KURASA

Friday, December 8, 2017

BOER GOAT - MBUZI BORA WA NYAMA


ASILI
Kiasili ni mbuzi wa Afrika ya kusini ingawa ndani yake kuna damu toka bara Ulaya na India, hii ndio Mbegu kubwa Zaidi ya mbuzi wa nyama ukilinganisha na wengine. Pia wanazalisha kiwango kikubwa cha maziwa ingawa wanafaa Zaidi kwa nyama.

RANGI
Wana mwili wenye rangi nyeupa na kichwani wana rangi nyekundu au hudhurungi (brown) ingawa wapo weupe kabisa au wekundu/hudhurungi kabisa na hii hutokea kwa 0.001%


UMBO
Wana umbo kubwa kufikia kilo 110-135 kwa madume
Kilo 90-100 kwa majike
Wana masikio yaliyolala kama mbuzi wa kinubi (Nubians)


UZAZI
Huwa wanazaa mapacha na huweza kuzaa mara 2 kwa mwaka
Majike ni wazazi na walezi wazuri wa watoto sababu wana maziwa ya kutosha
Watoto hukua haraka sana, na nia aina ya mbuzi ambao sio wakorofi (docile)
Kwenye baridi kali au joto kali huwa inawaathiri kwenye kubeba mimba


Monday, September 11, 2017

UANDAAJI WA MBEGU ZA PAPAI

Uandaaji wa mbegu za mipapai imekuwa ni changamoto kwa baadhi ya watu, leo nitaongelea uaandaaji wake mpaka kupanda na kupata miche yako
 Mbegu tulizotumia leo ni LADY RED ambazo hufaahamika zaidi kama Malkia FI toka nchini Taiwan na huzalishwa na kampuni inayojulikana kama KNOWN-YOU kama zinavyoonekana hapo pichani

 Fungua mbegu zako na uziweke kwenye chombo kisafi kisha jaza maji kiasi, ziloweke humo kwa siku 5 na kila siku badilisha maji
 Siku ya 6 zitoe na uziweke kwenye kitambaa kisafi kukwepa mashambulizi ya fangas, Funga vizuri na  lowesha maji kitambaa chako na ukihifadhi sehemu salama


Zoezi hili linatakiwa kufanyika ndani ya nyumba au banda ambalo litazikinga mbegu dhidi ya jua la moja kwa moja
 Siku ya 7 ukifungua utaona baadhi ya mbegu zimeanza kupasuka na tayari kwa kuanza kuota, panda mbegu zako moja moja kwenye viriba ambavyo ulishaviaandaa kabla kwa kuvijaza udongo wenye rutuba, kama utaweka mbolea hakikisha ilishaoza kabla, viriba viwekwe kwenye kivuli hasa chini ya miti

 Baada ya siku kadhaa mbegu zako zitaanza kuota kama inavyoonekana pichani
 Udongo unatakiwa uwe wenye rutuba na usiotumisha maji
Hakikisha unamwagia maji kila siku angalau mara moja na hasa jioni wakati hali ya joto imepungua

 Baada ya wiki 2 miche itakuwa imefikia kimo cha sentimeta tano, hapa unaweza kuongeza mbole ya kukuzia kama ya kuku na pia kuondoa miche yako kwenye kivuli na kuiweka juani kama njia ya kuandaa kukabiliana na hali ya shamba (hardening off)





Friday, May 19, 2017

MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE

Kila ugonjwa huwa na dalili zake kuu ambazo hutofautisha na magomjwa mengine, ingawa zipo zile za kufanana mfano kutokula vizuri, kushusha mabawa, kuzubaa/kusinzia na joto kuwa juu

No 1: NEWCASTLE /KIDERI / MDONDO
Dalili kuu: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba. kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30% na mult vitamin.

No 2: GUMBORO / INFECTIOUS BURSAL DISEASE.
Dalili kuu:Kuharisha rangi nyeupe kama chokaa. Ukimpasua baada ya kufa kunakuwa na kama matone ya damu kifuani na kwenye firigisi sehemu ya mbele
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.

