KURASA

Monday, September 27, 2010

SIKU YA KICHAA CHA MBWA DUNIANI

Kila mwaka tarehe 28 ya mwezi wa tisa (september) ni siku ya kichaa cha mbwa duniani, hapa nchini serekali katika kampeni ya siku hii maalum imetoa kiasi cha chanjo 100,000 bure kwa mafugaji mbwa katika mikoa ta Dar es salaam, Mtwara, Lindi na Pemba

kutokana na takwimu za wizara ya mifugo na uvuvi inaonyesha mwaka jana watu 21,000 walingatwa na mbwa nchini Tanzania. Kati ya hao watu 51 walifariki dunia kwa sababu ya kichaa cha mbwa.

Ingawa kwa kiswahili ugonjwa huu unaitwa kichaa cha mbwa, lakini ukweli hushambulia hata wanyama wengine kama paka, ng'ombe, mbuzi, kondoo na hata binadamu, Ugonjwa huu kwa wanyama hauna dawa ila kinga tu kwanjia ya chanjo

Kuuelewa zaidi ugonjwa huu soma hapa
http://mitiki.blogspot.com/2009/08/kichaa-cha-mbwa.html

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni jana tu nimesikiliza kwenye habari hapa ya kwamba pia idadi ya mbwa vichaa na watu waliongátwa na mbwa imeongezeka sana. Je? inawezekana ni dunia nzima ipo hivyo. Sasa hii siku ya kichaa cha mbwa duniani huwa kinafanyika nini hasa??

emu-three said...

Mhhh, kichaa cha mbwa, na hakina dawa ila chanjo...mmmh, aisee, nakumbuka mbwa wetu alipigwa shaba na bwana shamba eti kuzuia kichaa cha mbwa, wakati huo nikiwa mdogo, iliniuma sana...
Haya magonjwa yanatokana na nini hasa...manake ukiangalia yanaendana na ndui...
Basi tukiwafuga hawa wanyama, tukumbuke kuwachanja, manake inatia hutuma...