Moja ya matatizo makubwa ya uzalishaji wa zao la
korosho ni ugonjwa wa Ubwiri unga.Ugonjwa huu unasababishwa na vimelea aina ya uyoga (fungus) viitwavyo
Oidium anacardii. Ugonjwa huu ni muhimu sana, kiasi kwamba kama
haukuthibitiwa, unaweza kupunguza mavuno
kwa zaidi ya asilimia 70. Ugonjwa huu
umeenea katika mikoa yote inayolima zao hili Tanzania. Hapo awali ugonjwa huu ulikuwa unaitwa kwa
jina la“ukungu” kutokana na uhusiano wake mkubwa na haliya hewa ya ukungu (litabwe
kwa Kimakonde) unaoonekana alfajiri/asubuhi katika miezi ya Juni - Septemba. Hivyo
basi, jina la Ubwiri unga
linatumika sasa ili kuwawezesha wakulima wasichanganye vitu hivyo viwili.
MASHAMBULIZI
Ugonjwa huu unashambulia maeneo yote machanga na teketeke katika
mti wa mkorosho, hasa machipukizi, majani, maua, mabibo na korosho
changa (tegu). Athari kubwa ya
ugonjwa huu inatokana na mashambulizi ya
maua, ambayo hushindwa kufunguka na kuwezesha chavua kufanya kazi yake, hatimaye
hunyauka na kukauka.
DALILI
Maeneo yaliyoshambuliwa na ugonjwa huu, hufunikwa na unga
unga mweupe au wakijivujivu ambao huonekana
kama vumbi vumbi. Vimelea au chembe chembe zinazoshambulia ni ndogo ndogo sana na
hazionekani dhahiri kwa macho, ila kwa darubini. Chembe chembe hizi
zinapozaliana kwa wingi katika maeneo ya mshambulizi, ndipo huonekana kama unga
unga mweupe/kijivu.
KWENYE MAJANI
Pamoja na kufunikwa na unga unga, majani yaliyoshambuliwa husinyaa, hubadilika
rangi, wakati mwingine hukunjamana. Majani machanga zaidi yanaweza kupukutika,
ambapo yale yaliyokomaa hayashambuliwi. Masalia ya mashambulizi kwenye majani yaliyokomaa, huonekana kama
mabaka ya kahawia, hata hivyo hayapukutiki.
KWENYE MAUA
Maua yanaweza kushambuliwa hata kabla ya kuchanua. Pamoja na
kufunikwa na unga unga weupe/kijivu, maua yaliyoshambuliwa sana
hushindwa kuchanua na hatimaye hukauka kabisa na kuwa kama
“majani yachai”. Hili ndilo sababisho kubwa la upungufu wa zao la korosho.
KWENYE MABIBO
Mabibo yaliyoshambuliwa huonyesha unyafuzi,hupasuka pasuka na ngozi yake
huonekana kuwa chafu. Hatimaye,
mabibo hayo huwa madogo kwa umbo,
yenye maji kidogo sana, hivyo kuyafanya maji yake kuwa matamu
sana.
KWENYE TEGU NA KOROSHO
Tegu
zilizoshambuliwa huweza
kubadilika rangi yake ya kijani/nyekundu na kuwa ya hudhurungi au bluu iliyo
mzito. Tegu zikishambuliwa zingali changa sana, huweza kupukutika. Tegu
zilizoshambuliwa zikifikia kukomaa, zinaonyesha uharibifu mkubwa wa ngozi yake
na huonekana chafu, hatimaye, wakati wa mauzo hutengwa katika daraja
lachini (grade II).
KUSTAWI KWA UBWIRI UNGA
Vimelea vya Ubwiri unga vinaishi kwenye mimea iliyo hai tu,
haijawahi kuoteshwa katika maabara. Ugonjwa huu hushamiri na kustawi vizuri
katika majira yenye ukungu, hasa kuanzia mwezi Mei/Juni hadi Septemba karibu
kila mwaka. Mazingira mwafaka kwa ugonjwa huu ni:
• Joto: 26 - 28 0C (bora 25 C)
• Unyevu (RH): 80-100% (bora 95%)
Ubwiri unga pia hupendelea
zaidi mikorosho iliyosongamana na isiyopitisha hewa vizuri. Ugonjwa huu
hupendelea mazingira ya kiangazi, hasa
kuanzia mwezi Juni hadi Septemba, haupendelei hali ya mvua na joto jingi.
Hivyo basi, katika miezi mingine (hasa wakati wa masika), vimelea
hujificha na kuishi Kwenye maotea au
machipukizi uvunguni mwa mikorosho au kwenye
maua yasiyo ya msimu. Hivi ndivyo vyanzo
vya Ubwiri unga, vyenye uwezo wa kuhifadhi ugonjwa msimu hadi mwingine. Ugonjwa
huu husambazwa kwa upepo ambao nao pia hushamiri
sana katika miezi ya Mei/Juni hadi Septemba.
KUDHIBITI
Zipo njia aina tatu zinazotumika kuthibiti Ubwiri unga, nazo
ni mbinu za asili, mbegu bora na madawa.
MBINU ZA ASILI
(Cultural control)
Kuondoa vyanzo vya
Ubwiri unga (sanitation).
