TANGA
MANYARA

RUKWA
RUVUMA

Hivi mnategemea kwa kutumia barabara hizi mkulima ataweza kweli kusafirisha mazao yake na kuyapeleka mjini kwenye masoko au mazao hasa yale yanayooza haraka kama matunda na mboga mboga si yataharibikia shambani.
Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Kama unataka kufanya kilimo, ufugaji wanyama, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki, kilimo cha miti ya mbao, kilimo cha majani na malisho ya mifugo, utaalamu wa mbolea na udongo katika mazingira halisi ya ki Tanzania basi wasiliana nami (mitiki1000@gmail.com) NB sihusiki na habari za masoko ya bidhaa yoyote ya kilimo na mifugo, kabla hujaingia kwenye mradi fanya utafiti wa masoko wewe mwenyewe
4 comments:
Heri na wewe kakangu. Ahsante kwa taswira nzuri, Hiyo picha ya mwisho ya Ruvuma naikumbuka ni njia ya kwenda Mbamba-by. Duh sehemu hizo mtu unaenda kama ni lazima uenda la sivyo mmmmmhhhhh!!
Ndio tanzania yangu niipendayo. Wakati watu wanakufa njaa upande wa pili wa barabara, wengine wanaozewa na mazao. Niliwahi kuandika kuhusu jambo kama hili hapa http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/02/tanzania-yangu-niipendayo-barabarani.html
lakini kwa taswira hizi mwanana ntaomba kuziongeza kisha niirudie makala kwani makala zetu hazi[itwi na muda kama hazijatekelezwa.
Blessings
Kweli mwenda kwao si mtoro Dada Yasinta unapajua kwenu hata kwa kupapasa tu,
Mzee wa changamoto tumia tu hizi picha ndio maana sikuzipiga mihuri kwa sababu nilihisi zinaweza kutumika maradufu
Ukizikuta kwangu usishangae mkuu.
Na mvua hizi za sasa, nafikiri kuna sehemu zitageuka visiwa vya muda
Post a Comment