Kutokana na maombi ya Ndugu Buyanza ya kutaka kufahamu kati ya kilmo cha mahindi na Mpunda kipi kina faida zaidi, nami nimejaribu kuchambua kidogo kati ya mazao haya mawili
MPUNGA
Katika hecta moja ya mpunga unaweza kuzalisha mpaka kilo 3675 kwa mkupuo mmoja, kama shamba ni jipya itakuchukua miezi 6 mpaka kuanza uvunaji, hii ni kwa sababu ya kuliandaaa shamba lako, baada ya mvuno wa kwanza utaweza kuvuna mara 3 kwa Mwaka. Hii inamaanisha kwamba unaweza kuvuna kiasi cha tani 10 -11 kwa Mwaka kama utafanya kilimo cha umwagiliaji.
Kilo ya mpunga sasa hivi ni shilingi 700 – 800 ingawa bei hupanda baadae kama utahifadhi mpunga wako kwa maana hiyo kwa Mwaka unaweza kupata kati ya shilingi milioni 7 mpaka milioni 8, gharama za kulima mpunga ni wastani wa asilimia 20- 22 ya mauzo, kwa maana hiyo kwa Mwaka kilimo chako kitatumia si zaidi ya shilingi milioni 2 kwa mara zote 3 utakazolima, hii ikijumuisha vibarua na mbolea.
MAHINDI
Kama utalima mahindi, ambayo unaweza kulima mara 2 kwa Mwaka kwa ukanda wa pwani na mara moja kama nisehemu zenye baridi, MAvuno kwa hecta moja ni kilo 7500 kwa maeneo yenye baridi na kilo 5000 kwa ukanda wa pwani ambapo utavuna kilo 10,000 kwa Mwaka. Bei ya mahindi kwenye soko ni wastani wa shilingi 400 kwa maana hiyo unaweza kupata shilingi milioni 4 kwa Mwaka.
Matumizi ya mbolea za viwandani ni lazima ili kufikia mavuno haya, Mbolea kama UREA itawekwa mara mbili wakati wa kupandia na kukuzia ikichanganywa na DAP (diamonium phosphate) ghara jumla ya mbolea hizi kwa mpando mmoja hufikia kiasi cha shilingi laki 7 mara mbili ni shilingi 1,400,000 ukongeza na gharama za kuandaa shamba na kupalilia kama 200,000 unapata jumla ya 1,600,000 kwa hiyo utabakiwa na kama shilingi 2,400,000
HITIMISHO
Mpunga ukilimwa kitaalam unawezza kukupatia faida shilingi milioni 5 kwa Mwaka, wakati mahindi yatakupatia shilingi milioni 2.5, faida ya mpunga inakuwa kubwa kwa sababu utalima mara 3 kwa Mwaka lakini kama utategema mvua utalima mamra 2 tu kwa Mwaka na utapata faida ya shilingi 3,300,000 kwa Mwaka
Hizi data ni kwa uzoefu wangu tu wa haraka haraka, bei ya mazao inaweza kupanda au kushuka na kiasi cha uzalishaji kwa hecta kinaweza kupanda au kushuka kutokana na aina ya mbegu, hali ya hewa na uzoefu wa mkulima mwenyewe. Kwa sasa hivi kilo ya unga wa mahindi ni shilingi 700 na debe la mpunga wa kyela ni shilingi 20,000, unaweza kupata faida zaidi kama utaachana na madalali na kupeleka mazzao yako sokoni mwenyewe
6 comments:
Vyote vina faida hamna tofauti.
ina tegemea na matumizi yake, hasa kwa vile kuna nchi zinazo tengeneza magari yanayo tumia mafuta ya mahindi
Nakubali kwamba mbunga una faida zaidi, kwasababu ni chakula kinacho pendwa na wengi, na haswa watu wa zanzibar.
Mahindi kwa sababu yanatupatia ugali na mimi kama Msukuma bila ugali maisha hayaendi!
Kila zao lina faida yake kulingana na hali ya hewa, mahitaji na matarajio ya mkulima. Kwa uzoefu wangu mpunga una kazi nyingi zaidi kuliko mahindi. Nilikuwa nachukia sana kupalilia mpunga kwenye tope na wakati mwingine kwenye maji mpaka magotini. Mahindi haya adha hiyo.
kwa kutumia mbolea ya kemikali kwa ecta unapata magunia mangapi?
kwa kutumia mbolea ya kemikali kwa ecta unapata magunia mangapi?
Post a Comment