KURASA

Thursday, April 30, 2009

DESMODIUM





Huu ni mmea ambao hutambaa adhini kama vile maharage, unapatikana zaidi nyanda za juu na sehemu zisizo na joto, majani yake huwa yana kwaruza na yanaweza kuchana mikono. mbegu zake huzaliwa kwenye vikonyo kama mimea jamii ya kunde kwa wastani mbegu nne



MATUMIZI (FAIDA)
Huu ni mmoja ya mimea ambayo inafaida zaidi ya moja kwa mkulima kama ataamua kuutumia ipaswavyo;




Desmodium inaweza kupandwa katikati ya mistari ya mazao kama mahindi, mtama, alizeti n.k, ambapo mmea huu huweza kusaidia mazao kwa kuongeza kiasi cha nitrojeni kwenye udongo (nitrogen fixer)maua yake huwa yanafukuza baadhi ya wadudu shambani (insect repelent) na mwisho huua magugu mengine yasiweze kuota kwa sababu yenyewe hutambaa juu ya ardhi (runners)na hukua haraka.




Desmodium pia hutumika kama chakula cha mifugo kwa sababu ya protini kiasi cha 18% -22% kabla ya kukaushwa na hushuka hadi 15% yakikaushwa, kwa hiyo mfugaji anaweza kuchanganya na majani ya kawaida na kuwalisha wanyama wake kwa nia ya kuongeza ubora wa chakula.

Friday, April 24, 2009

TANGO-Dawa ya kukausha maziwa mbwa anayenyonyesha



Hii le nitaongelea tunda la tango na madhumuni zaidi ni katika kumsaidia mbwa jike kukausha maziwa. Inaweza kutokea mbwa watoto wake wamekua na kuacha kunyonya au watoto wakafariki wakati bado wadogo mara baada ya kuzaliwa, na maziwa yake yasikauke yenyewe ingawa ni mara chache sana.





Maziwa yasipokauka yatamsababishia ugonjwa wa chuchu ujulikanao kama (mastitis)ambao husababisha maziwa kuvimba baada ya kushambuliwa na bakteria, tiba yake huwa ghari kiasi sana na mara chache husababisha vifo kwa mbwa.




Sasa basi kwa njia rahisi ukitaka kuepukana na hali hii inatakubidi kumsaidia mbwa wako kukausha maziwa, katika chakula chake msagie tango moja (1)ambalo limeondolewa maganda nusu na nusu kubakia kwa muda wa siku 3 mpaka 5 au mpaka maziwa yakauke.





BINADAMU
Kwa binadamu tango ni dawa la magonjwa mengi na kinga pia, inashauriwe liliwe likiwa na maganda yake kiasi yaani usimenye maganda yote. magonjwa yanayotibiwa na tango ni KUHARISHA magonjwa mengine ni kama presha ya kupanda na kushuka pia husaidia kurekebisha ngozi ya mwili

Sunday, April 12, 2009

MALARIA-Jinsi ya kuharibu mazalia ya mbu

MBU



Malaria limekuwa ni tatizo kubwa sana kwa nchi kama Tanzania, ambazo ni masikini na uwepo wake katika ikweta kunifanya iwe na joto na hivyo uwepo wa mbu wengi sana. Makala nyingi na kampeni zimekuwa juu ya kutibu malaria na nyingine juu ya kukinga malaria kwa njia kama za kutumia vyandarua vyenye dawa, kumeza dawa kwa wale wanaotembelea maeneo yenye mbu wengi (hasa wanaotoka ughaibuni) ambako hamna malaria
Njia kubwa ya kujikinga na malaria ni kuharibu mazingira ya mbu kuzaana, kwenye mazingira mengi tunayoishi ndizo sehemu mbu wanakozaliana, kwa hiyo inatubidi kufanya yafuatayo kupunguza au kuondoa mazalia ya mbu.


