Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Kama unataka kufanya kilimo, ufugaji wanyama, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki, kilimo cha miti ya mbao, kilimo cha majani na malisho ya mifugo, utaalamu wa mbolea na udongo katika mazingira halisi ya ki Tanzania basi wasiliana nami (mitiki1000@gmail.com) NB sihusiki na habari za masoko ya bidhaa yoyote ya kilimo na mifugo, kabla hujaingia kwenye mradi fanya utafiti wa masoko wewe mwenyewe
Saturday, October 3, 2009
KUKU WA KIENYEJI - UFUGAJI BORA
Kuku hutoka kwenye kizazi kinachojulikana kitaalam kama gallus gallus, Ufugaji huu nitaoelezea ni wa kienyeji kabisa ila huu umeboreshwa kidogo ili kuleta faida zaidi, kwanza itabidi uwe na eneo lakutosha kama ekari mbili (70m *140m) banda la kuku liwe linalohamishika na liwe limejengwa juu juu, hii husaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa kwa sababu kinyesi cha kuku kikilundikana huweza kubeba vimelea vya magonjwa
BANDA BORA LINALOHAMISHIKA
Banda liwekewe viota vya kutagia na unaweza kuwafundisha kuku kuvitumia mapema kabla ya kuanza kutaga kwa kuchelewa kuwafungulia asubuhi. Kwa kawaida kuku hupenda kulala bandani wakiwa juu juu kwa hiyo uweke baadhi ya fito au mbao nyembamba zikining’inia pia kuwe na vyombo vya chakula nje ya banda
Hakikisha banda halivuji na wanyama wakali hawaingii lakini liwe na hewa ya kutosha na lisiwe na joto wala baridi kali, ni vizuri ukiliweka chini ya miti
Ili kuboresha ufugaji huu inashauriwa kutumia majogoo ya kisasa ambayo yana patika kwa mazalishaji wa kuku kote nchini, pia unaweza kutumia majogoo ya kuku aina ya KUCHI wanaopatikana zaidi miko ya Singida na Shinyanga. Majogoo ya kisasa huweza kuhudumia wastani wa majike 20-25 na kuchi huweza kuhudumia majike 10 -15 kwa sababu ni wavivu kidogo
MAJOGOO YA KISASA INA YA CORNISH
Andaa na banda la kukuziA watoto ambalo litawakinga na wanyama wakali na mwewe, banda linakuwa wazi juu hukulikizuiwa na waya kwa 75% na 25% iwe imezibwa kwa mbao ili kuwapatia kivuli wanapohitaji, banda hili lina hitaji kuhamishwa hamisha angalau mara 5 kwa siku kutika mahali pamoja hadi pengine, hakikisha banda la watoto lina maji na chakula muda wote, pia kumbuka kuwawekea mabaki ya mboga za majani kama mchicha, kunde, kisamvu n.k
FAIDA
(A) Mfumo hauhitaji chakula maalum kama kuku wa ndani
(B) Wadudu kama utitiri na virobot hushambulia kuku mara chache
(C) Kuku hupata muda wa mazoezi kwa kutembea tembea
(D) Gharama za uendeshaji ni kidogo
(E) Hautumii muda mwingi
(F) Kiasi cha uchafu ni kidogo
HASARA
(A)Vifaranga huweza kuliwa na mwewe au wanyama
(B) Mayai huweza kupotea yakitagwa nje ya banda
(C)Kuku huweza kula mbegu zilizopandwa mashambani
(D)Vifo vya kuku ni vingi
CHANJO
Kuku wapewe chanjo ya kideri/mdondo kila baada ya miezi mitatu chanjo hii hupatikana nchini kote ukifika dukani ulizia chanjo ya newcastle, utapata maelekezo ya jinsi ya kuwawekea kuku kwenye maji ya kunywa, chanjo hii wapewe kuku wazima tu na wagonjwa watengwe mbali
MINYOO
Kuku hunyweshwa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu, kuna dawa kama piperazine na nyinginezo ambazo huwekwa kwenye maji
CHAWA NA UTITIRI
Unaweza kutumia dawa za kuogeshea mifugo kama ecotix au dawa ya unga unga ya kunyunyuzia kama akheri powder, dawa ya akheri unaweza kuimwaga bandani na kisha kumnyunyuzia kuku mwilini ukiwa umemning’iniza kichwa chini miguu juu ili mayoya yaacha nafasi ya dawa kuingia
MAGONJWA YA MAPAFU
Kuna magonjwa mengi yanayoshambulia mfumo wa hewa, dawa ya tylosin inauwezo mkubwa wa kupambana na magonjwa karibu yote, wape dawa hii mara tu unapoanza kuona dalili za mafua
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
16 comments:
kaka Bennet hapa darasa nzuri kweli ahsante sana.
Ningependa kufahamu kwanini banda la vifaranga lihamishwe mara 5 kwa siku. Hii inasaidia nini?
