UTANGULIZI
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu
MABANDA
Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura.
UFUGAJI WA NDANI
1 - Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha
2 - Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa kuzimeng'enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa
3 - Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri
4 - Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi
5 - Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao, box gumu au plastiki
UFUGAJI WA NJE
1 - Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk
2 - Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika
3 - Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali
4 - Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone wataalamu wakushauri au ng'oa yote)
MAJI
Tumia mabakuli ya kigae, usiweke vya plastiki maana huvitafuna na kuwaathiri au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku
CHAKULA
Wapewe majani makavu kwani muhimu sana kwa ajili ya mfumo wa kumeng'enya chakula, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho (concentrates) Kiasi cha protini wanachohitaji ni 17%
USAFI
Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watoto
MENO
Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu wakati wa kula, waone wataalam ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12
MIGUU
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake zinahitaji kupunguzwa zikikua sana waone maofisa ugani wa mifugo wakusaidie kwa hili
UBEBAJI
Usimbebe kwa kutumia masiki yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba na pia weka mkono mmoja kwa chini ili kusapoti uzito
DAWA
Wapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe kwenya mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa kama nilivyosema mwanzo
52 comments:
kaka bed twakushukuru sana kwa elimu yako tunauhitaji mchango wako sana
sawa sawa mtaalam kwanini tutumiye taula iliochoka huoni ni unyayapaa duhudumiye wanyama kama tunayvowahudumiya watoto wetu kwani hao wanahitaji huruma na upendo
Nashukuru Anony 5:41 na anany 6:52 ni kweli tuwape mataulo mapya kama hali inaruhusu,
Kwa faida ya wote kuna mdau ameniuliza afanye nini sungura wake wana viroboto na fangas jibu ni hili
Nashukuru na pole sana kwa kusumbuliwa na viroboto, nenda kanunue dawa ya unga inaitwa akheri powder nyunyuzia bandani na uwanyunyuzie sungura, pia unaweza kutumia dawa yoyote ya unga ya kuzuia viroboto wa paka, kwa ajili ya mba, ukurutu na fungusu anunue dawa inaitwa IVEMECTIN ni ya kuchoma kwa sindano lakini wewe dondoshea tone moja tu na ulipake sehemu iliyoathirika kama sehemu ni kubwa unaweza kuongeza tone lingine, ukiweka nyingi watakufa
kaka ben asante sana kwamsaasa wako MUUGU AKUBARIKI
hujaelezea masoko yao, ninaweza kuwauza wapi?
Asante sana kwa ushauri wako. Mimi nafuga sungura aina ya white german. Hivi sasa ninao sungura zaidi ya ishirini, lakini mara kwa mara wanapozaa hawatambui watoto wao wala kuwanyonyesha. pia hawana utamaduni wa kuandaa sehemu ya kuzalia hadi siku anapozaa ndo anajinyonyoa manyoya kidogo sana. Nifanye nini maana naona ni usumbufu sana kuwashika wanyonye kila mara. Pia naomba ushauri maana kasi yao ya kuzaliana ni kubwa hivyo wakiwa wengi watanishinda kuwahudumia mfano kwenye unyonyeshaji.
Pole sana dada Lucy kwa matatizo ya sungura wako. Kwa kawaida Sungura huandaa kiota siku chahche kabla ya kujifungua na hunyonyesha watoto wake asubuhi sana na jioni baada giza kuingia kwa kujificha sana, hunyonyesha kwa kujificha kutokana na mazingira ya asili porini ili kujikinga na maadui kwa hiyo tabia hii huendelea hata kwa sungura wa kufugwa ingawa si wote
USHAURI
1 - Angalia saizi ya mabanda yako kama iko sahihi na ukubwa wa sungura wako, kwa ninavyowajua German white\giants ni sungura wakubwa kwa umbo kwa hiyo saizi ya banda lazima iwe kubwa
2 - Lisha mlo kamili unaweza kutumia chakula cha kuku GROWERS MASH kama chakula cha ziada
3 - Epuka kuzaana ndugu kwa ndugu (inbreeding) kwani pia hujenga tabia hii kwa majike, itabidi ubadili majike na baada ya vizazi kadhaa utabadili pia madume ili yasizae na watoto wao
Aksante
Mimi napenda kufuga sungura, nipo dar nitapata wap sungura wa mbegu nzur na bei zao pia ningejua na gharama za matunzo yao. Asante.