NO 3: MAREK'S DESEASE/ MAHEPE
Dalili kuu:kuparalyse /kukakamaa and kwa miguu na mabawa, Hapa mguu mmoja mara nyingi huwa mbele na mwingine nyuma, kuvimba kwa kihifadhia chakula (crop), kwa kuku wa mayai huathiriwa wakiwa wadogo ila madhara hutokea wakifikisha miezi 5 wakianza kutaga.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.

NO 4: NDUI YA KUKU / FOWL POX.
Dalili kuu:Vipele sehemu zisizokuwa na manyoya kama vile vilemba vya kichwani (comb na wattle), puani na miguuni.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba., kupunguza madhara waoshe kwa maji ya uvugu vugu yenye chumvi ya mawe hadi Vipele viishe au vipake mafuta na mpe antibiotic kama Otc 20%.

No 5 MAFUA MAKALI/ INFECTIOUS CORYZA
Dalili kuu:Chafya, kusinzia, kuvimba sehemu za  uso, kichwa  na macho, ute mzito mweupe jichoni hupelekea jicho kuziba, udenda puani na mdomoni.
Tiba: Fluban, au  Tylodox au OTC 20 %, Tylosan, changanya na mult vitamin.

No 6: FOWL TYPHOID/ HOMA YA MATUMBO
Dalili Kuu:Mharo rangi ya njano.
Tiba: Esb3, Trimazine 30%, Tylodox.

NO 7 COCCIDIOSIS/ MHARO DAMU.
_Dalili kuu: Kinyesi/mharo rangi ya ugoro mwanzo na unavyoendelea kinakuwa rangi ya damu.
Tiba: Amprolium 20%,Esb3, Trimazine 30%, Vitacox, na Agracox.

NO 8: FOWL CHOLERA/ KIPINDUPINDU CHA KUKU.
Dalili kuu: kinyesi mharo wa kijani.
Tiba: Trimazine 30 % au Esb3.

NO 9 MAGONJWA MATATIZO YANAYOTOKAN NA LISHE DUNI
_Kuvimba macho, miguu kukosa nguvu na kashindwa kusimama au kutembea, kutaga mayai tepetepe, kula mayai, kudonoana.
Tiba: Chakula kiwe na mchanganyiko mzuri wa mult vitamin na protein, kwa wanaodonoana kata au choma midomo yao na uwape mboga za majani ukiwa umezining'iniza juu kidogo.


Kama utawapa kuku wako wa wanaotaga mayai dawa zenye sulphur ndani watapunguza kutaga mayai, kwa hiyo kama utaweza kupata dawa ambayo haina sulphur ndani yake itakuwa ni vizuri zaidi

Wednesday, March 15, 2017

INCUBATORS FOR SALE - VITOTOLESHA MAYAI VINAUZWA

Incubators za kisaasa kwa ajili ya kutotoleshea mayai kama ya Kuku, Kanga, Bata na kadhalika zinatengenezwa hapa hapa nchini na waTanzania wazalendo kutokana na mahitaji yako sahihi, Incubators hizi zinatengenezwa hapa hapa nchini kwa kutumia malighafi zinaziopatikana hapa nchini kwetu na zina ufanisi mkubwa sana na bei yake ni nafuu, Kuanzia mayai 120 ni automatic yaani zinageuza zenyewe mayai
                                                                                                                                                                                                                                 
      UKUBWA BEI (Tsh)
Mayai 60 230,000
Mayai 90 300,000
Mayai 120 580,000
Mayai 180 650,000
Mayai 240 680,000
Mayai 300 750,000
Mayai 480 850,000
Mayai 600 900,000
Mayai 900 1,200,000
Mayai 5000 4,500,000


Kwa mawasiliano mpigie Gimases:0764870930 Tabata Kimanga

Incub ators za kufundishia zenye vioo vitupu ili uweze kuona ndani kwenye muda wote, na battery cages za kufugia kuku nba Sungura zinatengenezwa pia ukitoa oda yako