Pia imeelezwa kwamba moja ya hasara ni kuwa "Vifo vya kuku ni vingi". Ufafanuzi unahitajika hapa.
Katika kuku 50, wangapi wanaweza kufa? Au hapa inazungumziwa uwezekano wa kuku wote kufa kwa mkupuo kutokana na magonjwa ya mlipuko?
LD karibu sana kwenye kijiwe hiki
Banda linatakiwa lihamishwe mara 2 tu ila kwa sababu watu ni wavivu nawaandikia 5 ili hiyo mara mbili ipatikane,Unaweza pia usilihamishe ila hakikisha kila siku linakuwa sehemu mpya na usilirudishe sehemu lilikopita mpaka baada ya siku 15
Kuhusu vifo vingi ni kwamba wanyama kama kicheche, kanu, nyegere, mbwa koko, kenge na hata mwewe ndio wanaoasababisha vifo vingi, pia wengi wanakuwa wavivu kuwapa chanjo hasa sehemu za vijijini
Hongera kwa elimu utoayo katika blog yako. Mimi ni miongoni mwa wakulima walioitikia kilimo kwanza.
Kaka hii mada ya kuku imenisaidia sana maana mimi ndio nimeanza ufugaji wa hawa kuku wa kienyeji kwa ari na kasi zaidi. Sasa any ideas ya maeneo nitakayopata majogoo ya kisasa yenye rangi tofauti kwa ajili ya kupandisha mikoo? Also vipi unafaham soko la kuku na mayai ya kienyeji hapa DSM?
:Kaka Ben,web yako ni nzuri na ninavutiwa na jinsi unavyojishughulisha na usivyo mchoyo wa maarifa kwa watu wengine.
Swali langu ni kwamba,banda linapokuwa juu juu,ni kitu gani kinachotumika kuwekwa chini ili kinyesi cha kuku kidondoke chini,na kuku wenyewe wawe comfortable kurandaranda ndani ya banda.Au hilo banda ni la kulala tu?
PILI ni ushauri au maoni,mmea wa alovera ukipondwa na kuchanganywa katika maji ya kuku huwa ni dawa nzuri sana kwa magonjwa mbalimbali ya kuku.
Kama kuna watu wanaweza fanya research zaidi itakuwa vizuri kisha watupe majibu ndani ya blog hii.
BIG UP BEN.
Hii ni changamoto nzuri sana katika kuinua na kurekebisha maisha ya mfugaji mdogo. Nami natoa mafunzo ya ufugaji bora darasa lipo kila jumamosi mahala ni Tarakea house Mwenge area. Karibuni wote. George Shao 0652402665
Mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji sasa naomba unipe formula ya kutengeneza chakula cha kuku wa kienyeji,chakula ready made kimekuwa cha bei sana.
Mimi ndo naanza ufugaji nilikua naomba utupe formula ya kutengeneza chakula cha kuku; ukianza na vifaranga mpakakuku wakubwa.
Mimi ndo naanza ufugaji nilikua naomba utupe formula ya kutengeneza chakula cha kuku; ukianza na vifaranga mpakakuku wakubwa.
Aksante sana kaka mimi binafsi nashukuru kwa elimu hii
Nimeipenda hii
nimependa uelimishaji wako nami naanza kutumia elimu uliyonipa
nashukuru kwa somo lako kaka vipi mtu anaweza kuchukua au kununua kuku matetea makubwa yani yaliyo anza kutetea au yanakaribia na nikawawekea na hayo majogoo ya kisasa ili waendelee kutaga je nitafanikiwa kama ilivyo ukianza nao?kama hapana ni kiasi gani inhathiri ufugaji?
asante
Bennet, salute kwako mkuu
Nimekuwa na imani moja ya kazi zitakazotupa unafuu wa maisha na kuongeza vipato kama sio kutajirika ni kilimo..sababu ni moja tu watu tunaongezeka wakulima wanapungua, nani atatulisha?
Kilichonifanya nipitie mitandao ni kutaka kujua/uzoefu kuhusu matatizo yanayonikabili katika ufugaji wa kuku wa kienyeji;
1. kuhusu magonjw na matibabu
2. Kuhusu tabia za kuku na namna ya kuzithibiti.
kwenye la kwanza kwa ujuzi/uzoefu wako ni magonjwa yapi yanayowakabili hawa kuku wa kienyeji na matibabu yake?
kwenye la pili kuku wangu kadili wakuavyo wamekuwa wakionesha tabia ambazo kwakweli ni zinanitia wasi wasi kuwa iko siku wanaweza hata kuuana Kupigana kwa majongoo; sasa basi nini nifanye kukabiliana na haya?
Msaada wako kaka...
@Stans Mpemba -
1- Kuhusu magonjwa ya kuku ugonjwa mkuu kwa kuku wa kienyeji ni Mdondo ndenda kwenye maduka ya pembejeo upate chanjo yako kila baada ya miezi mitatu.
2- Punguza majogoo yako kwani jogoo moja la kienyeji linatosha kwa watetea 10 - 15
Post a Comment