KURASA

Friday, December 24, 2010

SALAMU TOKA KWA DADA NAYMA



Kaka Ben Salaam
Leo nimekula ugali nyama na mchicha. Jana nilienda shamba nikachuma mchicha wa shambani kwangu, na mahindi ya ugali wa shambani kwangu, baadhi ya siku huwa nakula kande jioni ya mahindi ya shambani kwangu huwa nakula ndizi za shambani kwangu nakula mayai ya mifugo yangu na mapapai makomamanga, mihogo na viazi kuku wa kienyeji mifugo yangu mapera na mastafeli.



Unajua nilianzaje kupenda kilimo? niliingiwa uchungu siku moja kwenda sokoni nikauziwa papai sh 1500/- du nikaamua kuanza kupanda site miti ya matunda hadi ikawa imezidi ndipo nikaamua kutafuta shamba kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani kwangu nilifanikiwa hivyo matunda mengi siku hizi nakula natoa site nilikopanda miaka ya nyuma kuna ndizi aina kama sita, michungwa miwili mfenesi mmoja umeshaanza kuzaa muembe mmoja mkomamanga m-peach na m-apple ingawa hiyo m-apple sijala matunda bado mihogo kidogo. Huko shambani ndoko nimepatas uhuru wa kupanda kila ninachoona nakipenda ili niweze kula. Nusu ua shamba napanda mitiki kwa ajili ya kulinda shamba langu, Hahahahaha Back to Eden.

NAYMA























Monday, December 13, 2010

KILIMO BORA CHA PILIPILI HOHO

Jina la kitalaamu la PILI PILI HOHO ni Capsicum annum. Asili ya zao hili ni bara la Amerika ya Kusini. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Iringa, Tanga (Lushoto), Mbeya, Ruvuma, Tabora na Arusha. Kilimo hiki kinaendeshwa na wakulima wadogo katika maeneo yenye ukubwa wa kati ya hekta 0.2-0.4 pia kuna maeneo ya wakulima wakubwa wenye hekta kati ya 2-20. Wakulima hao hujishughulisha na kilimo cha zao hilo kwa njia ya mkataba na kampuni hiyo.

Hoho hutumika katika kutengeneza rangi za asili za vyakula ambazo kwa sasa hupendwa zaidi kuliko zile zinazotokana na kemikali na pia huongeza ladha na harufu katika vyakula. Hivyo hutumika katika viwanda vya kusindika vyakula, kwa mapishi ya nyumbani na hata katika viwanda vya vipodozi kama rangi ya mdomo, uso n.k. Ina virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kama madini ya chuma, vitamin A na C.




2.0 TABIA YA MMEA
Hoho ni zao la jamii ya pilipili isiyo kali, tunda lake ni nene kiasi la duara pia linaweza kuwa lililochongoka,.

3.0 ENEO NA HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO
Hoho hustawi vema katika maeneo ya usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 2,000 yenye mvua ya wastani wa mm.600-1,250 na wastani wa joto la nyuzi za sentigredi 21 hadi 24. Udongo wa tifitifu wenye rutuba, usiotuamisha maji na wenye hali ya uchachu (pH) kati ya 5.0-6.5 hufaa zaidi. Umwagiliaji ni muhimu pale mvua inapokuwa chache.

4.0 UZALISHAJI
4.1 UTAYARISHAJI WA KITALU

Chagua eneo katika ardhi isiyo na mtelemko mkali na yenye rutuba ya kutosha. Ardhi iwe imepumzishwa bila kuoteshwa mazao ya jamii ya pilipili, biringanya, nyanya, n.k. ili kuepukana na mashambulizi ya wadudu na magonjwa.
Tayarisha kitalu kabla ya msimu wa mvua. Andaa vizuri matuta manne yenye urefu wa wastani wa mita 10 kila moja na upana wa mita moja (1) ili kustawisha miche inayotosha ekari moja.

Acha njia ya nusu mita kati ya tuta na tuta. Mwagilia maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu na endelea kunyweshea kulingana na hali ya hewa na hali ya udongo. Sia mbegu kwenye, mstari, nafasi kati ya mstari na mstari ni sm 10 na kina cha sm1. Kiasi cha mbegu cha nusu kilo kinatosha eneo la hekta moja. Weka matandazo kwenye kitalu au tumia nailoni nyeusi ili kuhifadhi unyevunyevu na kuzuia uotaji wa magugu.

