Kumekuwa na baadhi ya watu ambao huwatapeli baadhi ya watu kwa kuwauzia samaki wa baharini na kuwaambia kwamba niwa maji baridi, wanachofanya ni kuwavua samaki wa maji chumvi toka baharini, na kisha kuwaweka kwenye chombo kizuri chenye maji baridi yasiyo na chumvi, wakiwa humo huweza kushi hata zaidi ya masaa 12 na ndipo huanza kuishiwa nguvu na baadae kufa.
Kwa kawaida samaki wa baharini ni wazuri zaidi ya wale wa maji baridi, na hii ndio huwavutia zaidi watu wasio na uelewa wa samaki wa urembo na kuwa nunua, kwa kawaida matapeli hawa utawakuta kwenye makutano ya barabara kubwa na huuza samaki hawa kwa wenye magari wakati wa foleni kubwa za jioni, na wakisha kuuzia kesho huama eneo hilo na kuamia lingine maana wanajua kwamba utawatafuta
Huyu niliyemnasa kwenye video hii alikuwa kwenye mataa ya Ubungo, mimi nilikuwa natokea mwenge kuelekea maeneo ya Ilala
Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Kama unataka kufanya kilimo, ufugaji wanyama, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki, kilimo cha miti ya mbao, kilimo cha majani na malisho ya mifugo, utaalamu wa mbolea na udongo katika mazingira halisi ya ki Tanzania basi wasiliana nami (mitiki1000@gmail.com) NB sihusiki na habari za masoko ya bidhaa yoyote ya kilimo na mifugo, kabla hujaingia kwenye mradi fanya utafiti wa masoko wewe mwenyewe
Wednesday, November 24, 2010
Thursday, November 18, 2010
KILIMO BORA CHA MAEMBE
Maembe hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Tabora, Pwani, Mtwara, Tanga, Mwanza, Morogoro na Mbeya. Uzalishaji wake ni wastani wa tani 159,472 kwa mwaka. Maembe ni zao muhimu la biashara na chakula.
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI
Ili kupata mazao bora ni muhimu kuzingatia kanuni bora za kilimo cha maembe hasa kanuni
zifuatazo:
Kuchagua aina bora ya kupanda kulingana na mahitaji ya soko.
Panda umbali wa mita 10 kwa kumi kama utatumia miembe ya kuunga, hii ni kwa sababu haiwi mikubwa sana kwa sababu haiishi miaka mingi, kwa ile ambayo si ya kuunga panda umbali wa mita 15 kwa 15 kwa kila mti mmoja wa muembe
DHIBITI MAGONJWA, WADUDU, NA MAGUGU
• Fanya ukaguzi wa shamba mara kwa mara ili uweze kudhibiti wadudu na magonjwa ya matunda kabla madhara hayajawa makubwa
UGONJWA WA KUTU KWENYE MAJANI
• Ni muhimu kudhibiti wadudu, magonjwa na magugu ili kupata mazao bora ambayo yatapata soko zuri na kuweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
• Hakikisha shamba ni safi wakati wote ili kupata matunda bora na kurahisisha uvunaji.
MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA
Kusafisha shamba pamoja na barabara za shamba
• Safisha shamba ili kurahisisha uvunaji na usafirishaji shambani.
Kukagua shamba kuona maembe kama yamekomaa Maembe hukomaa katika kipindi cha miezi 4 hadi-6 tangu kutoa maua kutegemea hali ya hewa na aina.
DALILI ZA MAEMBE YALIYOKOMAA
• Maembe hung’ara
• Kwa aina nyingine rangi ya kijani hufifia na kuanza kubadilika kuwa ya manjano.
ANDAA VIFAA VYA KUBEBEA, SEHEMU YA KUFUNGASHIA NA USAFIRI.
VIFAA VYA KUBEBEA
• Ngazi
• Vikapu
• Mifuko
• Ndoo
• Vichumio
VIFAA VYA KUFUNGASHIA
• Makasha ya mbao/plastiki na ya makaratasi magumu na matenga
VYOMBO VYA KUSAFIRISHIA
• Matoroli
• Magari
• Baiskeli
• Matela ya matrekta
KUVUNA
Njia bora ya kuvuna maembe ni Kuchuma kwa mkono
• Kwa miembe mifupi chuma maembe pamoja na kikonyo chake
• Kwa miembe mirefu chuma kwa kutumia kichumio maalumu
KICHUMIO MAALUM
• Acha kikonyo chenye urefu wa sentimita tatu hadi nne ili kuzuia madoa ya utomvu. Utomvu huchafua matunda na hushusha ubora. Pia embe lililovunwa bila kikonyo chake huingiliwa na vimelea vya ugonjwa kwa urahisi.
