Kuchagua matunda ya
mlimao kutoka kwenye mti mama
Chagua na kuvuna
malimao yaliyoiva vizuri. Usitumie malimao yaliyooza.
Miche ya milimao ndiyo imekuwa ikitumika sana kama miche shina kwa ajili ya kuunganisha michungwa na miti ya matunda ya jamii yake kama vile michenza, midimu, madalanzi, mawashington nk.
Aina nyingine ya mmea shina kwa ajili ya kuunganisha michungwa na miti ya matunda ya jamii yake ni Karizo na Volkameriana. Aina hizi bado ni ngeni kwa watu wengi.
Miche ya milimao ndiyo imekuwa ikitumika sana kama miche shina kwa ajili ya kuunganisha michungwa na miti ya matunda ya jamii yake kama vile michenza, midimu, madalanzi, mawashington nk.
Aina nyingine ya mmea shina kwa ajili ya kuunganisha michungwa na miti ya matunda ya jamii yake ni Karizo na Volkameriana. Aina hizi bado ni ngeni kwa watu wengi.
Kukamua na kundaa
mbegu za malimao.
Kata tunda kwa
mzunguko bila kuingiza kisu hadi katikati ya tunda ili kuepuka kukata mbegu.
Kamua mbegu zote kutoka kwenye tunda na ziweke kwenye chombo kisafi. Safisha mbegu ili kutoa utelezi wote (utelezi unazuia uotaji mzuri wa mbegu).
Chagua nbegu zinazozama kwenye maji kwani mbegu zinazoelea juu ya maji hazioti.
Mbegu za malimao zipandwe mara tu baada ya kusafishwa kwani kwa kufanya hivyo mbegu zinaota vizuri zaidi kuliko mbegu zinazokaushwa kwanza kabla ya kupanda.
Kamua mbegu zote kutoka kwenye tunda na ziweke kwenye chombo kisafi. Safisha mbegu ili kutoa utelezi wote (utelezi unazuia uotaji mzuri wa mbegu).
Chagua nbegu zinazozama kwenye maji kwani mbegu zinazoelea juu ya maji hazioti.
Mbegu za malimao zipandwe mara tu baada ya kusafishwa kwani kwa kufanya hivyo mbegu zinaota vizuri zaidi kuliko mbegu zinazokaushwa kwanza kabla ya kupanda.
Kuandaa tuta na
kupanda mbegu za malimao
Andaa tuta lenye kimo
cha sentimeta 20. Tumia udongo
unaopitisha maji kwa urahisi ( udongo wa kichanga au mchanga wenyewe ni bora
zaidi). Sawazisha vizuri
sehemu ya juu ya tuta.
Kupanda mbegu za
malimao:
Weka alama za mistari
kwenye tuta kwa nafasi ya sentimeta kumi (10) mstari hadi msitari (alama hizo
ziwe na kina cha sentimeta moja na nusu (1.5) hivi. Panda mbegu kwa
kuzidondosha moja moja kwenye mstari kwa nafasi ya sentimeta moja (1). Fukia mbegu kwa
kurudishia udongo wa pembeni ya mstari. Mbegu za limao zinaota
siku ishirini na nane au zaidi toka siku ya kupandwa.
Kupandikiza miche
shina ya milimao
Miche ya milimao ina
pandikizwa ikiwa na majani mawili yaliyokomaa. Jaza udongo kwenye
kiriba ukiacha nafasi ya sentimeta mbili juu kwa ajili ya kumwagilia maji. Ng'oa miche bila
kuharibu mizizi.
Pandikiza miche iliyo bora tu. Tumia kijiti au kifaa maalumu kuweka shimo katikati ya kiriba.
Weka mche kwenye shimo na shindilia udongo vizuri.
Zingatia kwamba mmea unaweza kuathirika endapo udongo utafukiwa juu sana ya sehemu linalotenganisha mizizi na shina.
Pandikiza miche iliyo bora tu. Tumia kijiti au kifaa maalumu kuweka shimo katikati ya kiriba.
Weka mche kwenye shimo na shindilia udongo vizuri.