4.2 UTAYARISHAJI WA SHAMBA

Shamba lilimwe vizuri na kuweka matuta ili kuhifadhi unyevunyevu na kurahisisha umwagiliaji. Matuta yanaweza kuwa makubwa au madogo kulingana na matakwa ya mkulima. Matuta makubwa hupandwa mistari miwili na matuta madogo hupandwa mstari mmoja.




4.3 UPATIKANAJI WA MBEGU

Mbegu ambazo hutumika ni chotara ambazo huuzwa kwenye maduka ya pembejeo za kilimo nchi nzima. Haishauriwi kutumia mbegu kutoka zao la msimu uliopita kwani ubora wa paprika utaharibika na hivyo kuharibu soko unashauriwa kununua mbegu bora.

4.4 UPANDAJI
Mbegu huoteshwa na kukuzwa kitaluni kwa muda wa wiki 6-8 na miche hupandikizwa shambani ikiwa na urefu wa sm.6-10. Mwagilia maji kitaluni kabla ya kuhamisha miche. Panda shambani kwa nafasi ya sm.75-90 kati ya miche kwa sm.90-105 kati ya mistari, wastani wa miche 12,500 itapatikana kwa hekta. Weka samadi shambani tani 25-37 kwa hekta wiki 1-2 kabla ya kupandikiza miche, au kilo 560-670 za NPK (mbolea ya viwandani) kwa hekta kwa uwiano wa 4:7:7 katika udongo usio na rutuba ya kutosha.

ITALIAN PAPRIKA



5.0 KUHUDUMIA SHAMBA
Palizi ifanyike mara magugu yanapotokea shambani. Umwagiliaji maji ufanyike kama ilivyo kwa mazao mengine kama nyanya. Tumia mbolea kiasi cha kilo 140 za SA au CAN kwa hekta hasa wakati mmea inapotoa matunda ili kupata matunda makubwa na kuvuna kwa muda mrefu (hadi miezi 10).

6.0 MAGONJWA NA WADUDU


Wadudu
• Funza wa vitumba
• Vidukari
• Kidomozi (Leaf miner)

Kudhibiti: Tumia dawa aina ya permethrin
Magonjwa
• Kuoza mizizi
• Mnyauko wa majani
• Batobato
Kudhibiti: Choma nyasi kwenye kitalu kabla ya kusia mbegu.
Badilisha mazao yasiyo ya jamii ya pilipili.

7.0 UVUNAJI
Matunda ya kwanza huwa tayari kuvunwa kuanzia miezi 2-3 baada ya kupandikizwa; matunda yaliyokomaa vizuri na kuwa na rangi nyekundu ndiyo huvunwa. Matunda 30-80 hupatikana kwa mmea mmoja.
Ubora wa hoho huongezeka kutegemeana na kiwango cha rangi yake ikiwa ni nyekundu njano au kijani. Mazao kiasi cha tani 3.5 kwa hekta hupatikana. Baada ya kuvuna mwagilia maji, piga dawa (kama ni muhimu) na weka mbolea kuongeza uzalishaji unaofuata.

8.0 USINDIKAJI

Hoho huuzwa ikiwa bado fresh tofauti na jamii nyingine za pilipili ambazo zinaweza kukaushwa na kusindikwa kasha kuuzwa baadae.





9.0 SOKO LA PAPRIKA
Soko la hoho lipo nchi nzima kwenya masoko makubwa na hata magengeni, hoho hutumiwa zaidi kama kiungo cha kupikia mapishi mbali mbali au kutia kwenye kachumbari. Tatizo kubwa wanalokabiliana nalo wakulima ni kutokuwa na soko la uhakika ndani na nje ya nchi, mazao huweza kuoza shambani au njiani kutokana na tabu ya usafiri hasa vijijini ambapo mvua zikinyesha barabara hazipitiki kwa urahisi

Kuna aina ya pilipili isiyo kali kama hoho lakini ni ndefu kama pilipili za kawaida ijulikanayo kama PAPRIKA ambayo ina soko kubwa nje ya nchi. Zao hili kwa sasa huzalishwa kwa msukumo wa kampuni ya kigeni ya Hispania inayoitwa Tanzania Spices Ltd iliyopo mkoani Iringa



