Nyanya ni aina ya mboga inayo zalishwa kwa wingi sana duniani. Kwa Tanzania, nyanya ni zao la kwanza katika mazao ya mboga linalo limwa na kuliwa kwa wingi ukilinganisha na mboga zingine. Nyanya hutumika karibu Katika kila mlo. Kulingana na umuhimu wa zao hili kama chakula na pia kama zao linalomwingizia kipato Mkulima, kuna haja ya kutoa mafunzo kuhusu mbinu bora za uzalishaji wake. Pia kuna umuhimu wa kufundisha wakulima kutoka sehemu zingine wasiolima zao hili ili nao waweze kuzalisha nyanya na hivyo kuongeza idadi ya aina za mboga katika maeneo yao.
Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya
joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa
maua na matunda. Zao hili hupenda kipindi kirefu cha jua na
joto ili kuongeza ukuaji wa matunda na kupunguza magonjwa ya aina
ya ukungu/kuvu. Zao hili halipendi mvua nyingi ingawa
linahitaji maji kwa wingi. Katika kipindi chenye mvua nyingi na
jua kidogo nyanya hushindwa kutoa maua na matunda ya
kutosha bali huweka majani mengi. Katika kipindi hiki pia,
nyanya hushambuliwa sana na magonjwa ya ukungu. Nyanya hupendelea udongo unaopitisha
maji kwa urahisi na wenye rutuba ya kutosha na hivyo
hupenda samadi. Udongo uwe umetifuliwa vya kutosha kuruhusu
mizizi kushika vema.
AINA ZA NYANYA
Kuna aina kuu mbili za nyanya kulingana
na ukuaji wa mmea: yaani nyanya inayo refuka zenye
kuhitaji egemezi (mfano Money maker) na aina ya pili ni nyanya
fupi zenye kutoa matawi mengi mfano Roma na Cal J.
UKUAJI WA MICHE
Miche ya nyanya huzalishwa kwenye
kitalu kwa kupanda mbegu. Mbegu za nyanya huota baada ya
siku 5 hadi 10. Baada ya kukua kitaluni kwa muda wa
wiki 4 hadi 5 toka kuota kwa mbegu, miche hupandwa shambani.
Kabla ya kupandikiza shambani miche huandaliwa kwa kupunguza
umwagiliaji maji kwa siku moja au mbili ili miche izoee
hali ngumu kabla ya kuhamishiwa shambani. Hapo shambani miche hupandikizwa kwa
kuzamishwa katika kina kirefu zaidi ya ilivyo kuwa
kitaluni. Hii inasaidia miche kutoa mizizi ya pembeni mingi zaidi kwa ajili
ya kufyonza maji pamoja na virutubisho aridhini. Baada ya kupandikiza mwagilia
maji ya kutosha. Usimwagilie maji juu ya mche
wa nyanya. Katika kipindi cha jua kali, tandaza nyasi
kwenye tuta ili kupunguza upotevu wa maji na unaweza kuweka
kivuli kwa kutumia majani ya miti au migomba. Kulingana na aina ya nyanya na rutuba
ya udongo, nafasi ya kupandia ni sm 60 kati ya mstari hadi
mstari na 45 hadi 60 nafasi ya mche hadi mche. Kama udongo
hauna rutuba ya kutosha inapendekezwa kutumia nafasi
kubwa ya kupanda.
UTUNZAJI
Nyanya fupi zisizo refuka kwenda juu,
ni rahisi sana kutunza na hazihitaji huduma nyingi. Tatizo kubwa
ni kuwa kwa kutambaa chini, katika kipindi cha mvua huwa
karibu na magonjwa yatokanayo na udongo. Katika kipindi
cha jua kali, matunda huungua kwani mmea huwa na majani
machache tu yanayo kinga matunda yasipigwe na mionzi ya
jua.
MBOLEA
Licha ya mbolea ya kupandia,
unashauriwa kuongeza mbolea kipindi cha wiki mbili au tatu baada ya
kupandikiza miche bustanini. Mbolea hii ya kukuzia iwekwe
kuzunguka shina la mmea kwa umbali wa sentimeta 5 hadi
saba kutoka kwenye shina. Kwa mbolea kama vile CAN, NPK,
au SA tumia kifuniko kimoja cha soda kwa shina. Mbolea hii
inaweza kuwekwa mara mbili kabla ya mvuno wa kwanza. Ili kurefusha kupindi cha uzaaji wa zao
la nyanya (na hata mazao mengine yatoayo matunda kama vile
nyanya chungu, biringanya, pilipili hoho, nk) inapaswa
kuongezea mbolea katika kipindi cha uvunaji mfano baada ya
kuvuna mara mbili unashauriwa kuongeza mbolea ya samadi
na mbolea kama vile NPK. Hii inasaidia mmea kuendelea kutoa
maua bila kuchoka. Kwa kawaida nyanya fupi jamii ya “Roma”
huweza kuzaa na kuvunwa kwa kipindi cha wiki 6 hadi 8
tu. Lakini kama utakuwa unaongezea mbolea na kukazania matunzo
ya bustani (hasa usafi wa bustani na Kumwagilia maji ya
kutosha), nyanya zinaweza kuendelea kuzaa kwa muda mrefu
zaidi. Hii ni tofauti
na mazoea ya wakulima wengi kuwa mara
nyanya zianzapo kuzaa huduma za palizi na usafi wa
shamba huachwa na kutilia maanani kazi ya kuvuna pekee. Hii
inajitokeza zaidi kwenye aina ya nyanya fupi.
