KURASA

Friday, July 20, 2012

KUKU WA KIENYEJI WANAUZWA


Kuku wa kienyeji wenye uzito kati ya kilo moja na nusu na kuendelea wanauzwa bei ni kuanzia shilingi elfu kumi mpaka elfu kumi na tano tu (10,000 - 15,000) kutegemeana na ukubwa wa kuku mwenyewe kuku wanapatikama wengi kama 200, 


Pia mayai ya kuku wa kienyeji yapo , kwa trei moja ni shilingi elfu kumi tu (10, 000)kwa maulizio piga namba 0755-462970 ulizia Livin Matabaro

Tuesday, July 3, 2012

SUMA JKT NA SABA SABA

 FARMTRAC trekta bora kwa ajili ya kilimo cha kisasa






Kuku wazazi (parent stock) kwa ajili ya kuzalisha vifaranga vya kuku bora wa mayai na wa kienyeji (improved breed)



Battery cages kwa ajili ya kufugia kuku wa mayai, mfumo huu hutumia sehemu ndogo tu ya banda kufuga kuku wengi, na ni rahisi kwa sababu mifumo ya maji na chakula unaweza kuweka inayojiendesha yenyewe (automatic) na pia ni rahisi kukusanya mayai na haya vunjiki hovyo


 Hawa ni bata wa kawaida


 Bata mzinga
F

SABA SABA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

  Hii ni sehemu ya kwanza mara baada ya kuingi akwenye banda hili ambapo utakutana na sanamu kadhaa za wanyama wa mbugani













 Hii ni sehemu ya nyuma kwenye wakala wa mbegu za miti, hii ni baadhi ya miche inayopatikana kwenye vitalu vyao



Huu mti unaitwa msabuni au mhalinta





Mzinga wa nyuki wa kufugwa, huu ni mzinga wa kisasa kabisa







Mdau akinunua mbegu za miti ya misoji (mitiki) kutoka kwa wakala wa mbegu za miti (TTSA) kwa ajili ya kuotesha mwenyewe


PAN 4M-19 MBEGU BORA YA MAHINDI





aka MKOMBOZI mbegu bora kutoka kampuni ya mbegu ya PANNAR, mbegu hii ya chotara inafaa sana kwenye maeneo mbali mbali ya ukanda wa chini na kati wenye mvua kidogo na inavumilia sana ukame. mbegu hii ndiyo mkombozi wauhakika na itakufanya uepukana na njaa haswa katika kipindi hiki ambacho hali ya hewa haitabiriki





  • Punje zake ni ngumu za zinakoboleka vizuri, haishambuliwi na wadudu kwa urahisi na inauwezo wa kutoa magunia 25 kwa ekari moja
  • Inafaa kwenye maeneo mengi yenye hali mbaya ya hewa hasa ukame
  • Inavumilia sana magonjwa ya majani kama maize strips
  • Ni matamu sana kwa kuchoma
  • Inakomaa mapema sana siku 90 - 100 tangu kupanda
  • Inauwezo wa kutoa mahindi mawili mawili


Kwa wanaokwenda saba saba watembelee nyuma ya banda la PTA kwenye bustani za jeshi la magereza
na kwa mawakala wa jumla wasiliana nao kwa mawasiliano haya
P.O.BOX 10677 Arusha Tanzania
Tel +255 (0)27 250 4669
Fax +255 (0) 27 254 4669
info@pannar.co.tz
www.pannar.com

Wednesday, June 27, 2012

KILIMO BORA CHA MIPAPAI


MAHITAJI
Hali ya  hewa inayofaa kwa mipapai ni ya kitropik ambayo haina baridi kali na joto kiasi . Udongo usiotuamisha maji maji yakisimama kwa masaa 48 tu mpapai unaweza kufa, wenye ruruba ya kutosha kwa sababu mipapai haina mzizi mkuu haihiyaji udongo wenye kina kirefu, kipindi cha jua kali mpapai usiachwe zaidi ya wiki 8 bila kumwagiliwa maji kama hakuna mvua ingawa wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hii huongeza ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema sokoni

Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mwingi kwani huvunjika kirahisi, kama unashamba la mipapai itakubidi kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka shamba lako, miti kama miparachichi, migravilea, vibiriti (leucaena Spp) na miembe pia inafaa. Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai kwa mita 10 mpaka 20 juu zaidi

Kuendelea kupanda mipapai kwenye shamba moja kunaweza kusababisha usugu wa magonjwa, nashauri baada ya miaka 3 – 5 ubadilishe zao hili angalau kwa msimu mmoja ili kuua mzunguko wa magonjwa
Mipapai inaweza kuchanganganywa na miembe na mimea jamii ya michungwa, pia mazao ya msimu kama mahindi, mtama, ufuta , alizeti  na  mboga mboga yanaweza kulimwa

Kwa kaida kwenye mipapai kuna mipapai dume, majike  na yenye jinsia zote (multiplesex/hermaphrodite) ambayo huwa na mapapai marefu zaidi, na pia kuna isiyoeleweka ambayo huwa na mapapai mafupi sana

MBEGU
Kusanya mbegu toka kwenye mapai makubwa na yaliyo komaa na kuiva, kausha mbegu vizuri kbla ya kupanda, kama utapata mbegu za  kununua ni vizuri zaidi, baada ya kukausha hakikisha unazipanda ndani ya wiki moja

KUOTESHA MBEGU
Kuna wanaopendelea kuotesha mbegu kwanza na kisha kuhamishia miche shambani, sehemu ya kuoteshea iandaliwe miezi miwili kabla, mbegu zioteshwe kwenye kina kati ya sentimeta 1 – 2 chini ya udongo wenye rutuba au pakiti za plastiki, kiwango bora cha joto ni sentigredi 21 – 27 na itachukua kati ya wiki 1 – 4 kwa mbegu kuota, kwenye kila pakiti weka mbegu 2 – 3. Panda mbegu zako kwenye kitalu kwa umbali wa sentimeta 3 toka shimo hadi shimo na sentimeta 15 kati ya mistari, hakikisha maji hayatuami kabisa, pia unaweza kupiga dawa ya copper oxychloride gramu moja katika lita moja ya maji ilikukinga miche yako na fangasi

UOTESHAJI WA MOJA KWA MOJA
Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea ya kuku sehemu ya kupandia, mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia kukinga mipapai na magonjwa. Panda mbegu 3 – 5 kila shimo maana miche mingine inaweza kufa kwa magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota dume

KUHAMISHA MICHE TOKA KWENYE KITALU
Miche ihamishiwe shambani ikiwa na urefu wa sentimeta 20 – 40, kama udongo unatuamisha maji panda kwenye matuta yenye urefu wa sentimeta 40 – 60 mashimo yawe na ukubwa wa sentimeta 45 upana na sentimeta 30 kina na shimo lichanganywe na udongo na samadi bila kuacha kisahani cha maji, umbali ni mita 3 kwa 3 kwani mipapai inahitaji jua la kutosha

KUPUNGUZA MIPAPAI
Baada ya miezi 3 – 5 baada ya kupanda mipapai itatoa maua na hapo jinsia ya mipapai itajulikana na mingine itabidi ipunguzwe na hasa midume, mipapai yenye jinsi zote inatakiwa isizidi asilimia 10 – 20 na midume ibaki mmoja katika kila mijike 25, mimea yenye magonjwa pia inabidi ing’olewe

RUTUBA YA UDONGO
Weka kiasi chakilo 2 – 5 za samadi kwenye kila mpapai kwa mwaka ili kuongeza ukuaji na uzazi, mabaki ya mimea yanaweza pia kuwekwa kama matandazo na h ii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu usipotee.