10.0 GHARAMA YA UZALISHAJI WA HEKTA MOJA:

Mbegu Tshs. 24,000 /-
Vibarua 200,000/-
Mbolea(mboji/samadi) 300,000/-
Madawa 100,000/-
Jumla 624,000/-

MAPATO:
Kilo 3,500/- X 800/- 2,800,000/-

Wednesday, November 24, 2010

MATAPELI WA SAMAKI WA UREMBO

Kumekuwa na baadhi ya watu ambao huwatapeli baadhi ya watu kwa kuwauzia samaki wa baharini na kuwaambia kwamba niwa maji baridi, wanachofanya ni kuwavua samaki wa maji chumvi toka baharini, na kisha kuwaweka kwenye chombo kizuri chenye maji baridi yasiyo na chumvi, wakiwa humo huweza kushi hata zaidi ya masaa 12 na ndipo huanza kuishiwa nguvu na baadae kufa.

Kwa kawaida samaki wa baharini ni wazuri zaidi ya wale wa maji baridi, na hii ndio huwavutia zaidi watu wasio na uelewa wa samaki wa urembo na kuwa nunua, kwa kawaida matapeli hawa utawakuta kwenye makutano ya barabara kubwa na huuza samaki hawa kwa wenye magari wakati wa foleni kubwa za jioni, na wakisha kuuzia kesho huama eneo hilo na kuamia lingine maana wanajua kwamba utawatafuta

Huyu niliyemnasa kwenye video hii alikuwa kwenye mataa ya Ubungo, mimi nilikuwa natokea mwenge kuelekea maeneo ya Ilala

Thursday, November 18, 2010

KILIMO BORA CHA MAEMBE




Maembe hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Tabora, Pwani, Mtwara, Tanga, Mwanza, Morogoro na Mbeya. Uzalishaji wake ni wastani wa tani 159,472 kwa mwaka. Maembe ni zao muhimu la biashara na chakula.

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI
Ili kupata mazao bora ni muhimu kuzingatia kanuni bora za kilimo cha maembe hasa kanuni
zifuatazo:
Kuchagua aina bora ya kupanda kulingana na mahitaji ya soko.
Panda umbali wa mita 10 kwa kumi kama utatumia miembe ya kuunga, hii ni kwa sababu haiwi mikubwa sana kwa sababu haiishi miaka mingi, kwa ile ambayo si ya kuunga panda umbali wa mita 15 kwa 15 kwa kila mti mmoja wa muembe

DHIBITI MAGONJWA, WADUDU, NA MAGUGU

• Fanya ukaguzi wa shamba mara kwa mara ili uweze kudhibiti wadudu na magonjwa ya matunda kabla madhara hayajawa makubwa

UGONJWA WA KUTU KWENYE MAJANI



• Ni muhimu kudhibiti wadudu, magonjwa na magugu ili kupata mazao bora ambayo yatapata soko zuri na kuweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
• Hakikisha shamba ni safi wakati wote ili kupata matunda bora na kurahisisha uvunaji.

MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA

Kusafisha shamba pamoja na barabara za shamba
• Safisha shamba ili kurahisisha uvunaji na usafirishaji shambani.
Kukagua shamba kuona maembe kama yamekomaa Maembe hukomaa katika kipindi cha miezi 4 hadi-6 tangu kutoa maua kutegemea hali ya hewa na aina.

DALILI ZA MAEMBE YALIYOKOMAA

• Maembe hung’ara
• Kwa aina nyingine rangi ya kijani hufifia na kuanza kubadilika kuwa ya manjano.

ANDAA VIFAA VYA KUBEBEA, SEHEMU YA KUFUNGASHIA NA USAFIRI.


