KURASA

Wednesday, November 24, 2010

MATAPELI WA SAMAKI WA UREMBO

Kumekuwa na baadhi ya watu ambao huwatapeli baadhi ya watu kwa kuwauzia samaki wa baharini na kuwaambia kwamba niwa maji baridi, wanachofanya ni kuwavua samaki wa maji chumvi toka baharini, na kisha kuwaweka kwenye chombo kizuri chenye maji baridi yasiyo na chumvi, wakiwa humo huweza kushi hata zaidi ya masaa 12 na ndipo huanza kuishiwa nguvu na baadae kufa.

Kwa kawaida samaki wa baharini ni wazuri zaidi ya wale wa maji baridi, na hii ndio huwavutia zaidi watu wasio na uelewa wa samaki wa urembo na kuwa nunua, kwa kawaida matapeli hawa utawakuta kwenye makutano ya barabara kubwa na huuza samaki hawa kwa wenye magari wakati wa foleni kubwa za jioni, na wakisha kuuzia kesho huama eneo hilo na kuamia lingine maana wanajua kwamba utawatafuta

Huyu niliyemnasa kwenye video hii alikuwa kwenye mataa ya Ubungo, mimi nilikuwa natokea mwenge kuelekea maeneo ya Ilala

3 comments:

emu-three said...

Nchi ya bongo hii...unakumbuka ule wimbo wa `bongooo, bongo dar-esalaamu. Watu wanaweza wakauaza hata sumu, ilimradi tu wapate pesa hata bila kujali maisha ya anayemuuzia

Yasinta Ngonyani said...

kaazi kwelikweli jamani!!

Anonymous said...

jamani ndugu zetu wanachakarika wanabuni njia za kujipatiya chajio mimi sioni kama kuna tatizo kaka BEN jaribu kuwaelewesha vijana namna ya kuwafuga,tatizo kwawale wanaoishi mbali ya bahari hawawezi kuyapata maji ya bahari kama una uwezo wa kupata maji ya bahari hakuna usumbufu tatizo ni kujua samaki uliyonunua si wale wanaokula majani