• Vuna wakati wa asubuhi au jioni ili kuepuka jua kali linaloweza kubabua matunda.
• Wakati wa kuvuna hakikisha maembe hayadondoshwi chini, ili kuepuka kuchubuka kwa matunda ama kupondeka hasa yale yaliyoiva barabara. Aidha beba matunda kwa vikapu au mifuko na kusanya kwenye kivuli.
KUCHAMBUA MAEMBE
Kuchambua ni kutenga matunda yaliyooza, kupasuka, yenye dalili za magonjwa au kubonyea, ili kupata matunda yenye ubora kwa ajili ya matumizi, kusindika au kuuza.
• Matunda yaliyooza na yenye wadudu ni vyema yafukiwe ili kuzuia kuenea kwa wadudu waharibifu na vimelea vya magonjwa.
• Matunda yaliyopasuka, kubonyea , kuchubuka kidogo wakati wa kuvuna au kuiva sana yatumike haraka kwa chakula.
• Matunda mazuri ambayo hayajapata madhara yoyote yatunzwe kwa ajili ya kusindikwa, kutumika au kuuzwa.
KUSAFISHA MAEMBE
• Baada ya kuchambua, safisha matunda kwa maji safi ili kuondoa uchafu na mabaki ya madawa.
• Maembe yanayokusudiwa kuuzwa nje ya nchi hunyunyiziwa nta ili kuzuia kunyauka na kudumisha ubora.
• Baada ya kusafisha tumbukiza maembe kwenye maji yenye nyuzi joto zipatazo 52 za Sentigredi kwa muda wa dakika tano. Maji haya pia yanaweza kuchanganywa na madawa ya klorini asilimia 1 ili kuzuia magonjwa ya ukungu.
KUPANGA MADARAJA
Madaraja hupangwa kwa lengo la kurahisisha ufungashaji, usafirishaji na uuzaji. Madaraja hupangwa kulingana na ubora, ukubwa , aina rangi na uivaji.
KUFUNGASHA MAEMBE
Ufungashaji hufanyika katika sehemu safi na yenye kivuli. Ufungashaji wa kujaza kupita kiasi husababisha upotevu wa maembe. Aidha ubora hushuka kutokana na kuminyana na kubonyea kwa matunda wakati wa kusafirisha
TENGA LA KUFUNGASHIA MAEMBE
Inashauriwa kufungasha kwenye makasha ya mbao/ plastiki , makaratasi magumu au tenga kwa sababu zifuatazo:
• Matunda yanaweza kupangwa na kusafirishwa bila kuchubuka, kubonyea au kupasuka.
• Huweza kupakiwa na kupakuliwa kwenye chombo cha usafiri kwa urahisi.
Wakati wa ufungashaji ni muhimu kuzingatia yafuatayo:
• Kasha moja lisizidi uzito wa kilo 20 ili kurahisisha ubebaji.
• Makasha yawe imara na yenye matundu ya kutosha ili kuruhusu mzunguko wa hewa.
• Ni muhimu kutanguliza vitu vilivyo safi ndani ya vifungashio ili kuzuia michubuko na mipasuko ya matunda wakati wa kusafirisha.
• Maembe yapangwe kwa kubananisha na kwa kuhakikisha kuwa vikonyo havitoboi matunda na kusababisha majeraha wakati wa kusafirisha. Kubananisha matunda husaidia kuzuia mgongano unaoweza kusababisha matunda kusambaratika na hivyo kubonyea au kupasuka wakati wa kusafirisha.
KUSAFIRISHA
Ili kuepuka upotevu na uharibifu wakati wa kusafirisha, ni muhimu maembe yapangwe kwenye vyombo vya kufungashia na kusafirisha kwa uangalifu, ndani ya matela, mikokoteni na magari. Epuka kutupa matunda wakati wa kupakia na kupakua. Wakati wa kupanga mazao katika vyombo vya usafiri yasirundikwe ovyo na yasijazwe kupita kiasi ili yasimwagike. Vilevile yafunikwe ili yasipigwe na jua. Jua huongeza kasi ya kuoza. Matunda yakipigwa na jua kwa muda wa saa mbili mfululizo husababisha kuoza kwa asilimia 100.
KUHIFADHI
• Maembe huweza kuhifadhiwa kwenye chumba chenye hali ya hewa yenye joto la nyuzi 8 hadi 10 za Sentigredi na unyevu wa asilimia 85 hadi 90. Katika hali hiyo, maembe yanaweza kuhifadhiwa bila kuharibika kwa mwezi mmoja.
• Kagua mara kwa mara ili kugundua uharibifu unaoweza kutokea
Subscribe to:
Posts (Atom)