KURASA

Tuesday, July 3, 2012

SUMA JKT NA SABA SABA

 FARMTRAC trekta bora kwa ajili ya kilimo cha kisasa


Kuku wazazi (parent stock) kwa ajili ya kuzalisha vifaranga vya kuku bora wa mayai na wa kienyeji (improved breed)Battery cages kwa ajili ya kufugia kuku wa mayai, mfumo huu hutumia sehemu ndogo tu ya banda kufuga kuku wengi, na ni rahisi kwa sababu mifumo ya maji na chakula unaweza kuweka inayojiendesha yenyewe (automatic) na pia ni rahisi kukusanya mayai na haya vunjiki hovyo


 Hawa ni bata wa kawaida


 Bata mzinga
F

SABA SABA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

  Hii ni sehemu ya kwanza mara baada ya kuingi akwenye banda hili ambapo utakutana na sanamu kadhaa za wanyama wa mbugani

 Hii ni sehemu ya nyuma kwenye wakala wa mbegu za miti, hii ni baadhi ya miche inayopatikana kwenye vitalu vyaoHuu mti unaitwa msabuni au mhalinta

Mzinga wa nyuki wa kufugwa, huu ni mzinga wa kisasa kabisaMdau akinunua mbegu za miti ya misoji (mitiki) kutoka kwa wakala wa mbegu za miti (TTSA) kwa ajili ya kuotesha mwenyewe


PAN 4M-19 MBEGU BORA YA MAHINDI

aka MKOMBOZI mbegu bora kutoka kampuni ya mbegu ya PANNAR, mbegu hii ya chotara inafaa sana kwenye maeneo mbali mbali ya ukanda wa chini na kati wenye mvua kidogo na inavumilia sana ukame. mbegu hii ndiyo mkombozi wauhakika na itakufanya uepukana na njaa haswa katika kipindi hiki ambacho hali ya hewa haitabiriki

  • Punje zake ni ngumu za zinakoboleka vizuri, haishambuliwi na wadudu kwa urahisi na inauwezo wa kutoa magunia 25 kwa ekari moja
  • Inafaa kwenye maeneo mengi yenye hali mbaya ya hewa hasa ukame
  • Inavumilia sana magonjwa ya majani kama maize strips
  • Ni matamu sana kwa kuchoma
  • Inakomaa mapema sana siku 90 - 100 tangu kupanda
  • Inauwezo wa kutoa mahindi mawili mawili


Kwa wanaokwenda saba saba watembelee nyuma ya banda la PTA kwenye bustani za jeshi la magereza
na kwa mawakala wa jumla wasiliana nao kwa mawasiliano haya
P.O.BOX 10677 Arusha Tanzania
Tel +255 (0)27 250 4669
Fax +255 (0) 27 254 4669
info@pannar.co.tz
www.pannar.com