Kwa nyanya fupi ni vizuri kuhakikisha
kuna matawi mengi iwezekanavyo ili kuweza kupata matunda
mengi zaidi. Hivyo usipunguze matawi katika aina hii ya
nyanya. Kwa nyanya ndefu zenye kuhitaji egemezi,tunashauriwa
kukuza nyanya kwa tawi moja lisilo na
vichipukizi pembeni au matawi mawili na kuacha mnyanya urefuke.
Kupunguza majani ni muhimu pia katika
kupunguza maambukizo ya ukungu katika shina na pia kutoa nafasi ili
mwanga kupenya na kuruhusu mzunguko wa
hewa. Majani yapunguzwe kipindi cha asubuhi kwa
kutumia mkono na siyo kisu kwani kinaweza kueneza magonjwa
kutoka mche hadi mche. Kwa nyanya ndefu, majani ya chini ya
matunda huondolewa kadiri unavyo endelea kuvuna. Unashauriwa
upunguze majani wakati wa asubuhi kwa kutumia mkono na
pia usitoe zaidi ya majani matatu katika mmea kwa mara
moja.
UMWAGILIAJI
Nyanya ni zao linalohitaji maji mengi
sana kwa ajili ya ukuaji wa mmea na matunda yake. Umwagiliaji uwe
wa kulingana kwa kila siku iliyo pangwa. Usibadilishe
ovyo kiasi cha maji na ratiba ya kumwagilia. Hii inasababisha kuoza
kwa kitako cha nyanya. Pia ili kutunza maji katika udongo,
inashauriwa kuweka matandazo katika mzunguko wa shina la
nyanya au bustani yote. Nyanya inayo kua vizuri hutumia
maji lita mbili kwa siku
katika kipindi cha jua kali. Hivyo
katika umwagiliaji ni busara kuzingatia kiasi hiki cha maji katika
kipindi kama hiki. Pia kama unatumia keni, mpira au bomba
usimwagilie maji juu ya matawi ya nyanya kwani umwagiliaji wa namna
hii utasababisha kuenea kwa magonjwa ya ukungu.
MATATIZO YA KILIMO CHA
NYANYA
Matatizo yanayosumbua kilimo cha zao
hili ni magonjwa na wadudu waharibifu. Hapa tutajifunza
mbinu mbali mbali za kuzuia magonjwa na wadudu waharibifu.
WADUDU WAHARIBIFU
FUNZA WA NYANYA (Funza wa vitumba)
Huyu funza hushambulia mazao mengine
kama vile pamba, mahindi, mtama, maharage n.k. Mdudu
huyu hushambulia matunda ya nyanya kwa kutoboa na hivyo
kuyafanya yapoteze soko kwasababu hayafai kuuzwa katika
soko na pia yanaweza kuoza wakati wa usafirishaji. Ili kuthibiti piga dawa ya kuua wadudu
kama vile thiodan, sevin ya unga, karate, selecron, n.k.
Muarobaini hutumika pia katika kupunguza uharibifu wa mdudu huyu.
INZI WEUPE
Wadudu hawa huruka ruka kwenye shamba la nyanya na kukaa chini ya majani. Mdudu huyu hueneza magonjwa ya virusi kama vile “ukoma wa nyanya”. Usafi wa shamba na mazingira ya yake ni muhimu katika kupunguza kuzaana kwa wadudu hawa. Ili kuthibiti wadudu hawa kwenye bustani ya mboga na pia katika maficho yao, piga dawa kama vile karate, cypermethrin mara kwa mara. Panda mimea mingine (kama vile tumbaku) inayo vutia wadudu hawa kwenye maeneo ya bustani kisha piga dawa katika miche ya tumbaku ili kuwaangamiza kwa wingi.
