Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Kama unataka kufanya kilimo, ufugaji wanyama, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki, kilimo cha miti ya mbao, kilimo cha majani na malisho ya mifugo, utaalamu wa mbolea na udongo katika mazingira halisi ya ki Tanzania basi wasiliana nami (mitiki1000@gmail.com) NB sihusiki na habari za masoko ya bidhaa yoyote ya kilimo na mifugo, kabla hujaingia kwenye mradi fanya utafiti wa masoko wewe mwenyewe
Tuesday, September 29, 2009
SEHEMU YA 4 - MATUNZO YA WATOTO WA NGURUWE
Kwa kawaida hunyonya kwa wiki 5 -8, na baada ya hapo hutengwa na mama yao na kuanza kupewa chakula chenye protini 25% kwa muda wa wiki 6 za mwanzo
KUKATA MENO
Mara baada ya kuzaliwa watoto wakatwe meno kwa kutumia mkasi mkubwa au kifaa cha kukatia waya (wire cutter) umuhimu wa zoezi hili ni kwa sababu nguruwe huzaliwa na meno na mara wanapoanza kunyonya huumiza chuchu za mama yao na kumsababishia ugonjwa wa chuchu (mastitis)
MADINI CHUMA
Wakizaliwa tu wanahitaji madini ya chuma kwa wingi, maziwa ya mama yanatoa kiasi cha 10% tu, huwa wanapigwa sindano (Iron Injection) kiasi cha 155mg kwa kitoto kimoja ili kuwaongezea madini ya chuma ya ziada, muone mtaalamu wa mifugo akusaidie kwa hili
KUHASI
Madume ambayo yatakuzwa kwa ajili ya nyama ni vizuri yakahasiwa, hii husaidia ukuaji wa haraka na pia huondoa harufu ya balehe, Zoezi hili lifanyike wakati wakiwa na wiki 2-3 inapofika wiki ya 5 zoezi huanza kuwa gumu kwa sababu watoto wanakuwa wakubwa na litahitaji sindano za ganzi, zoezi hili linahitaji mtaalamu wa mifugo.
MINYOO
Mzazi anapokaribia kujifungua wiki ya mwisho achomwe sindano ya kuondoa minyoo na magonjwa ya ngozi ijulikanayo kama IVOMEC SUPER au IVERMECTIN zinazopatikana kote nchini, dawa hii husaidia kuwalinda watoto na minyoo hadi wanapoacha kunyonya ndio na wao wapigwe sindano hii ambayo pia itasaidia kuua minyoo ya mapafu, minyoo ya macho, viroboto na kuondoa ukurutu.
CHAKULA
Baada ya wili chache vitoto vitaanza kula chakula kidogo kidogo kwa kuanzia na kile anachopewa mzazi, hakikisha mzazi anapewa chakula kingi na chakutosha kwa sababu atakuwa anakula yeye na watoto wake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
13 comments:
Ndugu yangu Bennet, huogopi watu wanashughulikia haki za wanyama, yaani unazungumzia kuwahasi madume waziwazi....
he!he!he! hiyo mbona inakubalika kitaalamu, kwa mfano chama cha daranimlheaven kinachohusika na kuokoa wanyama waliotupwa au kuachwa na wamiliki wao, hawawezi kukupa mnyama uishinaye mpaka wamemuhasi
Nimejifunza kuhusu kuwakata meno watoto wa nguruwe nilikuwa sijui na wala sikuwahi kusikia. Nataka nikiwa Ruhuwiko nifuge nguruwe ntakutafuta kaka Bennet.
ndugu yangu yasinta chonde chonde usinisahau wakati ukichinja. haidhuru ukinisahau wakati wa kufuga.
LOL!
Kaka mwaipopo usipata taabu SITAKUSAHAU:- si unajua ule msemo kulima mmoja kula wengi...LOL
Siku ukichinja naona huko Ruhuwiko kutafurika wageni maana na mimi nitakuja fasta
imenivutia sana ntaanza kufikiria kufuga Kitimoto
Mimi ni msomaji mpya wa mada zako. Nimenunua nguruwe watatu jike wana miezi mitatu sasa. Ninapenda unifahamishe zaidi juu ya ung'oaji wa meno. Unayang'oa yote au inakuwaje na wakati wa kung'oa unalikata kipande au unavuta kwa maana ya kulitoa lote. tafadhari nisaidie hapa. zkerenge@gmail.com
Nadhan hao watakuwa vibogoyoo.
!Au nmekosea kaka bennet.
Darasa hili ni zuri mno, kwani linatuelimisha sana, hongera Bro Bennet!
Hongera sana na shukran sana kwa kutupa elimu
Nahitaji kitabu cha ufugaji wa nguruwe soft copy. Email ochaie4@gmail.com
Post a Comment