KURASA

Friday, January 7, 2011

KAMPUNI YAINGIZA MIKARATUSI YENYE UGONJWA SERENGETI

Kampuni ya tumbaku ijulikanayo kama Alliance One Tobacco imeingiza miche ya mikaratusi toka nchini Kenya yenye Magonjwa na kuisambaza kwa wakulima wilayani Serengeti.

Magonjwa hayo ni ugonjwa wa kukauka miche pamoja na ugonjwa wa mizizi (Eucalyptus root disease)imebainika na wataalamu toka maabara ya Chuo kikuu cha Sokoine (Morogoro) kwamba magonjwa hayo hayatibiki, ila ugonjwa unaweza kudhibitiwa kabla haujaibuka kwa kupiga dawa iana ya Acephate au Confidor wakati miche ipo kitaluni kabla ya kupandwa shambani.



Kitaalamu nashauri kabla ya kuingiza mbegu au miche ni lazima uchunguzi ukafanyika kwa kina ili kugundua kama kuna magonjwa ambukizi, kwa sababu kuna aina zaidi ya 200 za mikaratusi

kwa ushauri zaidi kwa mtu anayetaka miche au mbegu za miti, basi awasailianae na wakala wa mbegu za miti wa taifa (TTSA) ambao wapo Morogoro eneo la kihonda, pamoja na hayo baadhi ya tafiti zimeonyesha kwamba mikaratusi inaathari kwa mazingira kwa sababu inatumia kiasi kikubwa cha maji na kusababisha ukame hasa kipindi hiki cha mabadiliko katika tabia nchi



WITO sehemu kama serengeti ambapo ni urithi wa dunia nashauri makampuni na watu binafsi wajitahidi kupanda miti ya asili na kuachana na hii miti ya kigeni kama mikaratusi, sijaelewa pia kwa nini miti itoke nchi jirani ya Kenya wakati wangeweza kuanzisha vitalu hapa hapa nchini kwa kutumia mbegu ambazo tunazo tena za miti ya asili

UJERUMANI KATIKA KASHFA YA SUMU AINA YA DIOXINE

Nchi ya Ujerumani imeeingia katika kashfa baada ya mayai na kuku kukutwa na kirutubishi ambacho ni sumu aina ya dioxine ndani yake, inaaminika kwamba kirutubishi hicho kilisambazwa kati ya mwezi Novemba na Disemba mwaka jana kwa kampuni 25 za kutengeneza vyakula vya mifugo.



Sumu hiyo iligundulika katika majimbo 7 nchini Ujerumani wiki iliyopita, lakini wiki hii kimegundulika nchini Uholanzi ambapo Ujerumani iliwauzia mayai na kuku walioathiriwa na sumu hiyo.

Kiasi cha mayai 136,000 (toka kampuni mbali mbali za kuzalisha mayai )tayari yamegundulika kuwa na sumu hiyo, sumu hiyo iliingizwa katika virutubishi chakula (concentrates) kiasi cha tani 3000 ambazo zilinunuliwa na kutumiwa na makampuni mbali mbali.



mayai na kuku wote wenye sumu hiyo wakizuiliwa kuuzwa kwa matumizi yz Binadamu, Uchunguzi unaendelea ilikujua kama sumu hiyo ipo kwenye mazao menine ya mifugo kama nyama za ng;ombe na nguruwe, maziwa n.k