MAGUGU
Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili kuzuia uoataji wa magugu, magugu yang’olewe yakiwa machanga na epuka kuchimbua chini sana maana mizizi ya mipapai huwa juu juu, njia nzuri ni kuweka matandazo kwenye shamba lote ili kuzuia outaji wa magugu

UANGALIZI
  • Mipapai iangaliwe dhidi ya magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au kufukiwa chini ikiwa itabainika kuwa na maonjwa, piga dawa dhidi ya magonjwa ya fangasi na virusi mara yanapoibuka ili kuongeza uzaaji nakipato chako
  • Ondoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na hii ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.
  • Ondoa mapapi yote ambayo yatakuwa hayakuchavuliwa vizuri na acha yale yenye afya tu
  • Weka miti ya kuegemea kama mpapai utazaa matunda mengi na hasa wakati wa upepo mwingi ili kuzuia mipapai isivunjike
  • Mipapai ikitunzwa inaweza kuishi mika mingi, ila kwa ajili ya mazao bora ondoa mipapai na upande mingine baada ya kila miaka mitatu (3) kwani mpapai unapo kuwa mkubwa basi rutuba yote huishia kwenye mti wenyewe

Tuesday, June 19, 2012

UTITIRI - WADUDU WASUMBUFU WA MIKOROSHO


Utitiri wa mikorosho  au kwa jina lingine thrips (Thrips rubrocinctus), ni wadudu wadogo sana wenye mwili laini na rangi  kati  ya njano, kahawia au nyeusi. Utitiri  wakubwa  (adults) hutambulika kwa kuwa na mabawa na mwili wa kahawia (dark brown) au  mweusi,  pamoja  na upito  (band) wa rangi nyekundu kifuani. Wanaonekana vizuri kwa kutumia kikuzia umbo (lens).
Katika kipindi kirefu, utitiri ulikuwa ukionekana katika  maeneo mengi yanayolimwa korosho, lakini athari zake zilikuwa ndogo. Katika miaka ya hivi karibuni wameonekana kwa uwingi na kuleta hasara kubwa hasa katika  tarafa  za Lisekese na Chikundi wilayani Masasi.  Pia mashambulizi  ya wadudu hawa yameonekana katika wilaya za Nachingwea na Newala  kwa kiwango kidogo. Inakisiwa kuwa uongezekaji wa  wadudu  hawa husababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

MZUNGUKO WA MAISHA
Utitiri wakubwa hutaga mayai katika sehemu yachini  ya majani. Mayai yanaanguliwa baada ya siku 3 hadi 4 na  kutoa  vijititiri  vidogo  sana (larva I) ambavyo huwa ni  vyepesi  sana. Huingia  hatua  ya pili (larva stage II) baada ya siku 7 hadi 8.  Hatua hizi ndizo  ziletazo uharibifu mkubwa maana ndizo hatua za ulaji na ulafi  wa  hali ya juu. Baada ya wiki moja tena, ndipo hutokeza hatua ya kwanza ya “ninfu” (Nymph stage I) na hatua yake ya pili baada ya siku 3 hadi 4. Katika hatua hizi mbili (nymph stages), vijidudu hivi havitembei  wala  kula chakula bali hukaa mahali pamoja, hasa kwenye ardhi. Hatua hii ya “ninfu” hudumu kwa siku 11 hadi 12 kabla ya kupevuka na kuwa utitiri wakubwa (adults). Hivyo Mzunguko wa maisha yao toka yai hadi kupevuka ni mwezi mmoja. Utitiri hushamiri sana wakati wa  kiangazi mara tu  baada  ya mvua,  hasa kati ya mwezi June na Oktoba. Utitiri hupungua kabisa wakati wa mvua, hata hivyo huvuka msimu hadi mwingine kama utitiri wakubwa.

MASHAMBULIZI
Utitili wachanga pamoja na  wakubwa, hushambulia upande wa chini wa majani hasa yaliyokomaa, machipukizi na mashada ya maua. Utitili wachanga hubeba tone la majimaji mkiani na kudondoshea juu ya majani,  ambapo likikauka huacha doa la kahawia  au  nyeusi, lakini hasa rangi ya kutu. Maeneo yaliyoshambuliwa na  utitili  hubadilika rangi na kuwa na weupe weupe wenye mng’aro wa rangi ya fedha (silvery).  Baadaye hubadilika na kuwa na rangi ya udongo (kahawia), hatimaye hukauka na majani hupukutika Eneo  linaloshambuliwa hudumaa na uzalishaji  kuathirika. Maeneo mengi ambayo hushambuliwa na utitili huwa  korosho  hazizai kabisa. Miti iliyopukutisha majani kwa sababu yamashambulizi  ya utitiri, huweza kuchipuza tena kwenye mwezi Novemba na Desemba.

MAZAO MENGINE YANAYOSHAMBULIWA NA UTITIRI
Wadudu hawa hushambulia majani na hata maua ya aina  mbalimbali ya mazao na mimea, kama vile  mazao ya bustani (vitunguu nk), michungwa, pamba, aina ya nafaka. Kwa sababu ya wingi wa aina ya mimea inayoshambuliwa na utitiri,  udhibiti  wa wadudu hao unaweza kuwa mgumu kwa kiasi fulani.

KUSHAMIRI KWA UTITIRI
Wadudu hawa hupendelea mikorosho iliyosongamana,  isiyopitisha hewa vizuri, mikorosho  isiyopogolewa na mashamba yasiyohudumiwa kwa ujumla.  Hupendelea hasa miti mikubwa. Utitiri hupendelea hali ya ukame au kiangazi cha muda mrefu.

KUSAMBAA
Utitiri husambazwa hasa kwa njia ya upepo  au kwa kupanda vipando  (propagation  materials) ambavyo vimeshambuliwa.

KUDHIBITI KWENYE MIKOROSHO

Njia  pekee  inayotumika kudhibiti utitiri ni matumizi ya madawa. Dawa ya BASUDIN au KARATE ndiyo iliyopendekezwa  na watafiti kudhibiti utitiri wa korosho. Mchanganyiko wa mililita  5  za KARATE na lita moja ya maji  unatosha kudhibiti  wadudu hawa katika mti mkubwa usiozidi kipenyo (diameter) cha mita 10. Ni jambo la muhimu kukagua mashambulizi kuanzia mwezi Mei. Upuliziaji unaanza mara tu baada ya kuona dalili za  mashambulizi  au kuwaona wadudu wenyewe na kurudia baada yawiki tatu (siku 21).  Upuliziaji  unafanyika kutumia mashine ya moto (Mist blower) au yakawaida (Knapsack sprayer)  kutegemeana  na ukubwa wa mti. Ni muhimu kuanza kupuliza dawa mapema, ili kuweza kuwathibiti wadudu hawa wakiwa katika hatua zao za mwanzo kabisa za ukuaji wao ( hatua za lava na ninfu). Hii ni  muhimu kwa sababu ni vigumu kuudhibiti utitiri  wakubwa. Awamu 2 hadi 3 zinatosha kuthibiti wadudu hawa katika msimu mmoja. Ikibidi,  matunda (mabibo) yaliyopuliziwa dawa yasitumike mpaka baada ya siku 21

UBWIRI UNGA - UGONJWA MKUU WA MIKOROSHO


Moja ya matatizo makubwa ya uzalishaji wa  zao  la korosho ni ugonjwa wa Ubwiri unga.Ugonjwa huu unasababishwa  na vimelea aina ya uyoga (fungus) viitwavyo Oidium anacardii. Ugonjwa huu ni muhimu sana, kiasi kwamba kama haukuthibitiwa,  unaweza kupunguza mavuno kwa zaidi ya asilimia 70.       Ugonjwa huu umeenea katika  mikoa  yote inayolima zao hili Tanzania.  Hapo awali ugonjwa huu ulikuwa unaitwa kwa jina la“ukungu” kutokana na uhusiano wake mkubwa na haliya hewa ya ukungu  (litabwe  kwa  Kimakonde) unaoonekana  alfajiri/asubuhi katika miezi ya Juni - Septemba.  Hivyo  basi,  jina la Ubwiri unga linatumika sasa ili kuwawezesha wakulima wasichanganye vitu hivyo viwili.

MASHAMBULIZI
Ugonjwa huu unashambulia maeneo yote machanga na teketeke  katika  mti wa mkorosho, hasa machipukizi, majani, maua, mabibo na korosho changa (tegu). Athari kubwa  ya ugonjwa  huu inatokana na mashambulizi ya maua, ambayo hushindwa kufunguka  na  kuwezesha chavua kufanya kazi yake,  hatimaye  hunyauka  na kukauka.

DALILI
Maeneo yaliyoshambuliwa na ugonjwa huu, hufunikwa na unga unga mweupe au wakijivujivu  ambao huonekana kama vumbi vumbi. Vimelea au chembe chembe zinazoshambulia ni ndogo ndogo sana na hazionekani dhahiri kwa macho, ila kwa darubini. Chembe chembe hizi zinapozaliana kwa wingi katika maeneo ya mshambulizi, ndipo huonekana kama unga unga mweupe/kijivu. 

