MAHITAJI
Hali ya hewa inayofaa
kwa mipapai ni ya kitropik ambayo haina baridi kali na joto kiasi . Udongo usiotuamisha
maji maji yakisimama kwa masaa 48 tu mpapai unaweza kufa, wenye ruruba ya
kutosha kwa sababu mipapai haina mzizi mkuu haihiyaji udongo wenye kina kirefu,
kipindi cha jua kali mpapai usiachwe zaidi ya wiki 8 bila kumwagiliwa maji kama
hakuna mvua ingawa wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hii huongeza
ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema sokoni
Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mwingi kwani
huvunjika kirahisi, kama unashamba la mipapai itakubidi kupanda miti ya kukinga
upepo kuzunguka shamba lako, miti kama miparachichi, migravilea, vibiriti (leucaena Spp) na miembe pia
inafaa. Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai kwa mita
10 mpaka 20 juu zaidi
Kuendelea kupanda mipapai kwenye shamba moja kunaweza
kusababisha usugu wa magonjwa, nashauri baada ya miaka 3 – 5 ubadilishe zao
hili angalau kwa msimu mmoja ili kuua mzunguko wa magonjwa
Mipapai inaweza kuchanganganywa na miembe na mimea jamii ya
michungwa, pia mazao ya msimu kama mahindi, mtama, ufuta , alizeti na
mboga mboga yanaweza kulimwa
Kwa kaida kwenye mipapai kuna mipapai dume, majike na yenye jinsia zote (multiplesex/hermaphrodite)
ambayo huwa na mapapai marefu zaidi, na pia kuna isiyoeleweka ambayo huwa na
mapapai mafupi sana
MBEGU
Kusanya mbegu toka kwenye mapai makubwa na yaliyo komaa na
kuiva, kausha mbegu vizuri kbla ya kupanda, kama utapata mbegu za kununua ni vizuri zaidi, baada ya kukausha
hakikisha unazipanda ndani ya wiki moja
KUOTESHA MBEGU
Kuna wanaopendelea kuotesha mbegu kwanza na kisha kuhamishia
miche shambani, sehemu ya kuoteshea iandaliwe miezi miwili kabla, mbegu
zioteshwe kwenye kina kati ya sentimeta 1 – 2 chini ya udongo wenye rutuba au
pakiti za plastiki, kiwango bora cha joto ni sentigredi 21 – 27 na itachukua
kati ya wiki 1 – 4 kwa mbegu kuota, kwenye kila pakiti weka mbegu 2 – 3. Panda mbegu
zako kwenye kitalu kwa umbali wa sentimeta 3 toka shimo hadi shimo na sentimeta
15 kati ya mistari, hakikisha maji hayatuami kabisa, pia unaweza kupiga dawa ya
copper oxychloride gramu moja katika lita moja ya maji ilikukinga miche yako na
fangasi
UOTESHAJI WA MOJA KWA MOJA
Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea
ya kuku sehemu ya kupandia, mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia
kukinga mipapai na magonjwa. Panda mbegu 3 – 5 kila shimo maana miche mingine
inaweza kufa kwa magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota dume
KUHAMISHA MICHE TOKA KWENYE KITALU
Miche ihamishiwe shambani ikiwa na urefu wa sentimeta 20 –
40, kama udongo unatuamisha maji panda kwenye matuta yenye urefu wa sentimeta
40 – 60 mashimo yawe na ukubwa wa sentimeta 45 upana na sentimeta 30 kina na
shimo lichanganywe na udongo na samadi bila kuacha kisahani cha maji, umbali ni
mita 3 kwa 3 kwani mipapai inahitaji jua la kutosha
KUPUNGUZA MIPAPAI
Baada ya miezi 3 – 5 baada ya kupanda mipapai itatoa maua na
hapo jinsia ya mipapai itajulikana na mingine itabidi ipunguzwe na hasa midume,
mipapai yenye jinsi zote inatakiwa isizidi asilimia 10 – 20 na midume ibaki
mmoja katika kila mijike 25, mimea yenye magonjwa pia inabidi ing’olewe
RUTUBA YA UDONGO
Weka kiasi chakilo 2 – 5 za samadi kwenye kila mpapai kwa
mwaka ili kuongeza ukuaji na uzazi, mabaki ya mimea yanaweza pia kuwekwa kama
matandazo na h ii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu
usipotee.
MAGUGU
Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka
ili kuzuia uoataji wa magugu, magugu yang’olewe yakiwa machanga na epuka
kuchimbua chini sana maana mizizi ya mipapai huwa juu juu, njia nzuri ni kuweka
matandazo kwenye shamba lote ili kuzuia outaji wa magugu
UANGALIZI
- Mipapai iangaliwe dhidi ya magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au kufukiwa chini ikiwa itabainika kuwa na maonjwa, piga dawa dhidi ya magonjwa ya fangasi na virusi mara yanapoibuka ili kuongeza uzaaji nakipato chako
- Ondoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na hii ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.
