mto, ziwa na bwawa ni maambukizi ya magonjwa kwa samaki.
BWAWA LA ASILI
(b)UDONGO- Sehemu utakayochagua kwa ajili ya bwawa lako la samaki lazima iwe na udongo unaotuamisha maji ili kuzuia upotevu wa maji na kupunguza gharama za uendeshaji, unaweza pia kujenga kwa simenti
(c)MAFURIKO-Sehemu ya bwawa isiwe ambayo inaweza kupatwa na mafuriko kila msimu wa mvua sababu samaki wataondoka na mafuriko, pia magonjwa na kemikali zisizohitajika zitaingia bwawani na kuua samaki wako
BWAWA LILOJENGWA KWA AJILI YA SAMAKI WA UREMBO
(d)JOTORIDI-Ni muhumu kujua aina ya samaki unaotaka kufuga kama wataweza kuishi kulingana na kiasi cha joto cha sehemu husika.
(e) MIPANGO YA BAADAE- Seehemu husika lazima iendane na mipango ya baadae hasa kama unampango wa kutanua ufugaji wako, ni muhimu mradi uwe sehemu moja kupunguza gharama za usimamizi
MFANO WA BWAWA LILOJENGWA KWA AJILI YA UZALISHAJI WA SAMAKI WA CHAKULA
3 comments:
Umenikumbusha mbali sana wakati wa ujana wangu yaani ule mwaka 47 kaka zangu walikuwa wanafuga samaki. Ilikuwa hivi tulikuwa tukiishi Nyasa na baadaye tukahama kutokana na kuzoea kula samaki haikuwezekana kwa hiyo wakachimba kisima na kuanza kufuga samaki. Safi sana.
Masangu Matondo Nzuzumilla aliniambia anataka kufuga samaki wa kula, sasa na mimi nikaona bora nimweleze kile kidogo ninachojua, nina imani atafanikiwa
samahan naomba niulize samaki gani ni wazuri kufuga kwajili ya chakula? na je wanastahimili mazingira gani naomba mnisaidie nahitaju kujfunza kutoka kwenu! pia samak huweza pata magonjwa gani na hutibiwa na nini?
Post a Comment