KWENYE MAJANI
Pamoja na kufunikwa na unga unga,  majani yaliyoshambuliwa husinyaa, hubadilika rangi, wakati mwingine hukunjamana. Majani machanga zaidi yanaweza kupukutika, ambapo yale yaliyokomaa hayashambuliwi. Masalia ya mashambulizi  kwenye majani yaliyokomaa, huonekana kama mabaka ya kahawia, hata hivyo hayapukutiki.

KWENYE MAUA
Maua yanaweza kushambuliwa hata kabla ya kuchanua. Pamoja  na  kufunikwa na unga unga weupe/kijivu, maua yaliyoshambuliwa sana hushindwa  kuchanua  na hatimaye hukauka kabisa na kuwa kama “majani yachai”. Hili ndilo sababisho kubwa la upungufu wa zao la korosho.

KWENYE MABIBO

Mabibo yaliyoshambuliwa huonyesha  unyafuzi,hupasuka pasuka na ngozi yake huonekana kuwa chafu. Hatimaye,  mabibo  hayo huwa madogo kwa umbo, yenye  maji kidogo  sana, hivyo kuyafanya maji yake kuwa matamu sana.
KWENYE TEGU NA KOROSHO
Tegu  zilizoshambuliwa  huweza kubadilika rangi yake ya kijani/nyekundu na kuwa ya hudhurungi au bluu iliyo mzito. Tegu zikishambuliwa zingali changa sana, huweza kupukutika. Tegu zilizoshambuliwa zikifikia kukomaa, zinaonyesha uharibifu mkubwa wa ngozi yake na huonekana chafu, hatimaye, wakati wa mauzo hutengwa katika  daraja  lachini (grade II).

KUSTAWI KWA UBWIRI UNGA
Vimelea vya Ubwiri unga vinaishi kwenye mimea iliyo hai tu, haijawahi kuoteshwa katika  maabara.  Ugonjwa huu hushamiri na kustawi vizuri katika  majira  yenye ukungu, hasa  kuanzia mwezi Mei/Juni hadi Septemba karibu kila mwaka. Mazingira mwafaka kwa ugonjwa huu ni:
• Joto: 26 - 28 0C (bora 25 C)
• Unyevu (RH): 80-100% (bora 95%)

Ubwiri unga pia hupendelea  zaidi mikorosho iliyosongamana na isiyopitisha hewa vizuri. Ugonjwa huu hupendelea mazingira ya kiangazi, hasa  kuanzia mwezi Juni hadi Septemba, haupendelei hali ya mvua na  joto jingi.  Hivyo basi, katika miezi mingine (hasa wakati wa masika), vimelea hujificha na kuishi Kwenye maotea  au machipukizi uvunguni  mwa mikorosho au kwenye maua yasiyo ya msimu. Hivi ndivyo  vyanzo vya Ubwiri unga, vyenye uwezo wa kuhifadhi ugonjwa msimu hadi mwingine. Ugonjwa huu husambazwa kwa upepo ambao nao  pia hushamiri sana katika miezi ya Mei/Juni hadi Septemba.

KUDHIBITI
Zipo njia aina tatu zinazotumika kuthibiti Ubwiri unga, nazo ni mbinu za asili, mbegu bora na madawa.

MBINU ZA ASILI (Cultural control)

Kuondoa vyanzo vya Ubwiri unga (sanitation).
Hii ni kazi ya mikono ya kuondoa machipukizi na maotea yanayojificha kwenye uvungu  wa  mikorosho, kutumia vifaa kama vile upanga, mundu, shoka nk. Msingi wa kazi hii ni kupunguza kasi ya ugonjwa huu katika shamba kwa kuchelewesha mlipuko na  kasi ya mashambulizi. 

Kubadili mazingira ya ugonjwa katika miti.
Kupunguzia  matawi  (prunning) ya mikorosho ili kufanya  umbile  la  mwamvuli katika miti, ili kuruhusu joto na upepo kupenya kirahisi, inasaidia sana kuthibiti Ubwiri unga.
Kupunguza  miti (thinning) iliyosongamana na kuacha nafasi ya kutosha kati  ya miti, itasaidia kupunguza kuenea kwa ugonjwa.  Miti ikiwa  katikanafasi  ya kutosha, itawezesha hewa  kupenya  vizuri na kubadili mazingira ili yasiwe mazuri kwa kustawi kwa ugonjwa.

Kupanda mikorosho inayovumilia/kuhimili ugonjwa.
Ipo baadhi ya mikorosho  ambayo  inaweza  kuhimili mashambulizi ya ugonjwa hata kuweza  kutoa  Mazao bila ya kutumia kinga yoyote.  Aina zingine zinaweza kutoa maua na kuzaa kabla  ya  athari za ugonjwa hata kuweza kukwepa mashambulizi.  Hii  ni  baadhi  ya mikorosho  bora  ambayo hatimaye imepandwa katika eneo moja katika vituo  vyetu vyote vya kuendeleza korosho (Cashewnut Development Centre )kama NALIENDELE. Mbegu zinazopatikana toka mashamba hayo ni mbegu bora (polyclonal seed) ambazo zinaweza kuzaa bila madawa, lakini huzaa vizuri zaidi kama mtu atatumia dawa pia.


MATUMIZI YA MADAWA

Dawa ya Salfa (Sulphur)
Salfa ndiyo dawa inayotumika kwa wingi zaidi kukinga ugonjwa wa Ubwiri unga. Dawa hii ambayo ni ya unga, inapulizwa kwa kutumia mashine maalumu (motorised blower)  ya kupulizia dawa k.m. Maruyamana Solo. Kiwango cha  gramu  250 kwa mti, kwa mzunguko, ndicho kinapendekezwa.  Hivyo basi kwa mizunguko mitano kiasi cha kilo 1.25  cha  salfa kwa mti kwa mwaka kinahitajika.  Pia kuna salfa za maji kama Thiovit ambazo unaweza kupulizia kwa kutumia vinyunyuzia dawa vya kawaida (knapsack sprayer)

Wakati wa kuanza kupulizia sailfa
Mpulizo wa kwanza unaanza ambapo karibu asilimia 20za maua yamejitokeza na wakati sawa, zaidi ya asilimia 5 ya maua hayo tayari yawe  yanaonyesha dalili  za ugonjwa. Upimaji wa maua ili kujua  lini  upuliziaji  uanze, inasaidia kufanya matumizi sahihi  ya  dawa,  hatimaye faida/pato litakuwa kubwa kwa mkulima.
Inashauriwa kwamba upuliziaji ufanyike asubuhi na mapema, wakati ambapo kuna umande. Asubuhi, upepo nao  huwa  hauna nguvu sana na inashauriwa upuliziajiusizidi ya saa 3 asubuhi. Umande unasaidia salfa ya unga iweze kunata kwenye majani na maua. Ila kwa salfa ya maji kama thiovit unaweza kupulizia wakati wowote.vipindi vifuatavyo, vimependekezwa katika upuliziaji:Siku 14      14      14       21     21 

Dawa zingine badala ya salfa.
Madawa kadha wa kadha yamefanyiwa  utafiti sambamba na salfa. Aina tatu za dawa hizo   (waterbased  organics), zimependekezwa kwa matumizi ya wakulima, nazo ni Bayfidan, Anvil na Topas.  Kiwango cha upuliziaji ni ml 10 - 15 za dawa ndani ya0.75  -  1.25  za  maji kutegemeana na ukubwa wa mti. Vipindi kati ya mipulizo ni wiki tatu (siku  21)  na awamu (raundi) 3 zinatosha kwa msimu. Inashauriwa kwamba kutokana na gharama za dawa yamaji, zinafaa zitumike kwenye mikorosho ambayomkulima ana uhakika wa kutoa zaidi ya kilo 4 baada ya kupulizia.  Miti inayotoa chini ya kiasi hicho heri isipuliziwe, vinginevyo italeta hasara

KIFA UWONGO - MDUDU HATARI KWA MIKOROSHO


Kifa-uwongo (Mecocorynus loripes),. ni mdudu aina ya “weevil” ambaye hushambulia mashina ya mikorosho hata kufikia hatua ya kuuwa mti mzima. Mdudu huyu huitwa “kifa-uwongo” kwa sababu ya mbinu yake makini anayotumia kujihami. Mara tu aonapo mtu anapita karibu yake, huanguka chini na kujifanya kama amekufa kabisa. Kisha baada ya mtu yule kupita, yeye huamka tena na kuendelea na shughuli zake kama kawaida. Wamakonde humwita mdudu huyu “Nang’ang’ana”, ambapo Wayao nao humwita “Ng’ang’ani.

