KURASA

Sunday, August 30, 2009

MIKARATUSI NA UKWAJU - TIBA YA KIFUA

Mikaratusi na ukwaju ni tiba yenye nguvu dhidi ya kifua na kukohoa, tiba hii ni rahisi kuandaa na haina gharama.



UAANDAAJI
Chukua jani moja au zaidi ya mkaratusi lililokomaa kutoka katika matawi machanga/mapya ya mti, ponda ponda na uchuje kwenye maji kiasi cha mililita 100-200, unaweza kutumia blender pia kusagia dawa hii, kisha changanya na juisi ya ukwaju, pia unaweza kuongezea tangawizi kidogo ukipenda.


MATUMIZI
Kunywa mchanganyiko huu mara 3 kwa siku kwa siku 3-5
Ukitumia mchanganyiko huu mara moja kwa wiki ni kinga tosha kwa magonjwa ya njia ya hewa



MUHIMU Ukichemsha majani ya mkaratusi chumbani na kuacha mvuke usambae chumbani ni kinga tosha juu ya mafua, pia huleta harufu nzuri chumbani (air freshener)

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Oohhh! kaka Bennet nashukuru umerudi tena hapa kibarazani ume-missiwa naomba upite pale kwangu kuna mada inahusu ugonjwa wa ndizi kama utaweza kuwajuza wadau. Na asanmte kwa hili la leo dawa ya kifua.

Bennet said...

Asante kwa kunikumbuka na poleni kwa kunikosa kibarazani, sasa hivi niko busy sana na shamba kama unavyojua tunategemea mvua za el nino ingawa hazitakuwa kubwa sana, kwa hiyo utayarishaji wa mashamba ukianzia na miche ya kudumu, mifereji na usafishaji kwa jumla

Wakati wa mvua nyingi miche ya kudumu kama mitiki, michungwa, miembe, migomba n.k huwa inafaidika sana kwa sababu yenyewe haiathiriki na mvua nyingi ili mradi tu isiwe mabondeni maji yanakotuama

Anonymous said...

nimefurahi kukuona humu kwenye blog yako,jirani wangu wa sharifu shamba. mdau wa denmark

mumyhery said...

Shukran Mkuu