VIFAA VYA KUBEBEA
• Ngazi
• Vikapu
• Mifuko
• Ndoo
• Vichumio

VIFAA VYA KUFUNGASHIA
• Makasha ya mbao/plastiki na ya makaratasi magumu na matenga

VYOMBO VYA KUSAFIRISHIA
• Matoroli
• Magari
• Baiskeli
• Matela ya matrekta

KUVUNA
Njia bora ya kuvuna maembe ni Kuchuma kwa mkono
• Kwa miembe mifupi chuma maembe pamoja na kikonyo chake
• Kwa miembe mirefu chuma kwa kutumia kichumio maalumu

KICHUMIO MAALUM


• Acha kikonyo chenye urefu wa sentimita tatu hadi nne ili kuzuia madoa ya utomvu. Utomvu huchafua matunda na hushusha ubora. Pia embe lililovunwa bila kikonyo chake huingiliwa na vimelea vya ugonjwa kwa urahisi.
• Vuna wakati wa asubuhi au jioni ili kuepuka jua kali linaloweza kubabua matunda.
• Wakati wa kuvuna hakikisha maembe hayadondoshwi chini, ili kuepuka kuchubuka kwa matunda ama kupondeka hasa yale yaliyoiva barabara. Aidha beba matunda kwa vikapu au mifuko na kusanya kwenye kivuli.



KUCHAMBUA MAEMBE
Kuchambua ni kutenga matunda yaliyooza, kupasuka, yenye dalili za magonjwa au kubonyea, ili kupata matunda yenye ubora kwa ajili ya matumizi, kusindika au kuuza.
• Matunda yaliyooza na yenye wadudu ni vyema yafukiwe ili kuzuia kuenea kwa wadudu waharibifu na vimelea vya magonjwa.
• Matunda yaliyopasuka, kubonyea , kuchubuka kidogo wakati wa kuvuna au kuiva sana yatumike haraka kwa chakula.
• Matunda mazuri ambayo hayajapata madhara yoyote yatunzwe kwa ajili ya kusindikwa, kutumika au kuuzwa.

KUSAFISHA MAEMBE
• Baada ya kuchambua, safisha matunda kwa maji safi ili kuondoa uchafu na mabaki ya madawa.
• Maembe yanayokusudiwa kuuzwa nje ya nchi hunyunyiziwa nta ili kuzuia kunyauka na kudumisha ubora.
• Baada ya kusafisha tumbukiza maembe kwenye maji yenye nyuzi joto zipatazo 52 za Sentigredi kwa muda wa dakika tano. Maji haya pia yanaweza kuchanganywa na madawa ya klorini asilimia 1 ili kuzuia magonjwa ya ukungu.

KUPANGA MADARAJA
Madaraja hupangwa kwa lengo la kurahisisha ufungashaji, usafirishaji na uuzaji. Madaraja hupangwa kulingana na ubora, ukubwa , aina rangi na uivaji.


KUFUNGASHA MAEMBE

Ufungashaji hufanyika katika sehemu safi na yenye kivuli. Ufungashaji wa kujaza kupita kiasi husababisha upotevu wa maembe. Aidha ubora hushuka kutokana na kuminyana na kubonyea kwa matunda wakati wa kusafirisha

TENGA LA KUFUNGASHIA MAEMBE



Inashauriwa kufungasha kwenye makasha ya mbao/ plastiki , makaratasi magumu au tenga kwa sababu zifuatazo:
• Matunda yanaweza kupangwa na kusafirishwa bila kuchubuka, kubonyea au kupasuka.
• Huweza kupakiwa na kupakuliwa kwenye chombo cha usafiri kwa urahisi.

Wakati wa ufungashaji ni muhimu kuzingatia yafuatayo:
• Kasha moja lisizidi uzito wa kilo 20 ili kurahisisha ubebaji.
• Makasha yawe imara na yenye matundu ya kutosha ili kuruhusu mzunguko wa hewa.
• Ni muhimu kutanguliza vitu vilivyo safi ndani ya vifungashio ili kuzuia michubuko na mipasuko ya matunda wakati wa kusafirisha.
• Maembe yapangwe kwa kubananisha na kwa kuhakikisha kuwa vikonyo havitoboi matunda na kusababisha majeraha wakati wa kusafirisha. Kubananisha matunda husaidia kuzuia mgongano unaoweza kusababisha matunda kusambaratika na hivyo kubonyea au kupasuka wakati wa kusafirisha.

