KURASA

Monday, May 31, 2010

KILIMO CHA PILIPILI MANGA


Utangulizi

Jina la kitalaam ni Piper nigram na kwa kiingereza ni black pepper. Zao hili asili yake ni Mashariki ya Mbali, na linalimwa zaidi katika mkoa wa Tanga na Zanzibar.

Matumizi
Pilipili nyeusi na nyeupe zote hutumika kwa mapishi ya nyama, samaki na kwa mapishi mengine mbalimbali. Nchi za magharibi zina matumizi makubwa ya viungo hivi. Aidha pilipili mtama nyeusi ndiyo huzalishwa zaidi hapa nchini.

Uzalishaji
Hali ya hewa na udongo
Viungo vingi humea katika maeneo yenye joto la wastani kati ya nyuzi joto 24-26 na huzalishwa maeneo ya mwambao. Udongo wenye rutuba na unaopitisha maji na wenye uchachu wa kiasi cha pH 6.5. Mahitaji ya mvua ni mililita 1500-2000 kwa mwaka.




• Uchaguzi wa mbegu
Uchaguzi huzingatia mambo yafuatayo:-
a) Urefu wa pingili na ukubwa wa majani
b) Ufupi wa pingili unaoambatana na majani madogo.
Tofauti iko hadi kwenye umbile la matunda. Majani ya mche mama sehemu kinapokatwa kipando huondolewa wiki mbili kabla ya kukata. Vipando vyenye macho (nodes) 3-4 humika. Macho mawili huzikwa kwenye udongo na kipando kiwekewe kivuli. Inashauriwa kuweka mbolea ya samadi wakati wa kupanda.

• Nafasi ya upandaji
Nafasi ya kupanda ni mita 2-3 kati ya mmea na mmea endapo miche imepandwa na miti inayotakiwa kupogolewa mara kwa mara.

Mahitaji ya mbolea
Matumizi ya mbolea hapa Tanzania si makubwa katika kilimo cha viungo. Ingawa kiasi cha kilo 0.4 cha Urea, kilo 0.3 cha Superphosphate na kilo 0.3 cha Potash ya Muriate kinaweza kutumika kwa miche mikubwa.

• Miti ya kusimikia miche

Miche hupandwa kwa kusimikiwa nguzo ili ikue kwa kujizungusha kwenye miti kama mijenga ua, n.k. Mti huo wa kusimikia nao pia hupaswa kupunguziwa majani ili kupunguza giza. Kila kabla ya msimu miti hiyo hupaswa kupunguziwa matawi (pruning).

Kupogolea miche ya pilipili mtama
Mche ukifikia miezi 18 inapaswa kupogolea kwa kukata sehemu ya juu ya mche ili kufanya matawi mengine yachipue chini ya mche. Inashauriwa mche kuwa na urefu wa mita 3-3.5.

Uvunaji
Maua ya kwanza hutoka baada ya miaka miwili. Matunda hukomaa miezi tisa (9) hadi kumi (10).
Uvunaji ni mizunguko 5 hadi 6 kwa mwaka. Pilipili mtama inaweza kuvunwa kwa misimu miwili. Mavuno ni kati ya tani 0.35-3.75 kwa hekta.

Kuhifadhi
Pilipili mtama inaweza ikawekwa kwenye chombo kisichopitisha hewa na kudumu kwa miaka 20 bila kuharibika.

Mashambulizi ya wadudu na magonjwa
Hapa nchini hakuna matatizo makubwa ya wadudu na magonjwa.

Masoko
Soko la pilipili matama linapatikana ndani ya nchi na nje pia. Bei ya ndani ni kati ya Sh1,000-1,500. Zao hili huuzwa katika nchi za Uganda, Kenya, Uingereza, Ujerumani, Mashariki ya Kati, n.k. Bei ya Nje ni wastani wa dola za kimarekani 1,985 kwa tani.

15 comments:

Anonymous said...

Mkuu nashukuru sana kwa somo hili,kweli unastahili pongezi kwa juhudi zako za kuelimisha umma kuhusu kilimo.
Swali langu:ni muda gani wa mwaka ambao unafaa kwa kupanda pilipili manga?je kama natumia kilimo cha umwagiliaji naweza kupanda muda wowote au inabidi pia kuzingatia wakati wa mvua?shamba langu liko morogoro na ningependa kupanda pilipili manga.asante

Bennet said...

kama una maji ya kumwagilia huna haja ya kufuata misimu wewe panda muda wowote tu

Unknown said...

hello

kilo ya pilipili manga kwa kilo itakua sh ngapi saiv apa dar?

kama unafahamu..

thanks

Unknown said...

SHUKRAN SANA KAKA..
KWA SOMO.

BEI YAKE YA NJE KWA SASA NI SH. NGAP?
TUTAPATAJE SOKO LAKE LA NJE?

MIKOA MINGINE MBALI NA UFUKWEN
INAFAA KUOTESHA?

KWA HEKARI MOJA UNAWEZA KUVUNA KIASI GANI?

UBARIKIWE KULIKO WANAUME WOTE DUNIANI ASANTE.

Unknown said...

Mimi nataka tani 20 wapi nitapata na kwa sh napi nataka kusafrisha nje

Unknown said...

Sh Ngapi

Unknown said...

bei yake ni 10000-15000

Unknown said...

0785831234 my name is Brendan,pilipili manga,vitunguu maji,carrot,pilipili,nyanya.

4d said...

Wapi naezapata mbegu... nataka nilime Songea je inaweza kustawwì

4d said...

Kwa msaada wowote please write to me through..

jfshaurì@yahoo.com
0712818484
0788828787
0756828787

Nguvila the son said...

Jamaa yuko vizuri sana. Safi sana.

Nguvila the son said...

Jamaa yuko vizuri sana. Safi sana.

4d said...

Kilimo kinalipa...

4d said...

Kilimo kinalipa...

Unknown said...

Bwana Shauri naomba tujuze cost zake za kulima kwa heka..?