By Eng. Amossy Itozya
Asante sana kwa ushauri mzuri, kwani nimenunua sungura wawili ili nianze nao hivyo nimepata elimu nzuri jinsi ya kuwafuga, ila mnaandika comments hamtoi contact zenu ili tuweze kujenga hii network vizuri.
My contact: 0757-390-4747/0713-266008/0732266008
email: amossyi@yahoo.co.uk/amossy.itozya@gmail.com
Nami ninao wawili naanza nashkur kwa somo
Nami ninao wawili naanza nashkur kwa somo
Vipi kuhusu kuzaliana ni kila baada ya muda gani
kuna aina ngapi za sungura.
na ni sungura gani huzaa kwa wingi
Elimu nzuri tunashukuru mdau
Lucy pole sana napenda kuongezea watoto wakizaliwa ukiwashika mikono yako iwe misafi isiwe na harufu yoyote wakinukia harufu ambayo mama haitambui anajua sio wake hawezi kuwanyonyesha
Kaka Bennet, hongera sana!
..maelekezo yako yapo juu ya mstari!
Nakushkuru pia kwa kuniengezea elim,
+255785989666
fhm.battashy@gmail.com
Nimependa somo hili nahitaji kufuga sungura je nitawapataje pia ningependa mwalimu uweke number zako za simu ili iwe rahisi pia e mail ni bora zaidi
Asante sana kwa mafunzo mazuri. Je naweza kupata picha ya banda zuri la sugura? Ninao sungura lakini naona hawana maendeleo mazuri. Wengine wananiamiaba sababu banda langu halina hewa ya kutosha. Wengine wanasema mbegu niliyonayo sio nzuri n.k
Hongera Kwa elimu nzuri sana. Ningeomba anayejua Friday inayopatikana kwa ufugaji wa sungura atushirikishe. Ningependa kujua aina gani ni nzuri, inapatikana wapi? Masoko yapo wapi? Nk
Hongera Kwa elimu nzuri sana. Ningeomba anayejua Friday inayopatikana kwa ufugaji wa sungura atushirikishe. Ningependa kujua aina gani ni nzuri, inapatikana wapi? Masoko yapo wapi? Nk
Asanteni ndg...maelezo yenu yamenisaidia.
Habarini za jmos. Mimi nafuga sungura weupe ninao wachache kama 7 lkn tatizo kubwa ni hawa sungura kuchafuka na manyoya hubadilka na kuwa na rangi ya kahawia. Sijui ni kitu gani huchangia kuchafuka kwao maana ule mvuto wa sungura mweupe unaisha kabisa anapofikia hali hii ya uchafu.
Asante kwa elimu me ninasungura naona maendeleo mazuri napenda kujua Soko kwa ulaya na china
Naomba kama kuna group niwe add 0763370175 na anaeitaji sungura
nahitaji mbegu nzuri na ya kisasa ya sungura.nawapata wapi hapa dar es salaam.0658106568
nahitaji sungura namba yangu ya simu ya mkononi ni 0763299231 nipo Dar es Salaam.
Jaman kiukweli sungura ninao wengi na wakisasa na wanazidi kuzaliana nahitaji soko kubwa zaidi ya hili nililo nalo mm ni mwanachuo lakini ni ujuzi mzur wa matunzo lishe na dawa za sungura pamoja na aina yote pia yako katika somo contact me 0754295529 au 0657191921
Nimepata kitu leo na naaidi kuyafanyia kazi hayo yooote mlioleza.. my contact 0714343737 na email fahadisalum55@gmail.com
wapi naweza pata soko zuri la sungura? maana nimevutiwa nao na nataka nianze kufuga so nataka nilijue soko kwanza...my contact 0654 853020
Nami ninao watano na watoto watano
Nami ninao watano na watoto watano
Nipo nami katka mchakato WA kuanza Naomba msaada wenu +2557441463
Naitwa lulu, nipo dar nimeshawishika kufuga sungura pia lakini cjui wap ntawapata na uangalizi wao
Nataka mbegu ya kisasa na sungura wenye manyonya mengn nambar yangu 0716549305
Mkuu asante kwa elimu unayoitoa..Mimi Nina tatizo sungura wangu wamezaa na watoto wana miezi miwili lakin wanakufa ghafla ghafla tuu....unaweza kuta wanakula vizuri jion asubuhi ukiamka unakuta hata wawil wafu bandani....vipi tatizo ni nin?