MAISHA YA KIFA UWONGO
“Kifa-uwongo” kama wadudu wengine, hupitia hatua za yai, “lava” na “buu” kabla ya kuwa mdudu kamili. “Kifa uwongo” kamili aliyekomaa, ana rangi ya kahawia na urefu wa kama sentimita 2. Ana mdomo mrefu uliochongoka (snout) ambao daima anauficha kwa kuulaza kifuani pake. “Lava” wake ni aina ya funza (grab) mweupe, mwenye ngozi ya kukunjamana na kichwa cha rangi ya kahawia mzito (dark brown), yeye  daima huonekana amejikunja kama upinde.

“Kifa uwongo” wa kike hutoboa gamba la mkorosho kwa kutumia mdomo wake mkali, na kutaga yai moja moja. Baada ya mayai kuanguliwa, mafunza huanza kushambulia gamba la mti mara moja. Funza hawa wana midomo mikali kama misumeno, nao wanakula kwa bidii sana gamba la mti. Kadri wanavyokula ndivyo wanavyoongezeka ukubwa pia. Funza akaribiapo kuwa Buu (pupa), hupekecha ndani ya mti (kiasi cha sentimita 2.5 chini ya gamba) na kutengeneza matundu kwa ajili ya maficho ya buu (pupal chambers). Mabuu hujifungia ndani ya matundu hayo na hatimaye hugeuka na kuwa “Kifa uwongo” kamili. Mzunguko wa kutokea yai hadi “Kifa-uwongo” kamili, huchukuwa muda wa miezi sita, ambapo muda wa karibu miezi 2 - 2.5 huwa katika hatua ya mafunza, ambayo ndiyo yenye uharibifu mkubwa. “Kifa-uwongo” kamili ana mabawa na anaweza kuruka kwa nadra toka mti hadi mwingine. Mara nyingi wadudu hawa, huonekana wakidumu katika maeneo ya mashambulizi.  Mashambulizi yanaweza kuchukua muda wa mwaka au miwili katika mti mmoja, ambapo mti wa jirani unaweza kuwa huru kabisa bila mashambulizi!.  Mara nyingi “Kifa-uwongo” hupenda kuhamia mkorosho mwingine baada ya kuua kabisa mkorosho waliouanza kushambulia.

DALILI ZA MASHAMBULIZI
Maeneo ya mashambulizi huonekana wazi wazi hata toka mbali, kwa sababu ya uwepo wa Mchanganyiko wa utomvu na takataka kama za maranda ya seremala ambayo hatimaye hugeuka rangi na kuwa nyeusi.   Rangi ya majani ya mkorosho ulioshambuliwa sana, hubadilika na kuwa njano, kisha hunyauka na hatimaye hukauka. “Kifa-uwongo” hupendelea kushambulia miti mikubwa tu. Utafiti umeonyesha pia kwamba hupendelea miti iliyojeruhiwa kutokana na kukatwa kwa ajili ya ubebeshaji  (top-work) au hata ile ya kupunguzwa matawi. Inasadikika kwamba aidha eneo la jeraha ni rahisi kwa kifa uwongo kutaga mayai yake, au huenda kuna mvuto wa aina yake kutokana na harufu ya utomvu utokao eneo lenye jeraha na kufanya mvuto wa pekee kwa kifa uwongo kushambulia!

MKOROSHO ULIOSHAMBULIWA NA KIFA-UWONGO

JINSI YA KUDHIBITI KIFA UWONGO
Hakuna dawa ambayo inashauriwa kutumika katika kuthibiti wadudu hawa, badala  yake, mkulima mwenyewe anashauriwa kupambana nao ana kwa ana: Mwanzoni mwa mashambulizi. Ukaguzi wa mara kwa mara ufanyike kwa kila mkorosho kukagua mashambulizi hayo. Mara tu baada ya kuona  dalili  za mashambulizi ya wadudu hawa, bandua eneo la mashambulizi kwa kutumia kisu  au upanga na kuwaondoa mafunza wote. Funza akidondoka chini hana uwezo tena  wa kupanda kwenye mti au kufanya mashambulizi. Mabuu waliojifungia kwenye matundu  ya maficho  yao, wanaweza kuuawa kwa kutumia  ncha  kali, kama vile spoku yabaiskeli, ili kuwatoboa wakiwa  ndani  yamashimo yao.  Inashauriwa pia kuwasaka na kuwaua  kila “Kifa  uwongo” kamili (adults) kwa kuwakata vichwa vyao.

MASHAMBULIZI YALIYOKITHIRI
Inashauriwa  kukata na kuchoma moto mikorosho yote iliyoshambuliwa kwa kiwango  cha  hali ya juu, ili kuuwa mabaki ya mayai na funza waliopo

MILIBAGI - MDUDU MHARIBIFU WA MIKOROSHO


UTANGULIZI
Milibagi (Pseudococcus longispinus) ni wadudu waharibifu katika zao la korosho, waliojitokeza kuwa maarufu sana katika miaka ya tisini. Hawa ni wadudu wanaoonekana katika maeneo mengi ulimwenguni, lakini hushamiri na kuleta athari kubwa katika mazingira ya Tropikali. Mnamo mwaka 1990, milibagi walionekana kushambulia mikorosho katika maeneo ya mjini Masasi. Mwaka 1993, walionekana kuenea hadi wilaya za Nachingwea na Tunduru. Hivi leo, wadudu hawa wameenea karibu sehemu nyingi za kanda ya kusini, ingawa mashambulizi makubwa yapo wilayani Masasi, Tunduru, Nachingwea na Liwale.   Milibagi ni moja ya wadudu waharibifu wanaoishi na kuponea mimea. Wadudu hawa hutengeneza utando mweupe (scale) juu ya miili yao kwa ajili ya kinga na kujihami dhidi ya adui zao.

Milibagi huonekana katika mazao ya aina nyingi ikiwa ni pamoja na miembemafuta, mihogo, michungwa, minanasi nk. Pamoja na hivyo, kuna tofauti kati ya milibagi wanaoshambulia hayo mazao mbalimbali. Kwa mfano, milibagi wa mihogo (Phenacoccus manihoti), miembe (Rastrococcus invadens) ni tofauti na wale wa mikoroshoni (P. longispinus). Dalili za Mashambulizi ya Milibagi. Maeneo yaliyoshambuliwa na milibagi huonekana yamefunikwa na weupe weupe ambao ni utando unaofunika miili ya wadudu hao. Mikorosho iliyoshambuliwa sana na milibagi, huonekana kwa mbali kama vile imefukikwa na theluji. Mashambulizi ya Milibagi Milibagi wanaweza kushambulia eneo lolote la mmea kwa njia ya kufyonza. Kwa jinsi hiyo, milibagi huingiza matemate yao  katika maeneo ya mashambulizi na hatimaye huweza kueneza vimelea vya virusi. Milibagi hutoa utomvu mweupe mweupe kama asali na kufunika maeneo ya mashambulizi, hata kufanya mmea usiweze kupata mwanga wa jua vizuri hata kuzuia utengenezaji wa chakula cha mimea (photosynthesis).  Majani yaliyoshambuliwa sana na milibagi, hupukutika hivyo kuathiri uzalishaji. Maua yaliyoshambuliwa mapema na milibagi yanashindwa kuzaa. Korosho zilizoshambuliwa zingali zinakomaa, zinachafuliwa kwa utando na utomvu. 

Korosho hizo yamkini zisafishwe kwa mchanga kabla ya kufikiria kuuzwa, vinginevyo hutengwa katika daraja la pili. Mashambulizi ya milibagi, yanaweza kupunguza uzalishaji kwa kiwango cha asilimia 50% Kustawi kwa Milibagi. Milibagi huonekana kwa wingi wakati wa kiangazi, hasa mwezi Septemba hadi Novemba. Milibagi hupungua sana wakati wa mvua. Inaelekea kwamba mabadiliko ya hali ya hewa ni chanzo kikubwa cha mashambulizi ya milibagi kwenye mimea. Maisha ya Milibagi. Milibagi wa kike hutaga kiasi cha mayai 50-500 kutegemeana na mazingira. Mayai huanguliwa na kutokea Vitambaazi (crawler). Hatua hii ni muhimu kwa usambaaji wa milibagi. Hawa hutambaa mpaka kwenye ncha au vilele vya miti na kujitegeshea miguu yao ili wasambazwe kwa upepo, ndege au wadudu wengine. Binadamu pia wanahusika sana kusambaza wadudu hawa katika hatua hii. Hatua za lava zinazofuata ndizo za ulaji na uharibifu. Milibagi waliokomaa (adults) huwa hawajishughulishi (inactive), huwa hawali chakula na huishi muda mfupi (wiki au mwezi)

KUDHIBITI
Zipo  njia mbili ambazo zinaweza kutumika kudhibiti milibagi:
‰ 
NJIA YA KIBAIOLOJIA
Utafiti umeonesha kwamba  wapo wadudu  wengine ambao wanaweza kushambulia milibagi, kama vile:
 a) Ladibedi bito (Chilocorus spp)
b) Manyigu (Chrysopa spp)

Utafiti umeonesha kwamba idadi ya wadudu hawa mashambani ni ndogo kwa kuweza kudhibiti idadi kubwa ya milibagi. Utafiti wa kina zaidi unafanyika kuona jinsi ya kuwafanya wadudu  hawa waongezeke idadi ili kuweza kuwadhibiti milibagi mikoroshoni.