KUSAFIRISHA

Ili kuepuka upotevu na uharibifu wakati wa kusafirisha, ni muhimu maembe yapangwe kwenye vyombo vya kufungashia na kusafirisha kwa uangalifu, ndani ya matela, mikokoteni na magari. Epuka kutupa matunda wakati wa kupakia na kupakua. Wakati wa kupanga mazao katika vyombo vya usafiri yasirundikwe ovyo na yasijazwe kupita kiasi ili yasimwagike. Vilevile yafunikwe ili yasipigwe na jua. Jua huongeza kasi ya kuoza. Matunda yakipigwa na jua kwa muda wa saa mbili mfululizo husababisha kuoza kwa asilimia 100.

KUHIFADHI

• Maembe huweza kuhifadhiwa kwenye chumba chenye hali ya hewa yenye joto la nyuzi 8 hadi 10 za Sentigredi na unyevu wa asilimia 85 hadi 90. Katika hali hiyo, maembe yanaweza kuhifadhiwa bila kuharibika kwa mwezi mmoja.
• Kagua mara kwa mara ili kugundua uharibifu unaoweza kutokea

Saturday, October 9, 2010

KITUO CHA KUZALISHA NA KUFUGA SAMAKI KINGOLWIRA - MOROGORO



MSAIDIZI WA BWANA KALINGA akiwalisha kambale kwenye bwawa la kufugia








BUSTANI ya mipapai, maji yakitolewa kwenye mabwawa hutumika kumwagilia bustani hii


BATA akiogelea na kusaidia mzunguko wa oksijen kwenye maji


BWAWA lililochimbwa tayari kwa matumizi, mabanda ya bata na kuku yakiwa pembeni tayari


TANKI LIKIJENGWA


TANKI LA KULELEA VIFARANGA VYA SAMAKI


MTAALAMU BWANA KALINGA AKINIPA MAELEZO


MTAMBO WA KUTOTOLESHEA MAYAI YA KAMBALE MAABARA






MASHINE YA KUSAGIA CHAKULA CHA SAMAKI


CHAKULA CHA SAMAKI


KWA MAWASILIANO NA BW KALINGA
0757891761 au 0787596798
BEI YA KIFARANGA CHA SAMAKI NI KATI YA SHILINGI 30 - 50 KUTEGEMEA UKUBWA

KITUO CHA KUFUGIA SAMAKI MOROGORO MJINI BOMA ROAD

Nilibahatika kutembelea vituo vya ufugaji na uzalishaji wa samaki huko Morogoro mjini barabara ya boma na Kingolwira, mwenyeji wangu alikuwa ni Bwana Melton Kalinga ambapo tulishinda karibia kutwa nzima akinionyesha vitu mbali mbali huku tukibadilishana uzoefu na utaalamu wa kuzalisha samaki, wakati yeye alikuwa akinifundisha namna ya kuzalisha Sato na Kambale, mimi nilimfundisha namna ya kuzalisha samaki wa mapambo hasa Gold fish na Angels

HAPA NI MOROGORO MJINI BOMA ROAD kwenye kituo cha kufugia samaki, kuna mabwawa ambapo samki hufugwa baada ya kuzalishwa katika kituo cha Kingolwira


CHANZO CHA MAJI ni kutoka katika kisima cha kuchimbwa na maji huvutwa kwa pampu ya umeme





BANDA LA BATA kinyesi chao chakula cha samaki, pia wakiogelea husaidia kuingiza hewa kwenye bwawa (aeration)


SEHEMU YA KUWEKEA CHAKULA CHA SAMAKI sehemu hii imejengwa kwa kutumia miti na inahamishika


SEHEMU YA KUWEKEA CHAKULA CHA SAMAKI imejengwa kwa saruji, ni sehemu ya kudumu


BATA pia hufukuza ndege wanaokula samaki na kuwala vyura wala samaki


NDEGE MLA SAMAKI naye alikuwepo

Monday, September 27, 2010

SIKU YA KICHAA CHA MBWA DUNIANI

Kila mwaka tarehe 28 ya mwezi wa tisa (september) ni siku ya kichaa cha mbwa duniani, hapa nchini serekali katika kampeni ya siku hii maalum imetoa kiasi cha chanjo 100,000 bure kwa mafugaji mbwa katika mikoa ta Dar es salaam, Mtwara, Lindi na Pemba

kutokana na takwimu za wizara ya mifugo na uvuvi inaonyesha mwaka jana watu 21,000 walingatwa na mbwa nchini Tanzania. Kati ya hao watu 51 walifariki dunia kwa sababu ya kichaa cha mbwa.