Zingatia kwamba mmea unaweza kuathirika endapo udongo utafukiwa juu sana ya sehemu linalotenganisha mizizi na shina.
Kutunza miche shina ya
mlimao
Ondoa matawi ya
pembeni kila mara yanapojitokeza. Dhibiti wadudu na
magonjwa kila vinapojitokeza.
Miche wa mlimao inakuwa tayari kwa kuunganishwa inapofikia umri wa miezi sita (6) hadi miezi tisa (9) (hutegemea matunzo). Mche unakuwa kwenye hatua nzuri ya kuunganishwa unapofikia unene wa penseli.
Miche wa mlimao inakuwa tayari kwa kuunganishwa inapofikia umri wa miezi sita (6) hadi miezi tisa (9) (hutegemea matunzo). Mche unakuwa kwenye hatua nzuri ya kuunganishwa unapofikia unene wa penseli.
NAMNA YA UUNGANISHAJI MICHE JAMII YA MICHUNGWA
KWA KUTUMIA MKATO WA HERUFI T
KWA KUTUMIA KIPANDE
Kutunza miche
iliounganishwa
Mwagilia maji mara kwa
mara kuhakikisha kuna unyevu wa kutosha wakati wote.
Ondolea machipukizi
chini ya sehemu iliyounganishwa ili chakula cha mmea kitumike kwenye sehemu ya
juu
iliyounganishwa tu
Baada ya siku 14 hadi
21 mmea huwa tayari umesha ungana na mara nyingine vitawi kuchipua.
Kwa miche ya jamii ya
michungwa huu ni wakati wa kufungua utepe/plastiki.
Kwa miche ya miembe
baada ya kitawi kuchipua na kufikia majani manne yaliyokomaa ondoa utepe
/plastiki kwa kuifungua polepole (utepe unaweza kufunguliwa mapema endapo
utakuwa unaonekana kuuzuia mche kukua).
Tangu kubebesha hadi
kupandikiza huchukua wastani wa miezi 3 hadi 6.
Ni vema kupandikiza
mwanzo wa majira ya masika.
Mti uliobebeshwa
unauwezo wa kutoa maua wakati wowote baada ya kuunga. Lakini si vema kuuruhusu
uzae mapema kwani utadumaa.
Mti uruhusiwe kuzaa baada
ya kupata ukubwa wa kutosha Kwa hali ya kawaida hii ni baada ya miaka mitatu.
Wadudu na magonjwa ya
miche ya mitunda kitaluni
Wadudu na viumbe wengine jamii ya
buibui, jamii ya minyoo wadogo wadogo na magonjwa vinavyoweza kuleta madhara
kwa miche kwenye kitalu.
Wadudu waharibifu
i. Chawa mfuta
Hushambulia miche ya
milimao, miembe na mchungwa kitaluni na bustanini.
Hufyonza utomvu kutoka
sehemu changa za mmea na majani.
Wadudu hawa hutoa maji
maji yenye sukari ambayo huvutia vimelea vya ukungu mweusi kutokea kwenye
majani na hivyo kuathiri shughuli za
utengenezaji wa chakula cha mmea.
Kuzuia
Kuna wadudu wadogo
wadogo wenye umbo la kobe wanaokula chawa mafuta. Jamii hii ya wadudu huonekana
pia kwenye maboga.
Kama wadudu hawa
wanaleta madhara unaweza kutumia dawa za kuulia wadudu kama vile Endosulfan
(Thiodan), Diaziozon, Fenitrothion, Karate na Decis.
Pia tumia mbegu za
mwarobaini zilizosagwa na kuchangaywa ndani ya maji pamoja na sabuni ya unga.
Matunda ya mti huu yameonyesha
kupunguza kwa kiasi kikubwa wadudu wa aina hii.
ii. Viwavi wa majani
ya mitunda jamii ya michungwa
Mama wa kiwavi huyu ni kiepeo mkubwa
mwenye rangi nyeusi pamoja na mabaka meupe. Kipepeo jike hutaga
mayai kwenye majani na baada ya mayai
kutotolewa viwavi hutokea. Huwa ni wadogo wenye rangi ya udongo ama kijani na
alama nyeupe mgongoni. Viwavi hawa hutoa vitu kama pembe mbili kichwani za
kutishia maadui na hutoa harufu mbali wanapobugudhiwa
Madhara
Viwavi hawa hula majani machanga kwenye
miche. Huweza kusababisha miche kunyauka kwa kukosa majani hasa kwa miche
midogo ya michungwa.