Nimeanza kufuga Australian type na ninao dume mmoja na jike wawili. Nimempandisha jike mmoja wiki jana.
Nilinunua mbugu hii Morogoro chuo cha mifugo (TIA)Boma road.
Ukitaka sungura wako weupe wabaki na rangi yao nzuri hakikisha banda lao linakidhi viwango vya usafi, mfano: kutumia wavu kama sakafu ya banda. Njia hii inasaidia kinyesi na mkojo kutokubaki kwenye banda. Vinginevyo uwe na banda lenye ukubwa wa kutosha kiasi kwamba sungura watachagua eneo moja la kujisaidia na eneo kavu la kujipumzisha. Kwa hali hii nawe wapaswa kutenga eneo moja kwenye banda ambapo utakuwa ukiweka chakula chao na maji.
Kwa hali hii sungura wataishi kwenye hali ya usafi.
0717151125
eplema@gmail.com
Nimeanza kufuga Australian type na ninao dume mmoja na jike wawili. Nimempandisha jike mmoja wiki jana.
Nilinunua mbugu hii Morogoro chuo cha mifugo (TIA)Boma road.
Ukitaka sungura wako weupe wabaki na rangi yao nzuri hakikisha banda lao linakidhi viwango vya usafi, mfano: kutumia wavu kama sakafu ya banda. Njia hii inasaidia kinyesi na mkojo kutokubaki kwenye banda. Vinginevyo uwe na banda lenye ukubwa wa kutosha kiasi kwamba sungura watachagua eneo moja la kujisaidia na eneo kavu la kujipumzisha. Kwa hali hii nawe wapaswa kutenga eneo moja kwenye banda ambapo utakuwa ukiweka chakula chao na maji.
Kwa hali hii sungura wataishi kwenye hali ya usafi.
0717151125
eplema@gmail.com
Kaka sungula wangu amezaa ila sijui kuwaudumia maana sioni hata kuwanyonyesha wala nn
Sungura anapatwa kama kichaa anakimbia kwa nguvu sana ndani ya dakika then anaishiwa nguvu anaanguka na kukakamaa akijinyoosha na kupiga kelele,bdae anatulia na kupoteza fahamu baada ya dakika kama tano anazindika, ni nini tatizo ? Je nimpe dawa gani?
Pia alijipukutua manyoya kama anazaa lkn sijawahi kuwaona watoto wake
Namba yangu 0712 258005
Pia naomba kuelimishwa dalili za minyoo kwa sungura na dawa mzuri
Unao wa aina gani?
Safi sana your ryt nime experience
Habari yako mkuu,nimeyapenda sana mafunzo yako mungu akubariki,naitaji kuanza kuanza kufuga sungura je,ni aina gani nzuri ya kuanza nayo?
Habari yako mkuu,nimeyapenda sana mafunzo yako mungu akubariki,naitaji kuanza kuanza kufuga sungura je,ni aina gani nzuri ya kuanza nayo?
Asante kwa somo mzuri Mimi kila baada ya mwezi na nusu wanazaa ila kuna mtu aliniambia sungura awanywi Maji je nikweli,
Safi ushauri mzuri
Asante Sana kwa ushauri nahutaji mbegu dume na jike rangi nyeupe macho mekundu napatikana segerea mwisho dar saalam 0746334063
Naitaji sungura was kisasa namba yangu ni 0717565742
Post a Comment