Hii hapa chini ndiyo ya mayai 5000 na inauzwaTsh 4,500,000 tu, hapa ipo katika hatua za mwisho




Tuesday, February 7, 2017

CHAKULA CHA NGURUWE NA ULISHAJI

A.    Utangulizi

Chakula bora kwa Nguruwe ni moja  ya suala muhimu sana kwenye dhana nzima ya ufugaji wa Nguruwe wenye tija na faida kwa mfugaji. Chakula cha Nguruwe kinagharimu kama asilimia sabini ya garama zote za ufugaji wa nguruwe. Kati ya matatizo mengi yanayosababisha tija na ufanisi duni wa uzalishaji wa Nguruwe yanatokana na lishe duni. Lakini kama wakipatiwa lishe bora, tija na ufanisi wa uzalishaji utakuwa mkubwa hivyo kuongeza faida kwa mfugaji.

B.       Baadhi ya faida za kulisha lishe bora kwa nguruwe

1.     Lishe bora huharakisha ukuaji wa haraka wa Nguruwe nahivyo kupata uzito unaohitajika kwa kipindi kifupi.
2.    Lishe bora hupunguza gharama za ufugaji na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji kwa sababu nguruwe atahitaji kiasi kidogo tu cha chakula na atachukua muda mfupi kupata uzito mkubwa
3.  Lishe bora itapunguza maambukizi ya magonjwa.
4.  Lishe bora huongeza kiasi cha mayai yatakayoivishwa na mama Nguruwe na hivyo kuongeza idadi ya watoto watakaozaliwa

5.    Lishe bora huongeza kiasi cha maziwa yatakayotengenezwa na mama Nguruwe kwa ajili ya watoto hivyo kuwafanya wawe na afya bora itakayo wawezesha wakue haraka na kupunguza idadi ya vifo kwa watoto.

6.    Lishe bora inaongeza ufanisi wa madume ya Nguruwe na hivyo kuongeza uwezo wa kupanda


C.       Viini lishe muhimu kwenye lishe ya nguruwe

Nguruwe wanauwezo wa kula aina nyingi za vyakula lakini vyenye uwezo wa kumeng’enywa kwa urahisi. Chakula cha Nguruwe kilichokamilika kinahitaji kuwa na mchanganyiko wa viini lishe vitano, navyo ni

1.     Vyakula vyenye kutia nguvu mwilini (vyakula vyenye asili ya wanga) k.m
§    Pumba za mchele, Pumba za mahindi, Pumba za ngano, Machicha ya pombe yaliyokaushwa, Mihogo, Viazi vitamu, Viazi mviringo, Miwa, Ndizi mbichi, zilizoiva au zilizopikwa na makombo ya vyakula vya asili vya wanga n.k.

2.     Vyakula vya kujenga mwili (Vyakula vyenye asili ya protini) k.m  
§    Mashudu ya alizeti, mashudu ya pamba na mawese, unga wa dagaa/samaki, damu iliyokaushwa, soya n.k

3.     Vyakula vya asili ya madini
§    Chumvi ya mezani, chokaa ya mifugo (Limestone), mifupa iliyosagwa (bone meal), madini maalum ya nguruwe (Pig mix), madini mchanganyiko (k.m. maklic), madini ya chuma (hasa kwa watoto wa nguruwe) n.k.

4.       Vyakula vya asili ya vitamini k.m
§    Majani mabichi laini, Mbogamboga, Matunda k.m parachichi, maembe, mapapai n.k, viungo mboga kama nyanya, bilinganya n.k. Michanganyiko maalumu yenye viasilia vya vitamini k.m. Vitamini premix n.k.

