KURASA

Wednesday, July 25, 2012

TARATIBU NA MASHARTI YA MKOPO WA KUKARABATI TREKTA



1. Mwombaji atajaza fomu maalum ya maombi inayopatiakana kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa na kweye tovuti ya mfuko. Fomu hii itapitishwa na Afisa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya husika.

2.  Afisa Zana katika Halmashauri watashirikiana na mmiliki pamoja na fundi wake kufanya tathmini ya kiwango cha ubovu wa matrekta hayo katika maeneo yaliyoanishwa katika taarifa ya tafiti za awali ya ukarabati. Mapendekezo yazingatie kiwango cha matengenezo ili gharama za vipuri na fundi zisizidi kiwango cha juu kinachoweza kutolewa.

3. Mwombaji atachagua Mtengenezaji/Fundi kutoka  kwenye  orodha ya  kampuni zitakazoingia mkataba na Mfuko wa Pembejeo. Mtengenezaji/Fundi atafanya ukarabati chini ya usimamizi na ukaguzi wa Afisa Zana. Mtengenezaji/Fundi atawajibika kutoa hati ya kuthibitisha ubora wa kazi/matengenezo na gerentii  ya  miezi  sita  kwa  vipuri vilivyokarabatiwa.

4.  Fomu za maombi pamoja na vielelezo vinavyohitajika zitatumwa kwa Mkurugenzi Mtendaji, Mfuko wa pembejeo.

5.  Dhamana ya mkopo huu ni kadi halisi ya trekta na mali nyingine isiyohamishika.

6. Muda wa mkopo ni mwaka mmoja na nusu kwa riba ya asilimia nane (8%).

7.  Mwombaji sharti awe tayari kutoa huduma ye kukodisha trekta hilo kwa wakulima wenzake

TARATIBU NA MASHARTI YA MKOPO WA KUNUNUA TREKTA JIPYA

1.Mwombaji atajaza fomu maalum ya maombi inayopatikana katika Ofisi za kilimo za Halmashauri za Wilaya na Makao makuu ya Mfuko wa Pembejeo, jijini Dar-es-salaam na katika tovuti ya wizara ya kilimo.

2. Fomu za maombi zilizojazwa na kuambatanishwa na vielelezo vinavyohitajika zitapitishwa/kuidhinishwa na Afisa Kilimo wa Maendeleo ya Mifugo wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya husika na baadaye kutumwa mapema kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Pembejeo.

 3. Mikopo ya kununua matrekta inatolewa na Mfuko wa Pembejeo, baadhi ya benki na taasisi za fedha na     SCCULT (T) Ltd. kwa niaba ya Mfuko, mwombaji sharti atimize yafuatayo:-
a.    Awe na dhamana yenye hati miliki isiyohamishika iliyoandikishwa kwa jina la mwombaji.
b.    Awe na shamba binafsi lisilopungua hekta 50 na awe tayari kutoa huduma ya kuwalimia wakulima wengine
c.    Awe tayari kutekeleza masharti yote ya Mfuko wa Pembejeo au taasisi ya fedha na SCCULT yanayohusu mkopo wa ununuzi wa trekta jipya.
d.    Awe tayari kulipa asilimia moja (1%) ya mkopo kama gharama za nyaraka za mkopo na kusajili trekta kwa pamoja kwa jina lake na Mfuko
e.    Riba inayotozwa ni asilimia nane (8%) na marejesho hufanyika kwa muda wa miaka mitatu kila baada ya miezi mitatu.

KILIMO BORA CHA MPUNGA CHA UMWAGILIAJI


Maandalizi sahihi ya shamba ni jambo la msingi katika kuboresha kilimo cha umwagiliaji wa mpunga. shamba lisipoandaliwa vema husababisha mbinu bora zinazoshauriwa kutoonyesha matokeo katika kiwango kinachotarajiwa hasa katika uzalishaji. Kimsingi maandalizi ya shamba yanatakiwa yafanyike kwa usahihi
na kwa wakati katika mtiririko unaotakiwa. Zifuatazo ni hatua saba muhimu na za msingi katika kilimo cha mpunga

1. KUSAFISHA SHAMBA
Safisha shamba mapema kabla ya msimu kuanza. Kusanya na kuangamiza visiki na takataka nyingine zote. Masalia ya mazao yanaweza kutumika kutengeneza mbolea  ya mboji. Inapobidi tumia moto kwa uangalifu sana maana moto unaweza kuharibu mazingira, unaua wadudu rafiki, unaharibu udongo na kuteketeza mboji.

