KURASA

Sunday, June 7, 2009

UTUPA - DAWA YA KUULIA WADUDU

Huu ni mmea unaopatikana zaidi sehemu zenye baridi na nyanda za juu na unastawi sehemu zenye mvua za wastani na nyingi, huwa hauhimili ukame. Ni mmea unaokua haraka na kusambaa kama usipodhibitiwa, baadhi ya nchi umepigwa marufuku kupanda kwa sababu ya kutishia uoto wa asili



MATUMIZI
KUFUKUZA PANYA / MCHWA

Kama shamba lako limevamiwa na panya wanaochimba ardhini, panda huu mmea pamoja na mazao mengine kwa umbali wa mita 3 kila upande (3m * 3m) na mpakani mwa shamba lako, baada ya mwaka mmoja shaba halitakuwa na mashimo ya panya. kwa njia hii hii pia utafanikiwa kufukuza mchwa, kwenye majumba unaweza kuupanda kwenye kingo za nyumba na mpakani, kama kuna kichuguu cha mchwa panda miche hii na kichuguu kitakufa baada ya mchwa kuhama.

KUOGESHEA MIFUGO
Chukua kiasi cha kilo moja ya majani ya utupa na maji lita 25 loweka kwa masaa mawili (2) mpaka matatu (3) au chemsha kwa dakika 30 na lita 27 za maji, chuja kwa kitambaa kisha weka kwenye bomba lakuogeshea changanya na sabuni ya unga kidogo ili iweze kunata kwenye mwili wa mnyama wako na hapo inakuwa tayari kwa matumizi ONYO usitumie kuogeshea nguruwe hawana uwezo wa kuhimili dawa hii kwenye ngozi zao




KUNYUZIA SHAMBANI / BUSTANI
Chukua kiasi cha kilo moja ya majani ya utupa na maji lita 5 loweka kwa masaa mawili (2) mpaka matatu (3) au chemsha kwa dakika 30 na lita 6 za maji, chuja kwa kitambaa kisha weka kwenye bomba na uanze kunyunyuzia shambani au majumbani kwa minajili ya kuua wadudu kama mbu, mende, n.k

KUHIFADHI NAFAKA KWENYE GHALA
Chukua gram 100 za unga wa majani ya utupa changanya na mahindi au maharage kilo 100, funga vizuri gunia lako na hifadhi kwenye ghala. Dawa hii huwa na nguvu kwa muda wa mwaka mzima.

MBEGU ZA UTUPA



MATUMIZI MENGINE
Mmea huu ukipandwa mchanganyiko na mazao mengine huongeza rutuba ardhini kwa kuongeza kiasi na naitrojeni, mbegu zake hutumika kama chanzo cha protini kwenye ufugaji wa mbuzi ila zisiliwe nyingi kwani ni sumu, Unga wa mbegu zake unauwezo wa kusababisha samaki wapooze (paralyze)unga wa utupa gram 1 na maji lita 2.5 hutumika kama dawa ya minyoo kwenye ngombe na mbuzi kwa kiwango cha 1cc kwa kilo 10 za mnyama,

9 comments:

chib said...

Kwa nini usiwe mshauri wa waziri wa Kilimo ndugu yangu?

Yasinta Ngonyani said...

Nashukuru kwa darasa hili. Ila ni kweli kwa nini usiwe kama kaka Chib alivyosema.

mumyhery said...

Hivi una shamba?

Bennet said...

Nashukuru sana Chid na Yasinta kwa kunipa moyo, ningepata nafasi ninauhakika ningeleta mabadiliko hata kama ningepewe kijiji tu.

Mumyhery nina mashamba tena mengi tu kwa hapa Dar nina kama jumla ya ekari zipatazo 20, na kwetu Tanga nina zaidi ya ekari 100 na bado nina kiu ya kuongeza zaidi

mumyhery said...

inaelekea hayo mashamba yako yanalipa sana kwani wewe mwenyewe ni mtaalam katika mambo ya mimea, nikija bongo ntakutafuta unipe maelezo kidogo kuhusu vibustani vyangu

mumyhery said...

inaelekea hayo mashamba yako yanalipa sana kwani wewe mwenyewe ni mtaalam katika mambo ya mimea, nikija bongo ntakutafuta unipe maelezo kidogo kuhusu vibustani vyangu

Bennet said...

Nashukuru Mumyhery ukija bongo tutafutate kwani naamini na mimi nitajifunza zaidi toka kwako

Unknown said...

Kuna Sina ngapi za utupa na huu utupa jina lake la kisansi ni lipi

Unknown said...

Asante kwa kutuongezea maarifa