KURASA

Thursday, November 26, 2009

VITUNGUU

Ndugu Bunyanza kwa mara nyingine tena alitaka kujua kuhusu zao la vitunguu, na mimi bila hiyana naelezea yale machache ninayoyafahamu.



Zao la vitunguu hulimwa karibu kila mahali hapa nchini. Hata hivyo, mikoa inayolima kwa wingi ni Tanga, Arusha, Iringa, Kilimanjaro, Singida, Morogoro, Mara, Mbeya Dodoma na Manyara. Zao hili ni la biashara na chakula. Ekari moja inaweza kuzalisha gunia 80 – 100 za vitunguu zikitunzwa kitaalam, na mkulima anaweza kulima mara mbili kwa Mwaka kwa mbegu kubwa ambazo huchukua hadi miezi mitano (5) shambani. Bei ya wastani kwa gunia moja ni Tsh 60,000

MAMBO YA KUZINGATIA WA K ATI WA UZALISHAJI

Ili kupata vitunguu bora na vingi ni muhimu kuzingatia kanuni za kilimo bora cha vitunguu.Baadhi ya kanuni hizo ni kama zifuatazo: -



1 - Kuchagua aina ya mbegu

• Chagua aina bora kulingana na matakwa ya soko
• Pamoja na mahitaji ya soko ni muhimu pia kuchagua aina inayovumilia magonjwa, wadudu,kukomaa mapema na kutoa mazao mengi na bora.

2 - Kuweka mbolea
Vitunguu hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha.
• Tumia mbolea za asili ili kurutubisha udongo kwa lengo la kupata mazao mengi na bora.
• Iwapo ni lazima kutumia mbolea za viwandani muone mtaalam wa kilimo ili akuelekeze namna ya kutumia. Mbolea ikizidi huharibu ubora wa vitunguu.

3 - Kumwagilia maji
• Kagua shamba kuona kama udongo una unyevu wa kutosha. Iwapo unyevu ni mdogo mwagilia maji kufuata mahitaji ya mmea. Vitunguu vinapoanza kukomaa punguza kumwagilia ili kuepuka kuoza



4 - Kupalilia
• Palilia mara kwa mara ili kudhibiti magugu na kuwezesha vitunguu kutumia vizuri unyevu na virutubishi vilivyoko kwenye udongo. Pia magugu mengine huficha wadudu waharibifu kama vile utitiri mwekundu.
• Wakati wa kupalilia epuka kukata mizizi ya mimea.
• Pandishia udongo na kufunika shina la kitunguu wakati wa kupalilia ili kuzuia jua lisiunguze mizizi na kubabua vitunguu. Vitunguu vilivyoungua na kubabuliwa ubora wake hushuka napia huharibika upesi wakati wa kuhifadhi.

5 - Kudhibiti magonjwa na wadudu
Vitunguu hushambuliwa na magonjwa na wadudu mbalimbali ambao huweza kusababisha upungufu na ubora wa mazao. Ili kudhibiti tatizo hilo kagua shamba mara kwa mara kuona dalili za mashambulizi. Endapo kuna dalili za mashambulizi, chukua tahadhari ya kunyunyuzia dawa mapema kabla madhara hayajaleta upotevu mkubwa.

6 - Kupanda kwa nafasi:
Zingatia nafasi ya kupanda inayopendekezwa ili kupata vitunguu vyenye ukubwa uliokusudiwa. Wastani ni inchi 4 - 5 kutoka kitunguu kimoja hadi kingine, na inchi 12 - 18 kutoka mstari hadi mstari na kipandwe inchi 1 - 1.5 chini ya udongo

MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA

1 - Kukagua shamba
• Kagua shamba ili kuhakikisha kuwa vitunguu vimekomaa. Vitunguu huwa tayari kuvunwa miezi mitatu hadi mitano tangu kusia mbegu kutegemea aina ya mbegu na hali ya hewa.Dalili za vitunguu vilivyokomaa:

• Majani hunyauka na kuanza kukauka
• Asilimia kumi hadi 20 ya mimea huanguka majani na shingo hulegea.
• Majani hubadilika rangi kuwa ya manjano na baadaye kaki