2. KULIMA
Kulima husaidia kupunguza kiasi cha magugu, huruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji, hurahisisha mizizi kupenya na kuchanganya masalia ya mazao kwenye ardhi. Wakati wa kulima uangalifu unahitajika ili kuzuia kuharibu usawa wa ardhi. Kina cha kulima kiwe kati ya sentimeta 10 na 15. Ili kurahisisha na kuharakisha kazi ya kulima ni vema kutumia zana/mashine rahisi kama Trekta la mkono na wanyamakazi 

3. KUKARABATI/KUJENGA MAJARUBA
Baada ya kulima hakikisha kuwa kingo za jaruba zimekarabatiwa ili kuweza kuhifadhi maji vema. Kama ni shamba jipya, ujenzi wa kingo za jaruba  ufanyike kwa kufuata utaalamu unaotolewa. Kingo imara ni muhimu kudhibiti vema maji shambani. 
 
4. KUVURUGA
Weka maji shambani kiasi cha sentimeta 3 hadi 5 juu ya usawa wa ardhi ili kukamilisha vema uvurugaji. Jembe la mkono linatumika lakini ili kurahisisha na kuharakisha kazi hii ni vema kutumia trekta la mkono au wanyamakazi. Unapotumia wanyamakazi au trekta la mkono weka maji shambani si zaidi ya siku moja kabla. Shamba lililovurugwa vema huiwezesha mizizi ya miche kupenya vema ardhini.

5. KUSAWAZISHA SHAMBA
Baada ya kuvuruga ni lazima kuhakikisha kwamba shamba limesawazishwa vema. Shamba lililosawazishwa vema linaruhusu usambaaji mzuri  wa maji. Wakati wa kusawazisha kina cha maji kiwe kiasi cha sentimeta 3-5 juu ya usawa wa ardhi Ili kurahisha kazi hii tumia reki ya ubao ili kuvuta udongo kutoka sehemu zilizoinuka kuelekea sehemu zilizo bondeni

6.VYANZO NA ATHARI ZA UPOTEVU WA MAJI YA UMWAGILIAJI
Ili kupata maji ya kutosha inabidi kuhakikisha kwamba upotevu wa maji ya umwagiliaji unapungua kwa kiwango kikubwa na wakulima wanamwagilia maji kwa kiasi kinachohitajika bila kuzidisha kiwango.

Vyanzo vya upotevu wa maji ya umwagiliaji katika skimu za mfano ni pamoja na:
•  Maji yanayopotea kwenye mifereji mikuu, ya kati na ile midogo ya kusambaza maji mashambani.
•  Maji yanayopotea mashambani wakati wa kumwagilia.

Upotevu wa maji kwenye mifereji mikuu, ya kati na ile ya kusambaza maji unasababishwa na aina ya udongo uliotengeneza kingo za mfereji, uchafu na matengenezo hafifu ya mifereji.  Katika baadhi ya skimu upotevu wa maji kwenye mfereji mkuu uliosababishwa na kuvuja maji kwenye tuta la mfereji mkuu na kunywea chini ya ardhi ulikuwa mkubwa kiasi cha kuathiri upatikanaji wa maji kwenye  mashamba yaliyoko mbali na banio.Vilevile athari nyingine ilikuwa ni maji mengi kuingia sehemu yasikohitajika na kusababisha tatizo la maji kutuama kwa muda mrefu.Hivyo wakulima wanashauriwa kupunguza upotevu huu wa maji kwenye mfereji kwa kujengea na kusakafia. Upotevu wa maji mashambani wakati wa kumwagilia unasababishwa na kuvuja kwenye tuta linalozunguka jaruba, kunywea chini na kuzidisha kiwango cha maji ya kumwagilia kinachotakiwa. Hii mara nyingi inasababishwa na utengenezaji mbovu wa jaruba. utengenezaji wa majaruba na uimarishaji wa kingo za jaruba umesaidia kupunguza upotevu wa maji kwa kiwango kikubwa na hatimaye kuongeza mavuno na kipato cha mkulima. 

7. UPANDIKIZAJI MPUNGA
Ili kupata mavuno mengi na kukifanya kilimo cha mpunga kuwa cha faida ni muhimu  wakulima kuzingatia mbinu hii muhimu na kuachana na kilimo cha kiholela kwa kumwaga mbegu moja kwa moja shambani. Aidha kwa wakulima wanaofuata kanuni hii wamepata mafanikio makubwa. 

Faida zinazopatikana kwa kupandikiza mpunga
•  Mkulima huweza kuchagua miche bora na mizuri ikiwa  kitaluni.

•  Miche hukua haraka na yenye afya .
•  Kiasi kidogo cha mbegu huhitajika.
•  Mavuno huwa mengi.

Njia  za kupandikiza miche ya mpunga
Zipo njia kuu mbili za kupandikiza miche ya mpunga, nazo ni: 
•  Kupandikiza kwa mistari
•  Kupandikiza bila ya kufuata mistari (Mchaka mchaka).

