KURASA

Monday, September 11, 2017

UANDAAJI WA MBEGU ZA PAPAI

Uandaaji wa mbegu za mipapai imekuwa ni changamoto kwa baadhi ya watu, leo nitaongelea uaandaaji wake mpaka kupanda na kupata miche yako
 Mbegu tulizotumia leo ni LADY RED ambazo hufaahamika zaidi kama Malkia FI toka nchini Taiwan na huzalishwa na kampuni inayojulikana kama KNOWN-YOU kama zinavyoonekana hapo pichani

 Fungua mbegu zako na uziweke kwenye chombo kisafi kisha jaza maji kiasi, ziloweke humo kwa siku 5 na kila siku badilisha maji
 Siku ya 6 zitoe na uziweke kwenye kitambaa kisafi kukwepa mashambulizi ya fangas, Funga vizuri na  lowesha maji kitambaa chako na ukihifadhi sehemu salama


Zoezi hili linatakiwa kufanyika ndani ya nyumba au banda ambalo litazikinga mbegu dhidi ya jua la moja kwa moja
 Siku ya 7 ukifungua utaona baadhi ya mbegu zimeanza kupasuka na tayari kwa kuanza kuota, panda mbegu zako moja moja kwenye viriba ambavyo ulishaviaandaa kabla kwa kuvijaza udongo wenye rutuba, kama utaweka mbolea hakikisha ilishaoza kabla, viriba viwekwe kwenye kivuli hasa chini ya miti

 Baada ya siku kadhaa mbegu zako zitaanza kuota kama inavyoonekana pichani
 Udongo unatakiwa uwe wenye rutuba na usiotumisha maji
Hakikisha unamwagia maji kila siku angalau mara moja na hasa jioni wakati hali ya joto imepungua

 Baada ya wiki 2 miche itakuwa imefikia kimo cha sentimeta tano, hapa unaweza kuongeza mbole ya kukuzia kama ya kuku na pia kuondoa miche yako kwenye kivuli na kuiweka juani kama njia ya kuandaa kukabiliana na hali ya shamba (hardening off)