5*. Maji
§    Hii ni lishe muhimu kwenye chakula cha nguruwe, ila tofauti na viini lishe vingine vilovyotajwa hapo juu ambapo nguruwe anapewa kwa vipindi/muda na kiwango maalum, maji yanahitajika kwa nguruwe muda wote. Mahitaji ya maji ya kunywa kwa nguruwe ni kama ifuatavyo:-
o   Nguruwe anayenyonyesha lita 20 kwa siku
o   Nguruwe aliyeachishwa kunyonyesha lita 5 kwa siku
o   Nguruwe wanaokuzwa na kunenepeshwa wenye kilo 20 hadi 90 lita 5 kwa siku
o   Watoto wa nguruwe lita 1 kila mmoja   

      

D.        Jinsi ya kutengeneza chakula cha nguruwe

Wakati wa kutengeneza chakula cha nguruwe inabidi kuzingatia yafuatayo:

·         Mchanganyiko wako uwe na viinilishe vinne vilivyotajwa hapo mwanzo
·        Chagua aina ya viinilishe vinavyoweza kupatikana kwa urahisi na bei nafuu kwenye mazingira yako
·     Aina ya mchanganyiko wa chakula ni muhimu uzingatie mahitaji ya nguruwe kama umri (k.m. nguruwe wanaonyonya, waliochishwa kunyonya, wanaokua, na wanaonyonyesha)

Mfano jedwali Na 1 linaonyesha michanganyiko mbalimbali ya vyakula vya nguruwe.
  1. Mchanganyiko namba 1: inapendekezwa kwa wafugaji  walioko kwenye mazingira ambayo pumba za mahindi na mashudu ya alizeti yanapatikana kwa urahisi
  2. Mchanganyiko namba 2: kwa wale ambao pumba za mahindi, za mpunga, machicha ya pombe  na mashudu ya alizeti yanapatikana kwa urahisi.
  3. Mchanganyiko namba 3: kwa wale ambao pumba  za mpunga na mahindi yanapatikana kwa urahisi.



Jedwali namba 1: Michanganyiko mbalimbali ya vyakula vya nguruwe

Na

Aina ya viinilishe

Michanganyiko

Namba 1

Namba 2

Namba 3

1

Vyakula vya wanga

 

 

 

1. Pumba za mahindi

70.25

32

30.00

2. Pumba laini za mpunga

-

25

33.00

3.  Machicha ya pombe

     yaliyokaushwa

-

21

-

4. Mahindi yaliyoparazwa

-

-

10.00

2

Vyakula vya protini

 

 

 

A. Protini ya nafaka

 

 

 

1. Mashudu ya alizeti

22.00

14

22.00

2.Mashudu ya michikichi

-

-

 

3. Soya iliyochemswa na kuparazwa

-

-

-

B. Protini ya Wanyama

 

 

 

4.Unga wa dagaa/samaki

4.00

2.00

3.25

5.Damu iliyokaushwa

-

2.25

-

3

Vyakula viasili vya madini

 

 

 

 

1. Chumvi ya mezani

0.50

0.50

0.50

 

2. Chokaa ya mifugo    

   

2.00

2.00

2.00

 

3.  Unga  wa mifupa

1.00

1.00

1.00

 

4. Madini na vitamini    

    mchanganyiko

0.25

0.25

0.25

 

         Jumla

100.

100

100.




E.     Kiasi na namna ya kulisha

·         Nguruwe wanahitajika kulishwa aina hii ya chakula mara mbili (asubuhi na mchana) au zaidi kwa siku
·         Kiwango/kiasi cha kulisha kwa nguruwe wa aina na rika tofauti kimeonyeshwa kwenye jedwali Namba 2
·         Pamoja na vyakula vilivyotajwa, wafugaji wanashauriwa kuwapatia nguruwe vyakula vyao vya asili kama vyakula vya ziada mfano, majani mabichi laini, majani ya maboga, mbogamboga, matunda kama maparachichi, majani ya viazi n.k.     