◊ NJIA YA KUTUMIA MADAWA
Njia pekee inayotumika hivi sasa kuwadhibiti milibagi ni kutumia madawa. Dawa aina ya Selecron 720 EC  ndiyoiliyothibitishwa na utafiti itumike dhidi ya milibagi.

Dawa ya Selecron 720 EC Dawa hii ni ya aina ya maji, inayosambazwa  na kampuni ya Norvatis (Ciba Geigy). Inapulizwa kwa  kutumia mashine za moto  (motorized  blowers) kama vile Maruyama 150DX au Solo
◊ Kiwango cha upuliziaji  ni  mililita  7.1 ya dawa, ndani ya lita 1 ya maji kwa mti mkubwa.
◊ Upuliziaji unaanza mara tu  baada  yakuona  dalili  za mashambulizi yamilibagi. 
◊ Marejeo  ya upuliziaji yafanyike kila baada ya siku 7 – 14 kutegemeana na hali ya mashambulizi yalivyo.

Thursday, May 17, 2012

MBOLEA VUNDE


1. Namna ya kutayarisha Mboji/Mbolea Vunde/Mbolea Hai
Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama (matamahuruku)) ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo. Sehemu za vitu kama majani, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Matokeo ya kusazwa huku ni tofauti kabisa na zile sehemu zilizowekwa. Mboji iliyoiva hubadilika rangi na kuwa ya hudhurungi, tifutifu na hunukia vizuri.
Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama zake ni za chini sana na inafaa mno kuongezwa kwenye udongo ili kuinua mazao ya shamba.
Vipande vya vitu au sehemu ya viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au shambani bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji lakini itachukua muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba yake kupotea. Lakini kama muda ukitengwa ili kushugulikia mbolea matokeo yatakuwa mazuri na ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na jikoni yanatumika katika kutengenezea mboji.
Mboji iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa shambani. Mboji huchemka hata kiasi cha kuua magonjwa ya mimea na mbegu za magugu.
Majani makavu ya ndizi ni mazuri kwa kutunza vifaa vya mbolea na kuweka ukavu. Hali hii huwa huzuia kupotea kwa maji kabla ya kujenga lundo la mboji na wakati mbolea inapokuwa inaiva.


1.1 Vifaa visivyofaa kuwekwa kwenye mboji
 Sehemu za mimea ambazo zimenyunyiziwa dawa ya kuwaua wadudu (viuatilifu) na kwekwe juzijuzi (Pesticide/herbicides).  Vipande vya nyama kwa sababu vinavutia panya na wadudu wengine. Sehemu nyingi za Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama (matamahuruku)) ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo. Sehemu za vitu kama majani, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Matokeo ya kusazwa huku ni tofauti kabisa na zile sehemu zilizowekwa. Mboji iliyoiva hubadilika rangi na kuwa ya hudhurungi, tifutifu na hunukia vizuri. Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea , Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama zake ni za chini sana na inafaa mno kuongezwa kwenye udongo ili kuinua mazao ya shamba. Vipande vya vitu au sehemu ya viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au shambani bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji lakini itachukua muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba yake kupotea. Lakini kama muda ukitengwa ili kushugulikia mbolea matokeo yatakuwa mazuri na ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na jikoni yanatumika katika kutengenezea mboji.  Mboji iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa shambani. Mboji huchemka hata kiasi mimea na majani ambazo ziliambukizwa ugonjwa.  Vifaa vilivyo na ncha kali kama mwiba ambavyo vyaweza kujeruhi mikono na miguu. Magugu ambayo yanarudiarudia kila mwaka. Magugu kama hayo huuliwa kwa kuanikwa kwenye jua kali ili yakauke baadaye huchomwa ili yasienee na jivu lake huongezwa kwenye biwi, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Matokeo ya kusazwa huku ni tofauti kabisa na zile sehemu zilizowekwa. Mboji iliyoiva hubadilika rangi na kuwa ya hudhurungi, tifutifu na hunukia vizuri.

Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama zake ni za chini sana na inafaa mno kuongezwa kwenye udongo ili kuinua mazao ya shamba.
Vipande vya vitu au sehemu ya viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au shambani bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji lakini itachukua muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba yake kupotea. Lakini kama muda ukitengwa ili kushugulikia mbolea matokeo yatakuwa mazuri na ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na jikoni yanatumika katika kutengenezea mboji.
Mboji iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa shambani. Mboji huchemka hata kiasi cha kuua magonjwa ya mimea na mbegu za magugu.
Majani makavu ya ndizi ni mazuri kwa kutunza vifaa vya mbolea na kuweka ukavu. Hali hii huwa huzuia kupotea kwa maji kabla ya kujenga lundo la mboji na wakati mbolea inapokuwa inaiva.


1.1 Vifaa visivyofaa kuwekwa kwenye mboji
 Sehemu za mimea ambazo zimenyunyiziwa dawa ya kuwaua wadudu (viuatilifu) na kwekwe juzijuzi (Pesticide/herbicides).  Vipande vya nyama kwa sababu vinavutia panya na wadudu wengine. Sehemu nyingi za Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama (matamahuruku)) ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo. Sehemu za vitu kama majani, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Matokeo ya kusazwa huku ni tofauti kabisa na zile sehemu zilizowekwa. Mboji iliyoiva hubadilika rangi na kuwa ya hudhurungi, tifutifu na hunukia vizuri. Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea , Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama zake ni za chini sana na inafaa mno kuongezwa kwenye udongo ili kuinua mazao ya shamba. Vipande vya vitu au sehemu ya viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au shambani bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji lakini itachukua muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba yake kupotea. Lakini kama muda ukitengwa ili kushugulikia mbolea matokeo yatakuwa mazuri na ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na jikoni yanatumika katika kutengenezea mboji.  Mboji iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa shambani. Mboji huchemka hata kiasi mimea na majani ambazo ziliambukizwa ugonjwa.  Vifaa vilivyo na ncha kali kama mwiba ambavyo vyaweza kujeruhi mikono na miguu.huwa vimejaa nyumbani au shambani bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji lakini itachukua muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba yake kupotea. Lakini kama muda ukitengwa ili kushugulikia mbolea matokeo yatakuwa mazuri na ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na jikoni yanatumika katika kutengenezea mboji.
 Mboji iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa shambani. Mboji huchemka hata kiasi mimea na majani ambazo ziliambukizwa ugonjwa.
 Vifaa vilivyo na ncha kali kama mwiba ambavyo vyaweza kujeruhi mikono na miguu.
 Magugu ambayo yanarudiarudia kila mwaka. Magugu kama hayo huuliwa kwa kuanikwa kwenye jua kali ili yakauke baadaye huchomwa ili yasienee na jivu lake laweza kuongezwa kwenye lundo la mbolea.
 Vitu visivyo kua na uhai kama plastiki na chuma. 