Kuzuia
Kagua miche mara kwa mara na kuwaondoa
kwa mkono na kuwauwa au tumia dawa za kuulia wadudu kama vile Endosulfan, Diazonon
na Fenitrothion.
iii. Viwavi waharibifu
wa majani
Hawa ni viwavi wanao kula majani na
kuweka alama zinazofanana na mifereji au mistari ndani ya jani. Jani lililo
shambuliwa na mdudu huyu huonyesha michoro ya njia ndani ya jani alimo pita
mdudu. Mama wa viwavi hawa ni nondo. Viwavi hawa ni wadogo na wembamba kiasi
kuwa hula sehemu ya katikati ya jani na huacha
ngozi yenye rangi ya fedha. Jani
linaonyesha alama kama michoro ya vinjia vingi alimo pita funza. ushambulia
majani machanga na husababisha jani kujikunja na kuathiri kazi ya utengenezaji
chakula cha mmea.
Kuzuia –
Dawa - diazinon, fenitrothion, thionex,
karate, decis, n.k.
iv. Mdudu anayefyonza
majani machanga ya miembe.
Mdudu mkubwa ana rangi nyeusi kwenye
mabawa na mwili wake una rangi nyekundu. Ana pembe ndefu kuzidi urefu wa mwili
wake. Wadudu wakubwa na wadogo hushambulia mimea kwa kufyonza na hivyo kuingiza/kueneza
sumu inayosababisha sehemu zilizofyonzwa kufa.
v. Wadudu wanaofyonza
maji maji kwenye matawi na majani ya miche
Wadudu hawa hufunikwa na utando mweupe
kama nta. Wadudu wakubwa na wadogo hufyonza chakula cha mmea kwenye mashina,
matawi na majani ya miche na hata miti mikubwa ya matunda jamii ya michungwa.
Wadudu hawa hufuatwa sana na sisimizi kwa vile wanatoa maji yenye sukari ambayo
husababisha ukungu mweusi ambao hufanya matawi na majani kuonekana kama
yamepakwa masizi.
Kuzuia
Zuia sisimizi ambao
huwafuata wadudu hawa, kwani sisismizi huzuia maadui asili wa hawa wadudu
wasiweze kuwashambulia.
Tumia dawa za aina ya –
Diazinon au Endosulfan ili kuwaua.
vi) Panzi (Mburumundu)
Panzi hawa wanaweza kuleta madhara
makubwa pindi wanapokuwa wengi katika kitalu. Kwani aina hii ya panzi hula majani
ya miche na miti midogo iliyopandikizwa shambani hasa wakati wa kiangazi.
Kuzuia
Kuwatoa kwa mkono au
fimbo na kuwauwa.
Nyunyizia Mafuta ya
taa;
Dawa:- Fenitrothion
vii) Nyenyere
Ni vidudu vidogo jamii ya buibui.Viumbe
hawa hushambulia majani ya miche na miti mikubwa
na matunda.Nyenyere hushambulia sana
miche hasa wakati wa kiangazi na kipindi chenye joto kali
Kuzuia
Kama mshambulizi ni makubwa tumia dawa
- Malathion, dicofol.
Minyoo wadogo wadogo
Minyoo hawa hushambulia mizizi ya miche
na miti mikubwa ya mitunda jamii ya michungwa.
Ni vizuri kubadilisha mchanga/udongo au
kikuzia mimea mara kwa mara kwenye kitalu cha kuoteshea miche.
Endapo si rahisi kufanya hivyo tumia
dawa kama vile furadan au unga wa matunda ya mwarobaini kabla ya kuotesha tena miche
sehemu hiyo hiyo.
Magonjwa ya Mitunda
jamii ya michungwa shambani
i) Vidonda katika
shina
Huletwa na aina fulani ya ukungu.
Dalili za ugonjwa huu ni kutokea sehemu ya shina ambayo hubadilika rangi.