Jedwali na 2:  Viwango vya kulisha Nguruwe wa uzito mbalimbali

Na
Wakati
Uzito wa nguruwe (kilo)
kiasi cha chakula  (kilo kwa siku)
1.
Baada ya kuachishwa kunyonya hadi uzito kiasi
10 - 17
0.75
2.
Uzito uliozidi kiasi kidogo
18 - 29
1.00
3.
Uzito wa kawaida
30 - 40
1.50
4.
Uzito mkubwa kiasi
41 - 60
2.00
5.
Uzito mkubwa
61 - 80
2.5
6.
Uzito mkubwa sana
81 - 100
3.00


Jinsi ya kulisha makundi mbalimbali ya nguruwe

1.        Kipindi cha mamba, kuzaa hadi kuachisha kunyoyesha

1.1 Kipindi cha miezi mitatu baada ya kupandishwa
·              Apatiwe chakula kiasi k.m. kilo mbili kwa siku
·              Kiasi hiki kiendelee hadi wiki 3 kabla ya kuzaa

1.2 Wiki tatu kabla ya kuzaa
·              Ongeza chakula kufikia kilo 2½.

1.3 Wiki moja kabla ya kuzaa
·              Anza kuopunguza chakula taratibu hasa vyakula vya nafaka (Concentrate rations).
·              Ongeza vyakula vya  mbogamboga, majani laini na matunda (laxative meals).

1.4 Siku ya kuzaa
·              Usimpe chakula chochote cha nafaka.
·              Mpe vyakula vya mbogamboga,na  vilaini kwa kiasi kidogo tu
·              Mpatie maji ya kutosha.

1.5 Siku ya 1 – 2 baada ya kuzaa
·              Mpe ½ kilo ya chakula kamilifu.

1.6 Siku ya 3 na kuendelea
·              Ongeza chakula cha nafaka kwa kiasi cha kilo 1 kwa siku.
·              Ongeza kufikia kiwango kinachohitajika kulingana na idadi ya watoto alionao mama nguruwe.

Zingatia

·              Mama nguruwe anahitaji kilo 3 za chakula kwa matumizi yake ya kawaida.
·              Atahitaji kiasi cha theluthi moja (1/3)  ya kilo ya chakula kwa kila mtoto aliyenae
Mfano: kama mama ana watoto 9 atahitaji kiasi gani cha chakula?
Mahitaji mama peke yake
Mahitaji kutokana na watoto
Kiasi cha chakula kwa siku
3kg
Theluthi moja x 9
Kilo 6 kwa siku
                  3     +         (1/3   x  9)       =      6 Kg

·              Endelea kumpa kiwango hicho cha chakula mpaka ifikapo wiki moja kabla ya kuwaachisha watoto kunyonya.
·              Wiki moja kabla ya kuwachisha punguza kiwango taratibu mpaka kufikia kilo 3½ kwa siku.
 
Baada ya kuachisha kunyonya
·              Mama nguruwe apatiwe chakula bora kilicho na kiwango kikubwa cha madini na vitamini  kiwango cha kilo 2 – 3 kwa siku.
·              Hii itamsaidia kuivisha mayai, hivyo kumsaidia kupata joto mapema.

Chakula kwa ajili ya watoto wa nguruwe (Creep feed)
§    Hiki ni chakula wapewacho nguruwe wachanga wakiwa na umri wa wiki ya pili hadi wiki ya tatu.
§    Kipindi hiki mahitaji ya watoto ni makubwa ambayo hayawezi kuteshelezwa na maziwa pekee ya mama yao.
§    Chakula hiki kitawasaidia watoto kuzoea chakula kigumu, kutosheleza mahitaji yao, na hivyo huwawezesha watoto kukua kwa haraka
§    Creep feed inaweza kutengenezwa kwa kuchanganya viini lishe vifuatavyo


Aina ya  viinilishe
Asilimia

Mahindi yaliyobarazwa

30
Pumba za mahindi
40
Mashudu ya alizeti
18
Unga wa Dagaa
10
Unga  wa mifupa
0.5
Chokaa ya mifugo (limestone)
0.75
Chumvi ya mezani
0.5
Premix
0.25
Jumla
100