Ingawa kwa kiswahili ugonjwa huu unaitwa kichaa cha mbwa, lakini ukweli hushambulia hata wanyama wengine kama paka, ng'ombe, mbuzi, kondoo na hata binadamu, Ugonjwa huu kwa wanyama hauna dawa ila kinga tu kwanjia ya chanjo

Kuuelewa zaidi ugonjwa huu soma hapa
http://mitiki.blogspot.com/2009/08/kichaa-cha-mbwa.html

Thursday, September 23, 2010

DADA NAYMA ANAOMBA USHAURI ZAIDI

Hello Bro Bennet. Angalia miche yangu hatua iliyofikia bado sijaipeleka shambani,
naomba ushauri zaidi niliiotesha mwezi wa tano mwezi wa saba nikaiweka kwenye mifuko miche 300 tu.
nayma





Dada Nayma leo naomba nikuweke hadharani, wadau huyu dada nimekuwa nikimshauri kuanzia kuandaa mbegu, kitalu, kusia mbegu, umwagiliaji, kuhamisha mbegu kutoka kwenye kitalu hadi kwenye vipakti

Dada Nayma miche yako bado ni michanga kiasi, na kama unafuatilia utabiri wa mvua za msimu wa September mpaka November ni kwamba hakutakuwa na mvua za kutosha ila kwa mikoa ya kanda ya ziwa na zaidi Bukoba, nakushauri endelea kumwagilia miche yako ikue zaidi huku ukisubiri mvua za mwezi wa December mwishoni na January 2011, hapo itakuwa mikubwa ya kuweza kuhimili kama mvua zitakuwa chache

NB Hongera sana na anza kuandaa mbegu nyingine ili mwezi wa January uwe na miche mingi zaidi

KILA KAZI NA HATARI ZAKE

Leo nilikuwa nimekwenda kutibu mbwa 9 katika kampuni ya usafirishaji ijulikanayo kama Ruvuvu transport huko kurasini, mbwa hao walikuwa wanasumbuliwa na ugonjwa wa minyoo ya kwenye ngozi ujulikanao kama MANGE, ugonjwa huu husambazwa na viroboto wa mbwa


HAPA MBWA ANAANDALIWA



KUCHOMA SINDANO MBWA

Friday, September 17, 2010

SHARK - MKEMIA WA MAJI

Leo nilikuwa nabadili maji kwenye chombo cha kufugia samaki wa urembo (aquarium)baada ya kuweka maji masafi na kuwarudisha samaki wangu kuna kitu nikakigundua. Pamoja ya kwamba samaki wote ni wa urembo lakini kila mmoja anatabia yake, ni samaki wawili aina ya shark ambao wanauwezo wa kutambua maji kama yana kitu chochote kibaya, kwa mfano kama kemikali yoyote, chumvi au madini yoyote yale zaidi ya kiwango cha kawaida. Mara tu utakapowaweka kwenye maji ambayo hayako sawa basi utawaona wanakaa chini tu na wala hawaogelei kama kawaida yao.

Wakati narudishia mawe kwenye chombo chao yalisuguana na chenga chenga zake zikabadili ubora wa maji, ingawa hayakuwa na tatizo lolote kiafya lakini samaki hawa aina ya shark waliweza kugundua hilo na walikaa kama wanavyoonekana hapa kwenye picha mmoja aligeuka juu chini kama vile kafa.







Baada ya kuona wako hivo nikawasha pampu ya kuongeza hewa kwenye maji pamoja na filter baada ya dakika kama 10 samaki hao wakaanza kuogelea kama kawaida, angalia video hii


Hawa hapa kwenye video ni goldfish aina ya shubunkin, redcap na goldspike


Angel fish ni aina nyingine ya samaki nilionao


Huyu anajulikana kama catfish, nayeye kazi yake kubwa ni kisafisha vioo na urembo wa ndani, anauwezo pia wa kumla samaki yoyote aliyekufa bila ya wewe kuanza kuhangaika kumtoa