Wadudu hawa huruka ruka kwenye shamba la nyanya na kukaa chini ya majani. Mdudu huyu hueneza magonjwa ya virusi kama vile “ukoma wa nyanya”. Usafi wa shamba na mazingira ya yake ni muhimu katika kupunguza kuzaana kwa wadudu hawa. Ili kuthibiti wadudu hawa kwenye bustani ya mboga na pia katika maficho yao, piga dawa kama vile karate, cypermethrin mara kwa mara. Panda mimea mingine (kama vile tumbaku) inayo vutia wadudu hawa kwenye maeneo ya bustani kisha piga dawa katika miche ya tumbaku ili kuwaangamiza kwa wingi.
MINYOO
Mdudu huyu hukaa kwenye udongo wenye unyevu wa kutosha. Huvamia mizizi ya
nyanya na kuharibu mfumo wa usafirishaji maji na
chakula kwenye nyanya iliyo athirika. Uking'oa
mche wa nyanya utaona vifundo kwenye mizizi.
KUZUIA
Mbinu za kuthibiti ongezeko la wadudu
hawa ni kuharibu hali ya udongo inayo mfanya aishi na kuzaana.
Mbinu hizi ni: Kulima shamba kwa
kutifua baada ya kuvuna nyanya ili udongo wa chini ukae juani na kukauka.
Hii inasaidia kuangamiza wadudu hawa kwa joto na
ukosefu wa maji. Choma moto na
kuteketeza mabaki ya nyanya baada ya kuvuna. kuzungusha aina ya zao
la nyanya au jamii ya nyanya na mazao mengine yasiyo vamiwa na adui
huyu. Hii huwafanya minyoo wasipate hifadhi na
chakula kutoka kwenye mimea wanayo tumia kuishi na
kuzaliana. Hivyo idadi yao kupungua katika udongo. kabla ya kupanda zao
weka samadi nyingi katika udongo kwenye eneo lililo athiriwa na wadudu
hawa kwani hawapendi udongo wenye samadi nyingi. Panda manung'a nung'a
(Tagetes spp) katika eneo lililoathirika na minyoo hawa, mimea
hii hutoa sumu ya aina fulani ambayo huathiri ukuaji na
kuzaliana kwa minyoo hawa.
MAGONJWA
Uchunguzi umeonyesha kuwa katika maeneo
ya Kilombero na Gairo, nyanya na mazao mengine jamii ya
nyanya ndiyo hushambuliwa sana na magonjwa kuliko
mazao mengine ya mboga.
UKUNGU
Huu ni ugonjwa unaopenda hali ya unyevu
mwingi hewani. Hivyo hujitokeza zaidi wakati wa
masika. Pia sehemu zenye umande mwingi wakati wa usiku, ugonjwa huu hujitokeza
hata wakati wa kiangazi.
DALILI ZAKE
Ugonjwa huu hushambulia shina, maua na
matunda. Kuungua kwa majani kama vile yamechomwa na maji
moto. Chini ya jani utaona unga unga mweupe. Matunda pia
hushambuliwa na ugonjwa huu na hugeuka kuwa meusi na
magumu.
KUZUIA
Inabidi kuchanganya
mbinu mbali mbali za kupambana na ugonjwa huu. Kwanza ni usafi wa
shamba kwa jumla yaani hakikisha unaondoa magugu katika
bustani. Tandaza nyasi juu ya
matuta yaliyo pandwa nyanya. Ondoa majani yaliyo
zeeka na yanayo onyesha dalili za ugonjwa huu. katika kupunguza majani,
hakikisha sehemu za chini ya mmea ni wazi na kuna
mzunguko mzuri wa hewa. Punguza majani katika
mmea ili kupunguza umande na ukungu kwenye mmea. Baada ya kupunguza
majani na machipukizi hakikisha unatupa mbali majani hayo na siyo
kuyaacha kwenye tuta la bustani. Ondoa kabisa mmea ulio
na dalili za ugonjwa huu Kupiga dawa katika
kipindi cha mvua mara baada ya mvua kubwa. Fanya hivyo mara moja au
mara mbili kwa wiki kutegemea na wingi au
mfululizo wa mvua. Unapoona jua limetoka piga dawa ili
ugonjwa usijitokeze tena. Baadhi ya madawa yanayofaa kukinga
ugonjwa huu ni Dithane M45, Bravo, Benlate , Ridomil, Topsin
n.k. Kumbuka kuwa kila
mwaka madawa yenye nguvu zaidi
hutengenezwa, hivyo uliza watalaam walioko karibu nawe. Ingawa
Blue Copper inauzwa kwa bei nafuu, nguvu yake in kidogo
sana kuthibiti huu ugonjwa. Muarobaini pia unaweza kutumika
kupunguza ugonjwa huu. Changanya unga unaotokana na mbegu za
muarobaini kiasi cha nusu kilo ya unga katika lita 20 za
maji.
