Moja ya matatizo makubwa ya uzalishaji wa  zao  la
korosho ni ugonjwa wa Ubwiri unga.Ugonjwa huu unasababishwa  na vimelea aina ya uyoga (fungus) viitwavyo
Oidium anacardii. Ugonjwa huu ni muhimu sana, kiasi kwamba kama
haukuthibitiwa,  unaweza kupunguza mavuno
kwa zaidi ya asilimia 70.       Ugonjwa huu
umeenea katika  mikoa  yote inayolima zao hili Tanzania.  Hapo awali ugonjwa huu ulikuwa unaitwa kwa
jina la“ukungu” kutokana na uhusiano wake mkubwa na haliya hewa ya ukungu  (litabwe 
kwa  Kimakonde) unaoonekana  alfajiri/asubuhi katika miezi ya Juni - Septemba.  Hivyo 
basi,  jina la Ubwiri unga
linatumika sasa ili kuwawezesha wakulima wasichanganye vitu hivyo viwili. 
MASHAMBULIZI
Ugonjwa huu unashambulia maeneo yote machanga na teketeke  katika 
mti wa mkorosho, hasa machipukizi, majani, maua, mabibo na korosho
changa (tegu). Athari kubwa  ya
ugonjwa  huu inatokana na mashambulizi ya
maua, ambayo hushindwa kufunguka  na  kuwezesha chavua kufanya kazi yake,  hatimaye 
hunyauka  na kukauka. 
DALILI
Maeneo yaliyoshambuliwa na ugonjwa huu, hufunikwa na unga
unga mweupe au wakijivujivu  ambao huonekana
kama vumbi vumbi. Vimelea au chembe chembe zinazoshambulia ni ndogo ndogo sana na
hazionekani dhahiri kwa macho, ila kwa darubini. Chembe chembe hizi
zinapozaliana kwa wingi katika maeneo ya mshambulizi, ndipo huonekana kama unga
unga mweupe/kijivu.  
KWENYE MAJANI
Pamoja na kufunikwa na unga unga,  majani yaliyoshambuliwa husinyaa, hubadilika
rangi, wakati mwingine hukunjamana. Majani machanga zaidi yanaweza kupukutika,
ambapo yale yaliyokomaa hayashambuliwi. Masalia ya mashambulizi  kwenye majani yaliyokomaa, huonekana kama
mabaka ya kahawia, hata hivyo hayapukutiki.
KWENYE MAUA
Maua yanaweza kushambuliwa hata kabla ya kuchanua. Pamoja  na 
kufunikwa na unga unga weupe/kijivu, maua yaliyoshambuliwa sana
hushindwa  kuchanua  na hatimaye hukauka kabisa na kuwa kama
“majani yachai”. Hili ndilo sababisho kubwa la upungufu wa zao la korosho. 
KWENYE MABIBO
Mabibo yaliyoshambuliwa huonyesha  unyafuzi,hupasuka pasuka na ngozi yake
huonekana kuwa chafu. Hatimaye, 
mabibo  hayo huwa madogo kwa umbo,
yenye  maji kidogo  sana, hivyo kuyafanya maji yake kuwa matamu
sana. 
KWENYE TEGU NA KOROSHO
Tegu 
zilizoshambuliwa  huweza
kubadilika rangi yake ya kijani/nyekundu na kuwa ya hudhurungi au bluu iliyo
mzito. Tegu zikishambuliwa zingali changa sana, huweza kupukutika. Tegu
zilizoshambuliwa zikifikia kukomaa, zinaonyesha uharibifu mkubwa wa ngozi yake
na huonekana chafu, hatimaye, wakati wa mauzo hutengwa katika  daraja 
lachini (grade II). 
KUSTAWI KWA UBWIRI UNGA 
Vimelea vya Ubwiri unga vinaishi kwenye mimea iliyo hai tu,
haijawahi kuoteshwa katika  maabara.  Ugonjwa huu hushamiri na kustawi vizuri
katika  majira  yenye ukungu, hasa  kuanzia mwezi Mei/Juni hadi Septemba karibu
kila mwaka. Mazingira mwafaka kwa ugonjwa huu ni:
• Joto: 26 - 28 0C (bora 25 C) 
• Unyevu (RH): 80-100% (bora 95%) 
Ubwiri unga pia hupendelea 
zaidi mikorosho iliyosongamana na isiyopitisha hewa vizuri. Ugonjwa huu
hupendelea mazingira ya kiangazi, hasa 
kuanzia mwezi Juni hadi Septemba, haupendelei hali ya mvua na  joto jingi. 
Hivyo basi, katika miezi mingine (hasa wakati wa masika), vimelea
hujificha na kuishi Kwenye maotea  au
machipukizi uvunguni  mwa mikorosho au kwenye
maua yasiyo ya msimu. Hivi ndivyo  vyanzo
vya Ubwiri unga, vyenye uwezo wa kuhifadhi ugonjwa msimu hadi mwingine. Ugonjwa
huu husambazwa kwa upepo ambao nao  pia hushamiri
sana katika miezi ya Mei/Juni hadi Septemba. 
KUDHIBITI
Zipo njia aina tatu zinazotumika kuthibiti Ubwiri unga, nazo
ni mbinu za asili, mbegu bora na madawa. 
MBINU ZA ASILI
(Cultural control) 
Kuondoa vyanzo vya
Ubwiri unga (sanitation). 
