
Kuku hutoka kwenye kizazi kinachojulikana kitaalam kama
gallus gallus, Ufugaji huu nitaoelezea ni wa kienyeji kabisa ila huu umeboreshwa kidogo ili kuleta faida zaidi, kwanza itabidi uwe na eneo lakutosha kama ekari mbili
(70m *140m) banda la kuku liwe linalohamishika na liwe limejengwa juu juu, hii husaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa kwa sababu kinyesi cha kuku kikilundikana huweza kubeba vimelea vya magonjwa
BANDA BORA LINALOHAMISHIKA
Banda liwekewe viota vya kutagia na unaweza kuwafundisha kuku kuvitumia mapema kabla ya kuanza kutaga kwa kuchelewa kuwafungulia asubuhi. Kwa kawaida kuku hupenda kulala bandani wakiwa juu juu kwa hiyo uweke baadhi ya fito au mbao nyembamba zikining’inia pia kuwe na vyombo vya chakula nje ya banda
Hakikisha banda halivuji na wanyama wakali hawaingii lakini liwe na hewa ya kutosha na lisiwe na joto wala baridi kali, ni vizuri ukiliweka chini ya miti
Ili kuboresha ufugaji huu inashauriwa kutumia majogoo ya kisasa ambayo yana patika kwa mazalishaji wa kuku kote nchini, pia unaweza kutumia majogoo ya kuku aina ya
KUCHI wanaopatikana zaidi miko ya Singida na Shinyanga. Majogoo ya kisasa huweza kuhudumia wastani wa majike
20-25 na kuchi huweza kuhudumia majike
10 -15 kwa sababu ni wavivu kidogo
MAJOGOO YA KISASA INA YA CORNISH
Andaa na banda la kukuziA watoto ambalo litawakinga na wanyama wakali na mwewe, banda linakuwa wazi juu hukulikizuiwa na waya kwa
75% na
25% iwe imezibwa kwa mbao ili kuwapatia kivuli wanapohitaji, banda hili lina hitaji kuhamishwa hamisha angalau mara 5 kwa siku kutika mahali pamoja hadi pengine, hakikisha banda la watoto lina maji na chakula muda wote, pia kumbuka kuwawekea mabaki ya mboga za majani kama mchicha, kunde, kisamvu n.k
FAIDA(A) Mfumo hauhitaji chakula maalum kama kuku wa ndani
(B) Wadudu kama utitiri na virobot hushambulia kuku mara chache
(C) Kuku hupata muda wa mazoezi kwa kutembea tembea
(D) Gharama za uendeshaji ni kidogo
(E) Hautumii muda mwingi
(F) Kiasi cha uchafu ni kidogo
HASARA (A)Vifaranga huweza kuliwa na mwewe au wanyama
(B) Mayai huweza kupotea yakitagwa nje ya banda
(C)Kuku huweza kula mbegu zilizopandwa mashambani
(D)Vifo vya kuku ni vingi
CHANJOKuku wapewe chanjo ya kideri/mdondo kila baada ya miezi mitatu chanjo hii hupatikana nchini kote ukifika dukani ulizia chanjo ya
newcastle, utapata maelekezo ya jinsi ya kuwawekea kuku kwenye maji ya kunywa, chanjo hii wapewe kuku wazima tu na wagonjwa watengwe mbali
MINYOOKuku hunyweshwa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu, kuna dawa kama
piperazine na nyinginezo ambazo huwekwa kwenye maji
CHAWA NA UTITIRIUnaweza kutumia dawa za kuogeshea mifugo kama
ecotix au dawa ya unga unga ya kunyunyuzia kama
akheri powder, dawa ya akheri unaweza kuimwaga bandani na kisha kumnyunyuzia kuku mwilini ukiwa umemning’iniza kichwa chini miguu juu ili mayoya yaacha nafasi ya dawa kuingia
MAGONJWA YA MAPAFUKuna magonjwa mengi yanayoshambulia mfumo wa hewa, dawa ya
tylosin inauwezo mkubwa wa kupambana na magonjwa karibu yote, wape dawa hii mara tu unapoanza kuona dalili za mafua