KURASA

Thursday, May 22, 2014

JINSI YA KUKATA MICHE YA MISOJI (MITIKI) marudio

Hii post niliwahi kuituma siku za nyuma (Friday, March 26, 2010) kutokana na maombi ya baadhi ya wasomaji ninaiweka tena. Kwa kawaida miche ya misoji mara baada ya kutolewa kwenye kitalu huitaji kukatwa, mjasiliamali aliyeko jijini Mwanza aitwae NAYMA aliniomba nimwelekeze kwa picha na mimi bila hiyana nilikwenda shamba na kung,oa mche mmoja na kuukata na kuupiga picha kabla ya kuukata na baada ya kuukata ili kupata kipandikizi

MCHE KABLA YA KUKATWA (angalia mishale kujua sehemu za kukata)


Mche wangu niliukata na kuacha kiasi cha nchi mbili au pingili mbili za vidole kwa sehemu ya juu ya mzizi na kwenye mzizi niliondoa ile sehemu nyembamba ya chini, kwa kawaida hii sehemu ya chini hufa mara baada ya kupandwa kwa sababu sehemu nene/kubwa ya mzizi inayoachwa ndiyo huifadhi maji na chakula cha mmea, nadhani hapa nitakuwa nimemsaidia kama bado nipigie kwenye ile namba niliyokupa

KIPANDIKIZI TAYARI KWA KUPANDWA


Kumbuka wakati wa kupandwa lazima uweke kisahani ili kiweze kukusanya maji kwa ajili ya ukuaji mzuri, kama ni udongo unaotuamisha maji usiweke kisahani bali wekea kama tuta au mwinuko

WEKA KISAHANI KAMA UDONGO HAUTUAMISHI MAJI


WEKA TUTA KAMA UDONGO UNATUAMISHA MAJI