Hii ni kazi ya mikono ya kuondoa machipukizi na maotea yanayojificha
kwenye uvungu  wa  mikorosho, kutumia vifaa kama vile upanga,
mundu, shoka nk. Msingi wa kazi hii ni kupunguza kasi ya ugonjwa huu katika
shamba kwa kuchelewesha mlipuko na  kasi
ya mashambulizi.  
Kubadili mazingira ya
ugonjwa katika miti. 
Kupunguzia 
matawi  (prunning) ya mikorosho
ili kufanya  umbile  la 
mwamvuli katika miti, ili kuruhusu joto na upepo kupenya kirahisi,
inasaidia sana kuthibiti Ubwiri unga. 
Kupunguza  miti (thinning)
iliyosongamana na kuacha nafasi ya kutosha kati 
ya miti, itasaidia kupunguza kuenea kwa ugonjwa.  Miti ikiwa 
katikanafasi  ya kutosha,
itawezesha hewa  kupenya  vizuri na kubadili mazingira ili yasiwe
mazuri kwa kustawi kwa ugonjwa. 
Kupanda mikorosho
inayovumilia/kuhimili ugonjwa. 
Ipo baadhi ya mikorosho 
ambayo  inaweza  kuhimili mashambulizi ya ugonjwa hata
kuweza  kutoa  Mazao bila ya kutumia kinga yoyote.  Aina zingine zinaweza kutoa maua na kuzaa
kabla  ya 
athari za ugonjwa hata kuweza kukwepa mashambulizi.  Hii 
ni  baadhi  ya mikorosho 
bora  ambayo hatimaye imepandwa
katika eneo moja katika vituo  vyetu
vyote vya kuendeleza korosho (Cashewnut Development Centre )kama NALIENDELE.
Mbegu zinazopatikana toka mashamba hayo ni mbegu bora (polyclonal seed) ambazo
zinaweza kuzaa bila madawa, lakini huzaa vizuri zaidi kama mtu atatumia dawa
pia. 
MATUMIZI YA MADAWA
Dawa ya Salfa
(Sulphur) 
Salfa ndiyo dawa inayotumika kwa wingi zaidi kukinga ugonjwa
wa Ubwiri unga. Dawa hii ambayo ni ya unga, inapulizwa kwa kutumia mashine
maalumu (motorised blower)  ya kupulizia
dawa k.m. Maruyamana Solo. Kiwango cha 
gramu  250 kwa mti, kwa mzunguko,
ndicho kinapendekezwa.  Hivyo basi kwa
mizunguko mitano kiasi cha kilo 1.25 
cha  salfa kwa mti kwa mwaka kinahitajika.  Pia kuna salfa za maji kama Thiovit ambazo unaweza
kupulizia kwa kutumia vinyunyuzia dawa vya kawaida (knapsack sprayer)
Wakati wa kuanza kupulizia
sailfa
Mpulizo wa kwanza unaanza ambapo karibu asilimia 20za maua
yamejitokeza na wakati sawa, zaidi ya asilimia 5 ya maua hayo tayari yawe  yanaonyesha dalili  za ugonjwa. Upimaji wa maua ili kujua  lini 
upuliziaji  uanze, inasaidia
kufanya matumizi sahihi  ya  dawa, 
hatimaye faida/pato litakuwa kubwa kwa mkulima. 
Inashauriwa kwamba upuliziaji ufanyike asubuhi na mapema,
wakati ambapo kuna umande. Asubuhi, upepo nao 
huwa  hauna nguvu sana na
inashauriwa upuliziajiusizidi ya saa 3 asubuhi. Umande unasaidia salfa ya unga iweze
kunata kwenye majani na maua. Ila kwa salfa ya maji kama thiovit unaweza
kupulizia wakati wowote.vipindi vifuatavyo, vimependekezwa katika upuliziaji:Siku
14      14     
14       21     21 
Dawa zingine badala
ya salfa. 
Madawa kadha wa kadha yamefanyiwa  utafiti sambamba na salfa. Aina tatu za dawa
hizo   (waterbased  organics), zimependekezwa kwa matumizi ya wakulima,
nazo ni Bayfidan, Anvil na Topas.  Kiwango
cha upuliziaji ni ml 10 - 15 za dawa ndani ya0.75  - 
1.25  za  maji kutegemeana na ukubwa wa mti. Vipindi
kati ya mipulizo ni wiki tatu (siku 
21)  na awamu (raundi) 3 zinatosha
kwa msimu. Inashauriwa kwamba kutokana na gharama za dawa yamaji, zinafaa
zitumike kwenye mikorosho ambayomkulima ana uhakika wa kutoa zaidi ya kilo 4
baada ya kupulizia.  Miti inayotoa chini
ya kiasi hicho heri isipuliziwe, vinginevyo italeta hasara




2 comments:
Nimefurahi sana kusoma utaalamu huu katika blogger. nataka kuuliza katika heka moja ni miche mingapi ya mahindi inastahili kuwepo ili kutoa matokeo mazuri kujua kila heka utapata gunia ngapi?. vivyo hivyo kwa ufuta na halizeti ukizingatia kupanda kwa mistari?. mlangwaa@yahoo.com
Nataka kujua kuhusu nikitaka kuanzisha ugugaji wa samaki vitu gani vya muhimu vya kuanza navyo
Post a Comment