Hii ni kazi ya mikono ya kuondoa machipukizi na maotea yanayojificha
kwenye uvungu wa mikorosho, kutumia vifaa kama vile upanga,
mundu, shoka nk. Msingi wa kazi hii ni kupunguza kasi ya ugonjwa huu katika
shamba kwa kuchelewesha mlipuko na kasi
ya mashambulizi.
Kubadili mazingira ya
ugonjwa katika miti.
Kupunguzia
matawi (prunning) ya mikorosho
ili kufanya umbile la
mwamvuli katika miti, ili kuruhusu joto na upepo kupenya kirahisi,
inasaidia sana kuthibiti Ubwiri unga.
Kupunguza miti (thinning)
iliyosongamana na kuacha nafasi ya kutosha kati
ya miti, itasaidia kupunguza kuenea kwa ugonjwa. Miti ikiwa
katikanafasi ya kutosha,
itawezesha hewa kupenya vizuri na kubadili mazingira ili yasiwe
mazuri kwa kustawi kwa ugonjwa.
Kupanda mikorosho
inayovumilia/kuhimili ugonjwa.
Ipo baadhi ya mikorosho
ambayo inaweza kuhimili mashambulizi ya ugonjwa hata
kuweza kutoa Mazao bila ya kutumia kinga yoyote. Aina zingine zinaweza kutoa maua na kuzaa
kabla ya
athari za ugonjwa hata kuweza kukwepa mashambulizi. Hii
ni baadhi ya mikorosho
bora ambayo hatimaye imepandwa
katika eneo moja katika vituo vyetu
vyote vya kuendeleza korosho (Cashewnut Development Centre )kama NALIENDELE.
Mbegu zinazopatikana toka mashamba hayo ni mbegu bora (polyclonal seed) ambazo
zinaweza kuzaa bila madawa, lakini huzaa vizuri zaidi kama mtu atatumia dawa
pia.
MATUMIZI YA MADAWA
Dawa ya Salfa
(Sulphur)
Salfa ndiyo dawa inayotumika kwa wingi zaidi kukinga ugonjwa
wa Ubwiri unga. Dawa hii ambayo ni ya unga, inapulizwa kwa kutumia mashine
maalumu (motorised blower) ya kupulizia
dawa k.m. Maruyamana Solo. Kiwango cha
gramu 250 kwa mti, kwa mzunguko,
ndicho kinapendekezwa. Hivyo basi kwa
mizunguko mitano kiasi cha kilo 1.25
cha salfa kwa mti kwa mwaka kinahitajika. Pia kuna salfa za maji kama Thiovit ambazo unaweza
kupulizia kwa kutumia vinyunyuzia dawa vya kawaida (knapsack sprayer)
Wakati wa kuanza kupulizia
sailfa
Mpulizo wa kwanza unaanza ambapo karibu asilimia 20za maua
yamejitokeza na wakati sawa, zaidi ya asilimia 5 ya maua hayo tayari yawe yanaonyesha dalili za ugonjwa. Upimaji wa maua ili kujua lini
upuliziaji uanze, inasaidia
kufanya matumizi sahihi ya dawa,
hatimaye faida/pato litakuwa kubwa kwa mkulima.
Inashauriwa kwamba upuliziaji ufanyike asubuhi na mapema,
wakati ambapo kuna umande. Asubuhi, upepo nao
huwa hauna nguvu sana na
inashauriwa upuliziajiusizidi ya saa 3 asubuhi. Umande unasaidia salfa ya unga iweze
kunata kwenye majani na maua. Ila kwa salfa ya maji kama thiovit unaweza
kupulizia wakati wowote.vipindi vifuatavyo, vimependekezwa katika upuliziaji:Siku
14 14
14 21 21
Dawa zingine badala
ya salfa.
Madawa kadha wa kadha yamefanyiwa utafiti sambamba na salfa. Aina tatu za dawa
hizo (waterbased organics), zimependekezwa kwa matumizi ya wakulima,
nazo ni Bayfidan, Anvil na Topas. Kiwango
cha upuliziaji ni ml 10 - 15 za dawa ndani ya0.75 -
1.25 za maji kutegemeana na ukubwa wa mti. Vipindi
kati ya mipulizo ni wiki tatu (siku
21) na awamu (raundi) 3 zinatosha
kwa msimu. Inashauriwa kwamba kutokana na gharama za dawa yamaji, zinafaa
zitumike kwenye mikorosho ambayomkulima ana uhakika wa kutoa zaidi ya kilo 4
baada ya kupulizia. Miti inayotoa chini
ya kiasi hicho heri isipuliziwe, vinginevyo italeta hasara
2 comments:
Nimefurahi sana kusoma utaalamu huu katika blogger. nataka kuuliza katika heka moja ni miche mingapi ya mahindi inastahili kuwepo ili kutoa matokeo mazuri kujua kila heka utapata gunia ngapi?. vivyo hivyo kwa ufuta na halizeti ukizingatia kupanda kwa mistari?. mlangwaa@yahoo.com
Nataka kujua kuhusu nikitaka kuanzisha ugugaji wa samaki vitu gani vya muhimu vya kuanza navyo
Post a Comment