MADIMBWI

Kufukia madmbwi yote yanayozunguka nyumba tunazoishi na mazingira tuliyopo ili kuhakikisha hamna maji yanayotuama jirani na makazi yetu. Hii pia inahusisha kuondoa vitu vyote vinavyoweza kuhifadhi maji mara mvua inaponyesha, vitu kama vifuu vya nazi, makopo, matairi ya magari n.k


MAJANI

Ni muhimu kufyeka au kulima majani yote na vichaka kuzunguka makazi yetu hasa vipindi vya mvua, pia maua ambayo ni urembo wa nyumba zetu nayo inabidi yapunguzwe kipindi hiki. Kwa kawaida mimea huwa na uwezo wa kutuamisha maji kidogo sana kwenye majani yake lakini mbu nao hutaga humo humo.


NJIA NYINGINE
Kuna baadhi ya mimea ambayo inauwezo wa kufukuza wadudu, kwa mfano mmea unaojulikana kama nyonyo (cast oil) ukipandwa karibu na makazi yetu una uwezo wa kufukuza mbu (repellent) na mbegu zake zikipondwa na kuchanganywa na maji na kisha kumwagwa sehemu basi huweza kufukuza wadudu kama mbu.

MMEA WA NYONYO (castor oil)



Kupulizia dawa za kuua wadudu (mf Icon) ni njia nyingine ya kuzuia mbu kuzaana, hii ni njia ya kemikali kwa hiyo iwe ya mwisho baada ya hizi za mwanzo zote kushindwa kufanya kazi au kutonyesha mafanikio.

Friday, April 10, 2009

UMUHIMU WA MITI

SEHEMU YA MSITU




Kuna usemi usemao MISITU NI UHAI ambao nina uhakika kila mtu anaujua vema, swala kubwa hapa ni jinsi ya kuitunza hii rasilimali ya asili tuliyopewa na mungu. Misitu yetu ambayo tunaitegemea kwa mambo mengi sana siku hizi imekuwa ikikatwa miti yake kwa ajili ya matumizi mbali mbali kama mbao na kuni, matumizi mengine kama dawa huwa hayana athari sana kwa misitu kwa sababu mtumiaji huchukua sehemu tu ya mti.

MTI WA MVULE


Kuna misitu ya asili na ile ya kupandwa, hii ya kupandwa iko ya aina mbili, kuna yenye miti ya asili ambayo madhumuni yake huwa ni kutunza mazingira au kurudisha hali ya uasilia (uoto wa asili) na kuna miti ya kigeni ambayo mara nyingi huwa kwa matumizi ya biashara au kipato, miti ya kigeni ni kama mikaratusi, mitiki (misoji), mipine, mivinje, migravilea n.k






Adui mwingine mkubwa wa misitu ni moto, vyanzo vya moto vinaweza kuwa shughuli za kilimo kwa maana ya kusafisha shamba, uwindaji ukiwa na nia ya kufukuza wanyama toka upande mmoja hadi mwingine, na urinaji wa asali ambapo moto huwashwa halafu majani mabichi ya aina fulani huchomwa ili kutoa moshi ambao huwalewesha nyuki.







VYANZO VYA MAJI

Vyanzo vingi vya maji huanzia kwenye misitu juu ya milima ambapo huanza kama chem chem kisha vijito halafu maji hutiririka kama mto. Kazi ya misitu ni kuzuia yale maji maji kuzama ardhini (mizizi) na pia majani ya miti huzuia maji maji yasichukuliwe kama mvuke

Chem chem nyingine hupita chini ya ardhi na kwenda kuibuka sehemu nyingine kama kisima cha asili, sehemu za misitu ambazo zimeharibiwa na ukataji miti kiasi cha kuathiri mfumo wa maji basi miti kama mikuyu na mikangazi hushauriwa kupandwa kwa wingi sehemu hizi, ingawa bado miti ya asili ya sehemu husika nayo pia inaweza kupandwa.Miti ya asili nchini kwetu ni kama mivule, mipodo, mininga, mikangazi, mikarambati n.k