KURASA

Friday, May 19, 2017

MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE

Kila ugonjwa huwa na dalili zake kuu ambazo hutofautisha na magomjwa mengine, ingawa zipo zile za kufanana mfano kutokula vizuri, kushusha mabawa, kuzubaa/kusinzia na joto kuwa juu

No 1: NEWCASTLE /KIDERI / MDONDO
Dalili kuu: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba. kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30% na mult vitamin.

No 2: GUMBORO / INFECTIOUS BURSAL DISEASE.
Dalili kuu:Kuharisha rangi nyeupe kama chokaa. Ukimpasua baada ya kufa kunakuwa na kama matone ya damu kifuani na kwenye firigisi sehemu ya mbele
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.

NO 3: MAREK'S DESEASE/ MAHEPE
Dalili kuu:kuparalyse /kukakamaa and kwa miguu na mabawa, Hapa mguu mmoja mara nyingi huwa mbele na mwingine nyuma, kuvimba kwa kihifadhia chakula (crop), kwa kuku wa mayai huathiriwa wakiwa wadogo ila madhara hutokea wakifikisha miezi 5 wakianza kutaga.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.

NO 4: NDUI YA KUKU / FOWL POX.
Dalili kuu:Vipele sehemu zisizokuwa na manyoya kama vile vilemba vya kichwani (comb na wattle), puani na miguuni.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba., kupunguza madhara waoshe kwa maji ya uvugu vugu yenye chumvi ya mawe hadi Vipele viishe au vipake mafuta na mpe antibiotic kama Otc 20%.

No 5 MAFUA MAKALI/ INFECTIOUS CORYZA
Dalili kuu:Chafya, kusinzia, kuvimba sehemu za  uso, kichwa  na macho, ute mzito mweupe jichoni hupelekea jicho kuziba, udenda puani na mdomoni.
Tiba: Fluban, au  Tylodox au OTC 20 %, Tylosan, changanya na mult vitamin.

No 6: FOWL TYPHOID/ HOMA YA MATUMBO
Dalili Kuu:Mharo rangi ya njano.
Tiba: Esb3, Trimazine 30%, Tylodox.

NO 7 COCCIDIOSIS/ MHARO DAMU.
_Dalili kuu: Kinyesi/mharo rangi ya ugoro mwanzo na unavyoendelea kinakuwa rangi ya damu.
Tiba: Amprolium 20%,Esb3, Trimazine 30%, Vitacox, na Agracox.

NO 8: FOWL CHOLERA/ KIPINDUPINDU CHA KUKU.
Dalili kuu: kinyesi mharo wa kijani.
Tiba: Trimazine 30 % au Esb3.

NO 9 MAGONJWA MATATIZO YANAYOTOKAN NA LISHE DUNI
_Kuvimba macho, miguu kukosa nguvu na kashindwa kusimama au kutembea, kutaga mayai tepetepe, kula mayai, kudonoana.
Tiba: Chakula kiwe na mchanganyiko mzuri wa mult vitamin na protein, kwa wanaodonoana kata au choma midomo yao na uwape mboga za majani ukiwa umezining'iniza juu kidogo.


Kama utawapa kuku wako wa wanaotaga mayai dawa zenye sulphur ndani watapunguza kutaga mayai, kwa hiyo kama utaweza kupata dawa ambayo haina sulphur ndani yake itakuwa ni vizuri zaidi

29 comments:

John Mwaipopo said...

habari Bennet
Hongera kwa kazi nzuri. Nimekutumia ujumbe kwenye e-mail. Au tuwasiliane 0757074566

Unknown said...

Nilikuwa nimechanganyikiwa juu kuku zangu zinaendelea kufa kwa hiyo ugojwa wa kufimba macho yani fowp pox , nimejaribu kupaka mafuta Badu zinaedelezi kufa

Unknown said...

Asante sana mtaalam wetu

Unknown said...

Asante kwa maelezo mazuri sana. Naomba kufahamu huo ugonjwa wa mahepe hauna Chanjo yake?.