1.2 Mfano wa vitu vinavyoweza kutumiwa kutengenezea mboji nyumbani





2. Namna ya kutengeneza mboji ya mimea
Kusanya vitu na vifaa vinavyohitajika katika utengenezaji wa mboji ambayo ni;
 Majani mengi mabichi/kijani na makavu. Majani jamii ya mikunde ni mazuri sana kwani hutengeneza kirutubishi cha naitrojeni (N) kwa wingi.
 Mabua ya mahindi au vitawi vya miti
 Udongo wa kawaida wa juu
 Samadi, mbolea yoyote ya wanyama au mboji ya zamani
 Majivu au vumbi la mkaa
 Maji

2.1 Hatua
1) Chagua sehemu karibu na eneo ambalo mboji itaenda kutumika na ambapo kuna hifadhi ya kutosha kukinga dhidi ya upepo, jua na mvua.
2) Katakata majani yawe madogo madogo ili yaweze kuoza haraka. Tengeneza msingi kama mita sita (6) urefu na upana wake mita 2 kwa kutumia majani magumu kama matawi/vijiti. Hii itahakikisha maji yanatiririka na hewa ina zunguka vizuri. Hakikisha kuna nafasi ya kutosha kufanyia kazi kwenye biwi bila kulikanyaga.
3) Weka sentimita 10 ya majani ambayo hayaozi haraka kwa mfano mabua vya mahindi au mimea mibichi/kijani.
4) Weka sentimita 10 ya vifaa ambavyo huoza haraka kwa mfano maganda ya mboga na matunda.
5) Weka sentimita 2 ya samadi (mbolea-hai ya wanyama), mabaki ya mbolea ya zamani kama yaweza kupatikana.
6) Weka udongo wa juu sentimita 10 kutoka kwenye shamba ambalo hulimwa.
7) Majivu na mkojo vyaweza kunyunyuziwa juu ili kufanya biwi/lundo kuoza haraka. Kukatakata majani
8) Nyunyizia maji kwenye biwi mpaka lilowe.
9) Rudia mpangilio huu kuanzia namba nne (4) mpaka lundo lifike mita moja (1.m) hadi moja na nusu (1.5m) kwenda juu isipokuwa vijiti/matawi ya kwanza.

2.2 Zingatia
Biwi/lundo cha mboji kinatakiwa kifunukwe ili kupunguza/kuzuia mvuke ama mvua nyingi ambayo hubeba rotuba kutoka kwenye mbolea. Weka gunia, nyasi ama matawi ya ndizi yaliyokauka.



 Kila tabaka/kunjo/safu yafaa kupangwa kuanzia kwenye ukingo ili lundo la mbolea lisiporomoke.
 Namna nyigine ya kuzuia lundo kuporomoka ni kwa kuweka vipande vya mbao kando ya biwi. Wavu wa nyuzi za chuma utafanya biwi kukauka.



3. Wadudu wenye manufaa na mazingira yanayohitajika kwenye Biwi
3.1 Wadudu ambao husaidia kufanya biwi kuoza
Viumbe wengi wanaohusika na kazi hii ya kuoza ni wadogo hawaonekani kwa macho matupu. Ila viumbe hawa huhitaji maji, hewa na vipande/sehemu ya viumbe wengine ambazo kwao ni chakula. Viumbe hawa hula vipande hivyo na hutoa hewa ya carbon dioxide, maji na joto.
Kuna hatua tatu kubwa wakati biwi linapooza; hatua ya kupanda joto, hatua ya kupoa/kuwa baridi na hatua ya kukomaa.
Wakati ya hatua ya kupanda joto, joto hufikia kiwango cha juu sana katikati mwa biwi. Uzuri wa joto hili ni kwamba magonjwa yaliyokuwa kwenye viungo vya biwi na mbegu za magugu huchomwa hadi kufa. Hatua ya pili ya kuwa baridi; uyoga (fungi) huwa na faida nyingi kwa sababu kazi yake ni kuzisaga nyuzi ngumu ambazo zimo kwenye viungo vya mimea au majani.
Kwenye hatua ya tatu, ‘hatua ya kukomaa’ viumbe wakubwa kama mchwa na nyungunyungu husaidia kusaga na kuchanganya mbolea.
Hali ya anga ikiwa na joto jingi viumbe hawa hufanya kazi haraka kuliko wakati ambapo hali ya anga ni baridi. Aina ya viungo vilivyotumika kujenga/kukuza biwi na ukali/uchungu (pH) wa udongo pia huathiri kiwango cha mbolea kuoza.
3.2 Mazingira yanayohitajika kwenye biwi
Biwi huhitaji vitu vitatu: hewa, maji na joto.

Hewa
Viumbe wadogo kwenye biwi huhitaji hewa ili waweze kuishi. Hewa ya carbon dioxide (CO2) ambayo imetolewa na wadudu hawa huhitaji kutolewa nje. Ikiwa hewa safi itakosekana, viumbe wengine wasiohitajika huingia na kutoa harufu mbaya na pia kufanya mbolea isioze haraka.

Maji
Kazi ya viumbe wadogo huwa polepole ikiwa biwi ni kavu. Aidha ikiwa biwi litalowa maji basi viumbe wadogo watakufa na kufanya biwi kuwa na uchachu badala ya kutengeneza mbolea. Hivyo basi kukagua kiwango halisi cha maji huhitaji ujuzi fulani.
Joto
Biwi hutoa joto wakati linaoza. Lundo likiwa na joto jingi viumbe wadogo hutoka, kisha huweza kurudi pindi linapopoa.
4. Matunzo ya Biwi
Ili kupata mbolea nzuri, biwi linapojengwa yafaa lishughulikiwe kwa utaratibu. Biwi hilo litahitaji maji, kupinduliwa, joto na muda unaofaa wa kukomaa.

4.1 Maji
Wakati wa kiangazi biwi/lundo la mboji huhitaji kumwagiliwa maji kila wiki. Maji katika lundo la mbolea hupimwa kwa kuweka fungu dogo la nyasi na kulitoa baada ya dakika tano. Nyasi isipoonyesha majimaji au unyevu itabidi maji yamwagwe kwenye lundo hilo.
Kuna njia kadha za kuzuia mvuke kuinuka kutoka kwenye biwi, hali kadhalika kiwango cha maji yanayomwagiliwa:
 Funika lundo kwa majani ya ndizi ama nyasi.
 Funika lundo kwa udongo.
 Lundo lisigeuzwegeuzwe

Biwi likilowa maji itabidi kifunuliwe na kuachwa kikauke kwenye jua kabla ya kujengwa tena.

4.2 Kupindua/kugeuza
Katika muda wa wiki tatu (3) baada ya kujenga/kukuza biwi/lundo ukubwa wake utakuwa umepungua sana. Kupindua biwi uhakikishe ya kwamba majani yaliyo kando yameoza pia hewa safi imerejeshwa. Kupindua biwi huchanganya majani yaliyotengenezwa na kukijenga upya. Majani yalivyo kando huwekwa katikati, ikiwa kuna ukavu, maji mengi na majani/viungo vikavu huongezwa. Kupindua kunatikiwa kufanyike kila baada ya wiki tatu.
Hali ya joto na kiwango cha maji yafaa kupimwa siku chache baada ya kupinduliwa. Kupinduliwa kwa mara ya tatu kutahitajika ikiwa viungo havitakuwa vimeoza kikamilifu. 


Mbolea yaweza kutengenezwa bila kupinduliwa ila viungo vilivyo kando havitaoza. Mbegu za magugu na viungo na magonjwa ya mimea hayatakufa. Viungo vilivyobaki hutengwa na kutumiwa kwenye biwi lingine. Japokuwa kugeuza hakuna lazima, kunapendekezwa ili kupata mbolea nzuri.

4.3 Kiwango cha Joto
Kupima kiwango cha joto kwenye biwi kunahitaji kijiti kirefu kichomwe ndani ya lundo siku kumi (10) baada ya kujengwa. Kijiti yafaa kionyeshe joto la kutosha kinapoguswa kwa mkono, la sivyo kuoza bado hakujaanza kufanyika. Katika hali kama hii, maji ama hewa itahitajika kwenye biwi na biwi kuachwa kwa muda. Ikiwa biwi lina joto jingi, biwi linaoza basi viumbe hai wanaweza kufa. Katika hali hii, hewa na maji itabidi kuongezwa ili kufanya biwi lipoe. Kiasi cha joto yafaa kupimwa mara kwa mara kwa kutumia kijiti.



Chini ya 57C
Joto hili linaweza kuivisha mboji lakini haliwezi kuua mbegu za magugu na magonjwa.

57-71C
Joto muafaka kwaajili ya kuivisha mbojj na kuua mbegu za magugu na magonjwa. Katika kiwango hiki cha joto, mbegu zote na vijimelea vyote vya magonjwa vilivyoko kwenye mchanganyiko wa mboji hufa na hivyo kutokuwepo pale mboji inapokuwa imeiva.

Zaidi ya 71C
Joto hili ni kali sana na huweza kusababisha madhara mengineyo kama vile kuzalishwa kwa gesi zenye madhara pia wadudu wenye manufaa ambao husaidia mboji kuiva huweza kukimbia. 