Huongezeka ukubwa na baadaye kutoa
utomvu. Ugonjwa huu hutokea sana kwenye sehemu iliyo na udongo ambao hutuamisha
maji.
ii) Ugonjwa wa kukauka
miti
Husababishwa na virusi ambavyo
husambazwa na chawa weusi. Ugonjwa huu hujionyesha kwa dalili zifuatazo:-
Kwa mitunda kama dalansi na ndimu
sehemu ya shina, ganda hunyauka na ndani yake hutokea mipasuko pasuko. Kisha mmea
hudhoofika pole pole na hutoa matunda madogo madogo. Majani ya mitunda
hubadilika ghafla na kuwa njano. Dalili hizi hutokea kutegemea aina ya mche-shina
na kikonyo vilivyotumika. Mche shina unaoweza kustahimili ugonjwa huu ni limao,
mchungwa na michenza aina ya cleoptra.
iii) Ugonjwa wa
kutobadilika rangi kwa machungwa
yanapokomaa
Ugonjwa huu hutokea hasa katika sehemu
za miinuko ya kati na husambazwa na vidudu viitwavyo psyllids, na vile vile kwa
kuchukua vikonyo vya kubebeshea kutoka kwenye miti inayoonyesha dalili za
ugonjwa.
Ugonjwa huu sio tishio sehemu za joto
za nyanda za chini. Dalili za ugonjwa huu ni kama zifuatavyo: Kwenye majani hutokea
mabaka ya rangi ya njano dalili kama vile mti uliokosa madini ya Zinc. Vile
vile hutokea machipukizi ya kusimama yasiyo ya kawaida, matunda huwa ya ukali
na hayabadiliki rangi kuwa njano yanapoiva.
Kuzuia
Sehemu ambazo ugonjwa unaweza kutokea
angalia wadudu kama chawa. Hakikisha wadudu hawa hawashambulii miche kwenye
kitalu. Wakiwepo, majani huonyesha kujikunja kwa kuweka mafundo sehemu ya juu.
Vile vile epuka kuchukua vikonyo kutoka kwenye miti yenye dalili za ugonjwa
huu.
iv)Nzi
weupe wa kwenye mimea jamii ya michungwa
Hawa ni wadudu ambao hukaa kwenye majani ya mimiea wakizaliana na kufyonza
virutubisho vya mmea, na hii husababisha mmea kudumaa na kutoa mazao duni
Kuzuia
Nja ya kiusalama zaidi ni kwa
kupandisha shambani wadudu aina ya Cales
noacki ambao huwala hawa nzi weupe na kuzuia kusambaa kwao
Magonjwa ya matunda ya
miembe shambani
Ukungu wa majani Husababishwa na ukungu
ambao kwenye majani hutokea alama enye rangi ya kahawia na halafu jani
hujikunja na baadaye kudondoka.
Kuzuia
Tumia dawa ya ukungu -
kama vile Benomyl.
Pulizia maji ya yaliyo
changanywa na unga wa mbegu za muarobaini
5 comments:
Hii blog ina elimu nzuri sana
Gingers sana kwa kazi nzuri
Space ya michungwa na milimao ikoje
Mlimao na ndimu huchukua muda gani kuanza kuzaa
Nataka kufahamu namna ya kubebesha mchungwa
Kwa zaidi ya miaka 13 ya ndoa sikuweza kuzaa, naendelea kuharibika hata nikipata mimba, madaktari wote hawakuweza kunisaidia, hadi dada yangu akanielekeza kwa Dr DAWN, ambaye alinisaidia nikapata ujauzito na sasa hivi kuwa na mtoto mzuri wa kike,
Anasaidia pia marafiki zangu wengi niliowaelekeza, Dr DAWN ni baraka kwa kila mtu anayewasiliana naye,
*Kama unataka kupata mimba.
*Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
*Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
*Kama unataka mume/mkeo arudishwe.
*Kama unataka kurejesha mali yako iliyoibiwa au Pesa.
*Ukitaka kutibu aina yoyote ya ugonjwa,
Wasiliana naye kwa WhatsApp: +2349046229159
Post a Comment