- Ondoa mapapi yote ambayo yatakuwa hayakuchavuliwa vizuri na acha yale yenye afya tu
- Weka miti ya kuegemea kama mpapai utazaa matunda mengi na hasa wakati wa upepo mwingi ili kuzuia mipapai isivunjike
- Mipapai ikitunzwa inaweza kuishi mika mingi, ila kwa ajili ya mazao bora ondoa mipapai na upande mingine baada ya kila miaka mitatu (3) kwani mpapai unapo kuwa mkubwa basi rutuba yote huishia kwenye mti wenyewe
21 comments:
Mkuu kwanini wewe usichaguliwe kuwa mbunge, wa `kilimo kwanza' maana hii kilimo kwanza naona kama ngonjera ya kufikirika!
Nashukuru sana kwa ushauri wako
Uncle,
Napenda sana pos zako.
Je, naweza kukupata vipi kwa ushauri zaid juu ya kilimo?
Papai zao zuri sana na kama ukipanda eka moja kwa 1000 mapapai utapata 1kila wiki, ukiuza 1000 kwa 300 tu ni laki 3 sasa ukiweka eka 5 ni 1.5m kwa wiki...dahhhh....Tanzania nzuri unataka kenda wapi? Lima ww?
wewe Mr primus umelima? you should lead by example.where is your shamba darasa tuje kujifunza kwa cc wajasilia mali.
kaka nakukubali cna,
nimegraduate from Sua bt still am learning a lot from ur site,
keep it up !!
napenda post zako, keep it up
mwaka jana mwezi wa 12 nilipanda papai katika shamba,mpaka hii leo nina mipapai 300 ambayo sasa inatengeneza matunda lakin kuna miti ambayo tayali ilisha zaa na matunfa meng nimeuza na kula...jaman kama unashamba komaa upande mipapai inalipa sana. wakati wa upandaj changamoto ni kidogo cha msing aldh alimwe vizur kwa trecta au ngo'mbe ili udongo uwe lain kwa mizizi ya mipapai ni lain sana haiwezi kupambana na aridh ngumu sana..
nashkuru mtaalam kwa maalezo yako ila ss wengine ndo kwanza tunataka tuanze ukulima wa mipapai ila sijui nianzeje maana nina eneo la wastani nataka nipande ila naomba maelezo zaidi vipi nianze.
Yanachukua muda gan kukua
George
naona una uzoefu tyr,kwenye zao hili kwa sababu unalima tyr,unapatikana wapi wewe nahitaji nione shamba lako nipate elimu zaidi kwa vitendo.
Hi George
Tunashukuru kwakuwa mwenzetu unao uzoefu wa papai kwasasa mana umeshalima , ombi langu je mbegu bora za papai ulipata wap na kwa bei gan? mana ,kuna makala ya Mkulima mbunifu yeye kazungumzia mbegu ya Red royal F1 ila bei yake pale kuna wadau walisema punje 50 ni elf 18, na Mkilima mbunifu akasema mbegu hii huvunwa mapema zaidi na na mfululizo kwa miaka 5 hadi 7 hivyo tunaomba ushauri kwako ambaye umeshapanda jee umetumia mbegu gan?.
Pia kuna na mtu nilimpgia cm akanambia gram 50 ya mbegu ya papai anauza 250,000/=, sasa wewe ukitusaidia itakuwa vizuri kujua eka moja unaweza panda miche mingapi.
Watanzania wenzangu wapenda fursa kwa heshima na Taadhima napenda niwapongeze sana kwa kupenda fursa hii ya kilimo pia ningependa kuwakaribisha kwa undani zaidi katika Group letu maalum lifahamikalo kama Bunge la uchumi BU huku utakutana na watekelezaji wa fursa kama hii Kuna spika pamoja na naibu spika wanaotoa mafunzo haya yakinifu zaidi follow my contacts to be directed
Naomba contact za Hilo group, je ni WhatsApp?
Mipapai yangu ina kama miezi miwil hv na nusu tokea nipande, na ukubwa wake kwa inayoenda vinzur ni sm kama 50-70 hv, je kwel itakuwa na uwezo wa kuzaa ndan ya miez mitano? Na kama sio tatizo litakuwa ni nini?
Ahsante
Naomba na Mimi kuunganishwa katika hilo group
Naomba na Mimi kuunganishwa katika hilo group
Asante kwa maelezo mazuri nimekuelewa
Asante kwa maelezo mazuri nimekuelewa
naomba kujiunga na group la kilimo hilo.
Post a Comment