Muhimu kuhakikishakuwa joto halizidi sana ili kuweza kuwa na mboji bora yenye virutubisho




KILIMO BORA CHA NYANYA



Nyanya ni aina ya mboga inayo zalishwa kwa wingi sana duniani. Kwa Tanzania, nyanya ni zao la kwanza katika mazao ya mboga linalo limwa na kuliwa kwa wingi ukilinganisha na mboga zingine. Nyanya hutumika karibu Katika kila mlo. Kulingana na umuhimu wa zao hili kama chakula na pia kama zao linalomwingizia kipato Mkulima, kuna haja ya kutoa mafunzo kuhusu mbinu bora za uzalishaji wake. Pia kuna umuhimu wa kufundisha wakulima kutoka sehemu zingine wasiolima zao hili ili nao waweze kuzalisha nyanya na hivyo kuongeza idadi ya aina za mboga katika maeneo yao.




MAHITAJI YA ZAO LA NYANYA
Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, yasiyo na ukungu mwingi hasa wakati zao linatoa maua na matunda. Zao hili hupenda kipindi kirefu cha jua na joto ili kuongeza ukuaji wa matunda na kupunguza magonjwa ya aina ya ukungu/kuvu. Zao hili halipendi mvua nyingi ingawa linahitaji maji kwa wingi. Katika kipindi chenye mvua nyingi na jua kidogo nyanya hushindwa kutoa maua na matunda ya kutosha bali huweka majani mengi. Katika kipindi hiki pia, nyanya hushambuliwa sana na magonjwa ya ukungu. Nyanya hupendelea udongo unaopitisha maji kwa urahisi na wenye rutuba ya kutosha na hivyo hupenda samadi. Udongo uwe umetifuliwa vya kutosha kuruhusu mizizi kushika vema.


AINA ZA NYANYA
Kuna aina kuu mbili za nyanya kulingana na ukuaji wa mmea: yaani nyanya inayo refuka zenye kuhitaji egemezi (mfano Money maker) na aina ya pili ni nyanya fupi zenye kutoa matawi mengi mfano Roma na Cal J.


UKUAJI WA MICHE
Miche ya nyanya huzalishwa kwenye kitalu kwa kupanda mbegu. Mbegu za nyanya huota baada ya siku 5 hadi 10. Baada ya kukua kitaluni kwa muda wa wiki 4 hadi 5 toka kuota kwa mbegu, miche hupandwa shambani. Kabla ya kupandikiza shambani miche huandaliwa kwa kupunguza umwagiliaji maji kwa siku moja au mbili ili miche izoee hali ngumu kabla ya kuhamishiwa shambani. Hapo shambani miche hupandikizwa kwa kuzamishwa katika kina kirefu zaidi ya ilivyo kuwa kitaluni. Hii inasaidia miche kutoa mizizi ya pembeni mingi zaidi kwa ajili ya kufyonza maji pamoja na virutubisho aridhini. Baada ya kupandikiza mwagilia maji ya kutosha. Usimwagilie maji juu ya mche wa nyanya. Katika kipindi cha jua kali, tandaza nyasi kwenye tuta ili kupunguza upotevu wa maji na unaweza kuweka kivuli kwa kutumia majani ya miti au migomba. Kulingana na aina ya nyanya na rutuba ya udongo, nafasi ya kupandia ni sm 60 kati ya mstari hadi mstari na 45 hadi 60 nafasi ya mche hadi mche. Kama udongo hauna rutuba ya kutosha inapendekezwa kutumia nafasi kubwa ya kupanda.


UTUNZAJI
Nyanya fupi zisizo refuka kwenda juu, ni rahisi sana kutunza na hazihitaji huduma nyingi. Tatizo kubwa ni kuwa kwa kutambaa chini, katika kipindi cha mvua huwa karibu na magonjwa yatokanayo na udongo. Katika kipindi cha jua kali, matunda huungua kwani mmea huwa na majani machache tu yanayo kinga matunda yasipigwe na mionzi ya jua.


MBOLEA
Licha ya mbolea ya kupandia, unashauriwa kuongeza mbolea kipindi cha wiki mbili au tatu baada ya kupandikiza miche bustanini. Mbolea hii ya kukuzia iwekwe kuzunguka shina la mmea kwa umbali wa sentimeta 5 hadi saba kutoka kwenye shina. Kwa mbolea kama vile CAN, NPK, au SA tumia kifuniko kimoja cha soda kwa shina. Mbolea hii inaweza kuwekwa mara mbili kabla ya mvuno wa kwanza. Ili kurefusha kupindi cha uzaaji wa zao la nyanya (na hata mazao mengine yatoayo matunda kama vile nyanya chungu, biringanya, pilipili hoho, nk) inapaswa kuongezea mbolea katika kipindi cha uvunaji mfano baada ya kuvuna mara mbili unashauriwa kuongeza mbolea ya samadi na mbolea kama vile NPK. Hii inasaidia mmea kuendelea kutoa maua bila kuchoka. Kwa kawaida nyanya fupi jamii ya “Roma” huweza kuzaa na kuvunwa kwa kipindi cha wiki 6 hadi 8 tu. Lakini kama utakuwa unaongezea mbolea na kukazania matunzo ya bustani (hasa usafi wa bustani na Kumwagilia maji ya kutosha), nyanya zinaweza kuendelea kuzaa kwa muda mrefu zaidi. Hii ni tofauti
na mazoea ya wakulima wengi kuwa mara nyanya zianzapo kuzaa huduma za palizi na usafi wa shamba huachwa na kutilia maanani kazi ya kuvuna pekee. Hii inajitokeza zaidi kwenye aina ya nyanya fupi.
Kwa nyanya fupi ni vizuri kuhakikisha kuna matawi mengi iwezekanavyo ili kuweza kupata matunda mengi zaidi. Hivyo usipunguze matawi katika aina hii ya nyanya. Kwa nyanya ndefu zenye kuhitaji egemezi,tunashauriwa kukuza nyanya kwa tawi moja lisilo na vichipukizi pembeni au matawi mawili na kuacha mnyanya urefuke.
Kupunguza majani ni muhimu pia katika kupunguza maambukizo ya ukungu katika shina na pia kutoa nafasi ili
mwanga kupenya na kuruhusu mzunguko wa hewa. Majani yapunguzwe kipindi cha asubuhi kwa kutumia mkono na siyo kisu kwani kinaweza kueneza magonjwa kutoka mche hadi mche. Kwa nyanya ndefu, majani ya chini ya matunda huondolewa kadiri unavyo endelea kuvuna. Unashauriwa upunguze majani wakati wa asubuhi kwa kutumia mkono na pia usitoe zaidi ya majani matatu katika mmea kwa mara moja.


UMWAGILIAJI
Nyanya ni zao linalohitaji maji mengi sana kwa ajili ya ukuaji wa mmea na matunda yake. Umwagiliaji uwe wa kulingana kwa kila siku iliyo pangwa. Usibadilishe ovyo kiasi cha maji na ratiba ya kumwagilia. Hii inasababisha kuoza kwa kitako cha nyanya. Pia ili kutunza maji katika udongo, inashauriwa kuweka matandazo katika mzunguko wa shina la nyanya au bustani yote. Nyanya inayo kua vizuri hutumia maji lita mbili kwa siku
katika kipindi cha jua kali. Hivyo katika umwagiliaji ni busara kuzingatia kiasi hiki cha maji katika kipindi kama hiki. Pia kama unatumia keni, mpira au bomba usimwagilie maji juu ya matawi ya nyanya kwani umwagiliaji wa namna hii utasababisha kuenea kwa magonjwa ya ukungu.


MATATIZO YA KILIMO CHA NYANYA
Matatizo yanayosumbua kilimo cha zao hili ni magonjwa na wadudu waharibifu. Hapa tutajifunza mbinu mbali mbali za kuzuia magonjwa na wadudu waharibifu.


WADUDU WAHARIBIFU

FUNZA WA NYANYA (Funza wa vitumba)
Huyu funza hushambulia mazao mengine kama vile pamba, mahindi, mtama, maharage n.k. Mdudu huyu hushambulia matunda ya nyanya kwa kutoboa na hivyo kuyafanya yapoteze soko kwasababu hayafai kuuzwa katika soko na pia yanaweza kuoza wakati wa usafirishaji. Ili kuthibiti piga dawa ya kuua wadudu kama vile thiodan, sevin ya unga, karate, selecron, n.k. Muarobaini hutumika pia katika kupunguza uharibifu wa mdudu huyu.