UKOMA WA NYANYA
Huu ni ugonjwa wa virus unao enezwa na
inzi mweupe. Inzi hawa hushambulia zaidi nyanya wakati wa
kiangazi, hasa kipindi cha joto kali.
DALILI
Majani machanga
hujikunja na baadaye majani yote. Kupungua kwa utoaji
maua na matunda na hata yakitokea matunda huwa ni madogo. Mmea kudumaa na
kutozaa kabisa.
KUZUIA
KUZUIA
Mbinu madhubuti ni kupunguza kuenea kwa
ugonjwa huu kwenye shamba kwa kudhibiti kuzaana na
kuenea kwa mdudu (inzi mweupe) kama tulivyo ona katika
kupambana na mdudu huyo, yaani: Kuondoa mimea michache
iliyo shikwa na ugonjwa maana wadudu hawa wanachukua ugonjwa
huu kutoka mimea hii. Kutumia mbegu zilizo
hakikishwa kuwa zinaweza kuvumilia ugonjwa huu na kutoa mavuno
mazuri. Usilime nyanya karibu
na eneo lililo na mazao kama bamia,mipapai maana mimea hii huhifadhi
inzi mweupe. Kuua inzi weupe wanaofyonza nyanya na kusambaza virusi kwa kutumia madawa. Tumia madawa
kama vile Selecron, Decis, Karate n.k. Epuka kuchanganya zao
la nyanya na mazao mengine yanayohifadhi hawa nzi kama vile
mipapai na bamia. Ng'oa na kuchoma moto
mimea yote iliyougua ugonjwa huu.
UGONJWA WA KUOZA
SEHEMU YA SHINA INAYOGUSA UDONGO NA MMEMA KUNYAUKA KAMA UMEKOSA MAJI
Wadudu wanaosabisha
ugonjwa huu hupatikana ardhini. Hakuna dawa ya kutibu
ugonjwa huu baada ya dalili
kujitokeza. Kupiga madawa za
viwandani ardhini kabla ya kupanda nyanya husaidia kupungu wadudu wa
ugonjwa. Epuka kupanda nyanya
au mazao jamii ya nyanya katika eneo moja kwa muda mrefu mfulilizo. Baadhi ya mazao yanayohusiana na nyanya ni bilinganya,
pilipili, ngogwe, mnavu, n.k.
Ugonjwa wa miche michanga ya nyanya kuoza sehemu ya shina inayogusa udongo na kufa ghafla
Ugonjwa wa miche michanga ya nyanya kuoza sehemu ya shina inayogusa udongo na kufa ghafla
Ugonjwa huu hushambulia miche kitaluni
na husabishwa na wadudu waishio ardhini. Mara baada ya
dalili, ugonjwa huu hauna dawa ila unaweza kukingwa kwa
kutumia njia zifuatazo: Choma moto udongo wa kutengenezea kitalu kabla ya kupanda mbegu zako. Kutumia mboji
husaidia kukinga miche dhidi ya ugonjwa huu. Epuka kumwagilia maji
kupita kiasi na kutumia kuvuli kizito
MATUNDA YA NYANYA
KUOZA KITAKO
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na: Umwagiliaji wa nyanya
bustanini usio na mpangilio maalumu. Mfano, kumwagilia mimea maji
mengi kisha kuiacha bila maji kwa siku kadhaa. Upungufu wa
virutubisho aina ya chokaa. Dalili zake ni matunda ya nyanya kuoza
sehemu ya kitako na kuonyesha rangi nyeusi. Kuzuia ugonjwa huu, zingatia kuwa na
utaratibu mzuri wa kumwagilia maji ambao haubadiliki ovyo
kiratiba na kiasi cha maji
2 comments:
Mbonaa nikipiga sim haipatikani
Kwa zaidi ya miaka 13 ya ndoa sikuweza kuzaa, naendelea kuharibika hata nikipata mimba, madaktari wote hawakuweza kunisaidia, hadi dada yangu akanielekeza kwa Dr DAWN, ambaye alinisaidia nikapata ujauzito na sasa hivi kuwa na mtoto mzuri wa kike,
Anasaidia pia marafiki zangu wengi niliowaelekeza, Dr DAWN ni baraka kwa kila mtu anayewasiliana naye,
*Kama unataka kupata mimba.
*Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
*Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
*Kama unataka mume/mkeo arudishwe.
*Kama unataka kurejesha mali yako iliyoibiwa au Pesa.
*Ukitaka kutibu aina yoyote ya ugonjwa,
Wasiliana naye kwa WhatsApp: +2349046229159
Post a Comment