VITUNGUU VILIVYOKAUKA MAJANI TAYARI KWA KUVUNA



2 - Kuvuna
Vitunguu vinapaswa kuvunwa mapema mara tu vinapokomaa ili kupata mazao mengi na bora.Uvunaji hufanyika kwa mikono ambapo jembe uma hutumika kuchimbua au kulainisha udongo.Udongo ukishalainishwa vitunguu hung’olewa kwa mkono. Inashauriwa uvunaji uanze asubuhi ili vitunguu viweze kunyauka na kukomaza ngozi sehemu za michubuko. Vitunguu visiwekwe juani na inapobidi kukomaza ngozi shambani, majani ya vitunguu yatumike kufunika vitunguu ndani ya matuta yake wakati wa mchana ambapo kuna jua. Kusanya vitunguu kwenye vikapu kisha vipeleke sehemu ya kukaushia. Vitunguu vya kukaushia kwenye kichanja ni bora zaidi, mizizi na majani hupunguzwa na kuachwa urefu wa robo inchi . Vitunguu vya kukausha kwa kunining’iniza havikatwi majani bali hufungwa kwenye mafungu na kupelekwa sehemu ya kukaushia.

16 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mara nyingi nimejaribu kulima vitunguu hapa lakini kuna wadudu wananiwahi sasa nitajaribu kufuata njia hii. Ahsante.

mumyhery said...

darasa zuri sana, shukran

Bennet said...

Nawashukuru sana Dada Yasinta na Mumyhery

Anonymous said...

Ebana shukran sana mkuu benet,hili somo ndo haswaaa nililokuwa nalihitaji...na limezima ule ubishi wangu ambao ulionifanya nisubiri kwanza majibu.

Buyanza

Anonymous said...

Mkuu japo mimi sijishughulishi na kilimo kwa sasa lakini nimefurahi kwamba wadau mpo mnajatibu kusaidia watanzania wenzetu ktk sekta hii muhimu ya kilimo.

Kazi nzuri.

Mdau Simon - New Delhi

Anonymous said...

asante sana kwa ushauri huu mzuri wa kilimo

Anonymous said...

Big up kaka, endelea na juhudi zako za kuwaelimisha na kuwakomboa watanzania. Tunahitaji upembuzi yakinifu wa uzalishaji wa zao la kitunguu.

Anonymous said...

habari yangu bwana benet,
Je unafikiri naweza kufanya kilimo ichi kwenye mkoa wa kagera?
maana nimeona nikoa uliyoitaji haitofatiani sana kwa hali ya hewa na Kagera

Masome said...

Hii ni tutorial nzuri, big up. Ntaifanyia kazi

ngome kombo said...

nimeipenda big up broo

Unknown said...

mimi pia ni mejifunza vizuri kupitia hapa katika hili zao la vitunguu...ningependa kujua msimu wa kilimo wa zao hili ni miezi gani?pia ningependa kujua ni maeneo gani kwa hapa Tanzania nikilima uwezekano wa kuuza bei nzuri unakuwa mkubwa?

Asantheni.

Immapolite said...

Mimi ndio nafanya study nataka kuanza kilimo cha vitunguu naombeni ushauri zaidi via 0766655535 napatikana moshi.

Unknown said...

Habari kaka , mimi nataka kulima mwaka huuu, ila sijuwi je ni muda gani naweza anza kulima kilimo cha vitunguu, pia nia gharama gani kwa heka
AKHSANTE

SALUM SIMBA

Unknown said...

Asanteni xana wadau mi nataka kulima maeneo ya rufiji nje kililmo hiki kitakubali nataka nilime ekari tano kwa utafit wangu aridh IPO vizuri xana

Unknown said...

Jaman nimevutiwa sana na elimu hii sasa nikitaka kuanza ni lazima niwe na mtaji wa sh. Gapi? Kwa ekali moja?

Habibty said...

Kwa tafiti niliyo fanya Mimi gharama ni 3,000,000 Kwa hekari moja, ila sifahamu ni miezi gani mizuri kuanza kilimo hiki kwa anae faham please contact me 0752148266