INZI WEUPE

Wadudu hawa huruka ruka kwenye shamba la nyanya na kukaa chini ya majani. Mdudu huyu hueneza magonjwa ya virusi kama vile “ukoma wa nyanya”. Usafi wa shamba na mazingira ya yake ni muhimu katika kupunguza kuzaana kwa wadudu hawa. Ili kuthibiti wadudu hawa kwenye bustani ya mboga na pia katika maficho yao, piga dawa kama vile karate, cypermethrin mara kwa mara. Panda mimea mingine (kama vile tumbaku) inayo vutia wadudu hawa kwenye maeneo ya bustani kisha piga dawa katika miche ya tumbaku ili kuwaangamiza kwa wingi.



MINYOO
Mdudu huyu hukaa kwenye udongo wenye unyevu wa kutosha. Huvamia mizizi ya nyanya na kuharibu mfumo wa usafirishaji maji na chakula kwenye nyanya iliyo athirika. Uking'oa mche wa nyanya utaona vifundo kwenye mizizi.
KUZUIA
Mbinu za kuthibiti ongezeko la wadudu hawa ni kuharibu hali ya udongo inayo mfanya aishi na kuzaana. Mbinu hizi ni: Kulima shamba kwa kutifua baada ya kuvuna nyanya ili udongo wa chini ukae juani na kukauka. Hii inasaidia kuangamiza wadudu hawa kwa joto na ukosefu wa maji. Choma moto na kuteketeza mabaki ya nyanya baada ya kuvuna. kuzungusha aina ya zao la nyanya au jamii ya nyanya na mazao mengine yasiyo vamiwa na adui huyu. Hii huwafanya minyoo wasipate hifadhi na chakula kutoka kwenye mimea wanayo tumia kuishi na kuzaliana. Hivyo idadi yao kupungua katika udongo. kabla ya kupanda zao weka samadi nyingi katika udongo kwenye eneo lililo athiriwa na wadudu hawa kwani hawapendi udongo wenye samadi nyingi. Panda manung'a nung'a (Tagetes spp) katika eneo lililoathirika na minyoo hawa, mimea hii hutoa sumu ya aina fulani ambayo huathiri ukuaji na kuzaliana kwa minyoo hawa.


MAGONJWA
Uchunguzi umeonyesha kuwa katika maeneo ya Kilombero na Gairo, nyanya na mazao mengine jamii ya nyanya ndiyo hushambuliwa sana na magonjwa kuliko mazao mengine ya mboga.


UKUNGU
Huu ni ugonjwa unaopenda hali ya unyevu mwingi hewani. Hivyo hujitokeza zaidi wakati wa masika. Pia sehemu zenye umande mwingi wakati wa usiku, ugonjwa huu hujitokeza hata wakati wa kiangazi.


DALILI ZAKE
Ugonjwa huu hushambulia shina, maua na matunda. Kuungua kwa majani kama vile yamechomwa na maji moto. Chini ya jani utaona unga unga mweupe. Matunda pia hushambuliwa na ugonjwa huu na hugeuka kuwa meusi na magumu.


KUZUIA
Inabidi kuchanganya mbinu mbali mbali za kupambana na ugonjwa huu. Kwanza ni usafi wa shamba kwa jumla yaani hakikisha unaondoa magugu katika bustani. Tandaza nyasi juu ya matuta yaliyo pandwa nyanya. Ondoa majani yaliyo zeeka na yanayo onyesha dalili za ugonjwa huu. katika kupunguza majani, hakikisha sehemu za chini ya mmea ni wazi na kuna mzunguko mzuri wa hewa. Punguza majani katika mmea ili kupunguza umande na ukungu kwenye mmea. Baada ya kupunguza majani na machipukizi hakikisha unatupa mbali majani hayo na siyo kuyaacha kwenye tuta la bustani. Ondoa kabisa mmea ulio na dalili za ugonjwa huu Kupiga dawa katika kipindi cha mvua mara baada ya mvua kubwa. Fanya hivyo mara moja au mara mbili kwa wiki kutegemea na wingi au mfululizo wa mvua. Unapoona jua limetoka piga dawa ili ugonjwa usijitokeze tena. Baadhi ya madawa yanayofaa kukinga ugonjwa huu ni Dithane M45, Bravo, Benlate , Ridomil, Topsin n.k. Kumbuka kuwa kila
mwaka madawa yenye nguvu zaidi hutengenezwa, hivyo uliza watalaam walioko karibu nawe. Ingawa Blue Copper inauzwa kwa bei nafuu, nguvu yake in kidogo sana kuthibiti huu ugonjwa. Muarobaini pia unaweza kutumika kupunguza ugonjwa huu. Changanya unga unaotokana na mbegu za muarobaini kiasi cha nusu kilo ya unga katika lita 20 za maji.


UKOMA WA NYANYA
Huu ni ugonjwa wa virus unao enezwa na inzi mweupe. Inzi hawa hushambulia zaidi nyanya wakati wa kiangazi, hasa kipindi cha joto kali.

DALILI
Majani machanga hujikunja na baadaye majani yote. Kupungua kwa utoaji maua na matunda na hata yakitokea matunda huwa ni madogo. Mmea kudumaa na kutozaa kabisa.






KUZUIA
Mbinu madhubuti ni kupunguza kuenea kwa ugonjwa huu kwenye shamba kwa kudhibiti kuzaana na kuenea kwa mdudu (inzi mweupe) kama tulivyo ona katika kupambana na mdudu huyo, yaani: Kuondoa mimea michache iliyo shikwa na ugonjwa maana wadudu hawa wanachukua ugonjwa huu kutoka mimea hii. Kutumia mbegu zilizo hakikishwa kuwa zinaweza kuvumilia ugonjwa huu na kutoa mavuno mazuri. Usilime nyanya karibu na eneo lililo na mazao kama bamia,mipapai maana mimea hii huhifadhi inzi mweupe. Kuua inzi weupe wanaofyonza nyanya na kusambaza virusi kwa kutumia madawa. Tumia madawa kama vile Selecron, Decis, Karate n.k. Epuka kuchanganya zao la nyanya na mazao mengine yanayohifadhi hawa nzi kama vile mipapai na bamia. Ng'oa na kuchoma moto mimea yote iliyougua ugonjwa huu.


UGONJWA WA KUOZA SEHEMU YA SHINA INAYOGUSA UDONGO NA MMEMA KUNYAUKA KAMA UMEKOSA MAJI
Wadudu wanaosabisha ugonjwa huu hupatikana ardhini. Hakuna dawa ya kutibu ugonjwa huu baada ya dalili
kujitokeza. Kupiga madawa za viwandani ardhini kabla ya kupanda nyanya husaidia kupungu wadudu wa ugonjwa. Epuka kupanda nyanya au mazao jamii ya nyanya katika eneo moja kwa muda mrefu mfulilizo. Baadhi ya mazao yanayohusiana na nyanya ni bilinganya, pilipili, ngogwe, mnavu, n.k.
Ugonjwa wa miche michanga ya nyanya kuoza sehemu ya shina inayogusa udongo na kufa ghafla
Ugonjwa huu hushambulia miche kitaluni na husabishwa na wadudu waishio ardhini. Mara baada ya dalili, ugonjwa huu hauna dawa ila unaweza kukingwa kwa kutumia njia zifuatazo: Choma moto udongo wa kutengenezea kitalu kabla ya kupanda mbegu zako. Kutumia mboji husaidia kukinga miche dhidi ya ugonjwa huu. Epuka kumwagilia maji kupita kiasi na kutumia kuvuli kizito


MATUNDA YA NYANYA KUOZA KITAKO
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na: Umwagiliaji wa nyanya bustanini usio na mpangilio maalumu. Mfano, kumwagilia mimea maji mengi kisha kuiacha bila maji kwa siku kadhaa. Upungufu wa virutubisho aina ya chokaa. Dalili zake ni matunda ya nyanya kuoza sehemu ya kitako na kuonyesha rangi nyeusi. Kuzuia ugonjwa huu, zingatia kuwa na utaratibu mzuri wa kumwagilia maji ambao haubadiliki ovyo kiratiba na kiasi cha maji
yanayowekwa. Rutubisha mimea kwa madini ya chokaa kwa kutumia mbolea aina ya CAN zenye madini haya.



UPUNGUFU WA WADINI YA FOSFPRASI