Aidha kati ya njia hizi mbili, njia ya kupanda kwa mistari ndiyo inayopendekezwa.zaidi. Pamoja na kwamba upandikizaji wa mistari unahitaji nguvu kazi zaidi, njia hii imeonyesha kuwa na mafaniko mengi ikilinganishwa na kupandikiza kiholela. Shamba lililopandwa kwa mistari ni rahisi kupalilia kwa kutumia kipalizi cha  kusukuma kwa mkono. Pia ni rahisi kwa mkulima  kupanga idadi ya mashina/mimea kwa eneo kwa  uchagua nafasi aitakayo itakayompa mazao mengi.

Uandaaji wa miche
Kabla ya kupandikiza miche shambani ni muhimu kufanya maandalizi yafuatayo:  
•  Inashauriwa kumwagilia miche kwanza ili kupata urahisi wa kungo’a
•  Ili kuzuia miche isikatike ovyo, miche ing’olewe kwa kushikwa chini zaidi ya shina
•  Epuka kung’oa miche mingi kwa wakati mmoja
•  Miche ifungwe kwenye mafungu madogo madogo ili kurahisisha usafirishaji na upandikizaji  shambani
•  Miche bora tu ndio ichaguliwe. Sifa za miche bora
•  Iwe na kimo kinacholingana, 
•  Iwe na majani mafupi yaliyosimama, yenye mizizi mingi na yenye afya, isiyoshambuliwa na wadudu wala magonjwa, 

Jinsi ya kupandikiza miche
•  Miche ishikwe  kwa vidole vitatu kama inavyoosha kweye picha chini 
•  Pandikiza kati ya miche 2 -3 kwa kila shina
•  Kwa mafanikio zaidi, miche ipandikizwe katika kina cha sentimita 2-3.



Friday, July 20, 2012

KUKU WA KIENYEJI WANAUZWA


Kuku wa kienyeji wenye uzito kati ya kilo moja na nusu na kuendelea wanauzwa bei ni kuanzia shilingi elfu kumi mpaka elfu kumi na tano tu (10,000 - 15,000) kutegemeana na ukubwa wa kuku mwenyewe kuku wanapatikama wengi kama 200, 


Pia mayai ya kuku wa kienyeji yapo , kwa trei moja ni shilingi elfu kumi tu (10, 000)kwa maulizio piga namba 0755-462970 ulizia Livin Matabaro

Tuesday, July 3, 2012

SUMA JKT NA SABA SABA

 FARMTRAC trekta bora kwa ajili ya kilimo cha kisasa






Kuku wazazi (parent stock) kwa ajili ya kuzalisha vifaranga vya kuku bora wa mayai na wa kienyeji (improved breed)



Battery cages kwa ajili ya kufugia kuku wa mayai, mfumo huu hutumia sehemu ndogo tu ya banda kufuga kuku wengi, na ni rahisi kwa sababu mifumo ya maji na chakula unaweza kuweka inayojiendesha yenyewe (automatic) na pia ni rahisi kukusanya mayai na haya vunjiki hovyo


 Hawa ni bata wa kawaida


 Bata mzinga
F

SABA SABA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

  Hii ni sehemu ya kwanza mara baada ya kuingi akwenye banda hili ambapo utakutana na sanamu kadhaa za wanyama wa mbugani













 Hii ni sehemu ya nyuma kwenye wakala wa mbegu za miti, hii ni baadhi ya miche inayopatikana kwenye vitalu vyao



Huu mti unaitwa msabuni au mhalinta





Mzinga wa nyuki wa kufugwa, huu ni mzinga wa kisasa kabisa







Mdau akinunua mbegu za miti ya misoji (mitiki) kutoka kwa wakala wa mbegu za miti (TTSA) kwa ajili ya kuotesha mwenyewe


PAN 4M-19 MBEGU BORA YA MAHINDI





aka MKOMBOZI mbegu bora kutoka kampuni ya mbegu ya PANNAR, mbegu hii ya chotara inafaa sana kwenye maeneo mbali mbali ya ukanda wa chini na kati wenye mvua kidogo na inavumilia sana ukame. mbegu hii ndiyo mkombozi wauhakika na itakufanya uepukana na njaa haswa katika kipindi hiki ambacho hali ya hewa haitabiriki





  • Punje zake ni ngumu za zinakoboleka vizuri, haishambuliwi na wadudu kwa urahisi na inauwezo wa kutoa magunia 25 kwa ekari moja
  • Inafaa kwenye maeneo mengi yenye hali mbaya ya hewa hasa ukame
  • Inavumilia sana magonjwa ya majani kama maize strips
  • Ni matamu sana kwa kuchoma
  • Inakomaa mapema sana siku 90 - 100 tangu kupanda
  • Inauwezo wa kutoa mahindi mawili mawili


Kwa wanaokwenda saba saba watembelee nyuma ya banda la PTA kwenye bustani za jeshi la magereza
na kwa mawakala wa jumla wasiliana nao kwa mawasiliano haya
P.O.BOX 10677 Arusha Tanzania
Tel +255 (0)27 250 4669
Fax +255 (0) 27 254 4669
info@pannar.co.tz
www.pannar.com