Unknown said...

Vp umefikia wap wamebahatika kupona kweli

Unknown said...

Vp wamebahatika kupona

Abdallahamani103@gmail.com said...

Tuma E-mail yako ndug kwa info zaid

Unknown said...

Msaada kuhusu formula ya mchanganyiko(protein,vitamin) Kwa kuchanganya chakula chakula cha kuku broiler

Anonymous said...

Nimependa bwana mtaalamu ninaswali chumvi inaumuhim kwenye chakula chakuku

Anonymous said...

Nimependa bwana mtaalamu ninaswali chumvi inaumuhim kwenye chakula chakuku

Anonymous said...

Nimependa bwana mtaalamu ninaswali chumvi inaumuhim kwenye chakula chakuku

Unknown said...

Kuku wangu ni wakienyeji wanaharisha kinyesi cha kijani mwisho hufa

Unknown said...

Good inasaidia

Unknown said...

Hi! Ahsante kwa maelezo mazuri

Unknown said...

Kwa ndui haina tiba alisi ila tunaweza kupunguza vifo kwa kuwapa sawa za broad spectrum antibiotics Kama otc, tetracycline na uwape multivitamin kwa siku tano itasaid Sana ndugu yangu

Unknown said...

Habari kiongozi, ni atumaini yangu unaendelea vizuri. Samahani naweza kupata nakala zako za maonjwa na Je unaweza ukawa na nakala za magonjwa hata kwa dawa za asili. Na Je kama anaumwa Mafia makali naweza kumpa dawa za binadamu

Unknown said...

sawa utoe na utalamu jinsi gani ya kuwapa huduma kuku na bata.

Unknown said...

Msaanda, fomula ya chakula. raymahe@gmail.com

Unknown said...

Nashukuru bro kwa elimu hii japo na Mimi nimepitia ufugaji Ila napenda kufatilia kwako pia kuwa karibu yako zikitokea furusa tuambiane

Unknown said...

Nashkur nimepata kitu
Nafuga koroila Lon tangu wiki hii naona wanasinzia niwape dawa gani

Unknown said...

Kuku wangu wanasinzia na kuharisha na wanakufa kweli msaada maana leo wanasinzia wote

Benjamin Jongera said...

Asante sana kwa elimu

Unknown said...

asante kwa ushauri Mimi kukuwangu walianza kusinzia jana niliwanunulia OTC 50% nimeamka leo nimekuta 10 wamekufa wanamwezi na wiki moja

Unknown said...

Asante kwa ushauli wako

Unknown said...

Chanjo za ndui ni week ya tatu lakn kabla ya week hiyo Tayari vidonda sa inakuwaje hapo

said...

Kwa zaidi ya miaka 13 ya ndoa sikuweza kuzaa, naendelea kuharibika hata nikipata mimba, madaktari wote hawakuweza kunisaidia, hadi dada yangu akanielekeza kwa Dr DAWN, ambaye alinisaidia nikapata ujauzito na sasa hivi kuwa na mtoto mzuri wa kike,
Anasaidia pia marafiki zangu wengi niliowaelekeza, Dr DAWN ni baraka kwa kila mtu anayewasiliana naye,
*Kama unataka kupata mimba.
*Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
*Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
*Kama unataka mume/mkeo arudishwe.
*Kama unataka kurejesha mali yako iliyoibiwa au Pesa.
*Ukitaka kutibu aina yoyote ya ugonjwa,
Wasiliana naye kwa WhatsApp: +2349046229159

Mr keen vet said...

Kuku wangu wanamatatizo yafuatayo
-wanatoa majimaji machoni na kupelekea upofu
-pia Kuna kuku nimekuta sehemu ya kiza imetokeza kwa nje

Mr keen vet said...

Kuna kuku nimekuta sehemu ya kizazi imetokeza kwa nje kama kiuvimbe ivi

Laurent said...

Naomba msaada kuku wangu anaharisha kinyesi cha majimaji kijani