KURASA

Friday, March 28, 2014

TOGGENBURG - AINA BORA YA MBUZI WA MAZIWA


Hii ni aina ya mbuzi wa maziwa ambao asili yake ni uswizi katika eneo la Obertoggenburg kama wanavyoitwa, hii ndio mbegu ya mbuzi wa maziwa wa zamani zaidi kuliko zote. Kwa hapa Tanzania wanapatikana Uyole, SUA na Tengeru (hivi vyote ni vyuo vya mifugo)

UZALISHAJI
Mbuzi hawa wanauwezo wa kuzalisha maziwa wastani wa lita mbili kwa siku au zaidi, hawatoi maziwa mengi kama Saanen ila maziwa yao yana kiasi cha mafuta kati ya 3% - 4%

MAUMBILE
Mbuzi hawa wana umbile la wastani lakini ni wakubwa kuliko mbuzi wa kienyeji, kilo 55 kwa majike na kilo 75 kwa madume, wana rangi ya kahawia (khaki) mpaka hudhurungi (brown)  pia wana mistari miwili usni yenye rangi ya maziwa au nyeupe kuanzia juu mpaka kwenye pua (kama duma) huwa na viwele (udder) vikubwa na pia ni wazazi na walezi wazuri, mara nyingi huweza kuzaa mapacha 

HALI YA HEWA
Mbuzi hawa hawawezi kuhimili hali ya joto, bali hufanya vizuri kwenye maeneo yanye baridi kama mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Njombe, Dodoma, Singida n.k. Wanahitaji chakula chakutosha ili kutoa maziwa mengi, pia chakula kiwe na virutubisho kamili. Ingawa pia wanaweza kuchungwa kwenye maeneo yenye ukame kiasi na wakaweza kufanya vizuri (good foragers)

TABIA
Mbuzi hawa huishi kwa makundi wakitoroka au kuingia kwenye shamba la mazao basi huenda wote na hufundishika kirahisi sana hii husababisha urahisi wa kuwafundisha kukamuliwa na mashine

FAYC KAY TRADING LTD - WAUZAJI WA MATREKTA NA ZANA ZA KILIMO


Hawa ni wajasiliamali wa kiTanzania waishio nchini Denmark, wanauza zana za kilimo zilizotumika (used) kama matrekta na majembe yake, matrailer, irrigation water pumps, Chemicals sprayer, harrows, planters, combining harvesters n.k


Unaweza kuwasiliana nao kwa namba zifuatazo wakiwa Denmark 0004560248586 au 0004527201580 unaweza kuwapigia au kwa kutumia whats up. pia wana email zifuatazo charlesurban00@hotmail.com au sweetfaydat@gmail.comWanazo brand za kimataifa zenye ubora wa hali ya juu kama Massey Ferguson, John Deere, New Holland, Ford na nyinginezi nyingi


Wednesday, March 26, 2014

KILIMO BORA CHA MDALASINI - CINNAMON


Mti wa mita 10 au zaidi. Hutoa machipukizi na kuota miti zaidi ya mmoja kwenye shina moja na kuongeza mavuno mengi, haya mashina mapya yasing'olewe bali yaachwe yakue na kuwa mti mkubwa.

AINA
Mchanganyiko; za kienyeji (ndogo) na za kigeni ( kubwa)

HALI YA HEWA NA UDONGO
· Mvua nyingi za kutosha 2000mm -2500mm kwa mwaka
· Udongo wenye rutuba
· Joto kwa wingi
· Hewa yenye unyevunyevu

KUSIA MBEGU KWENYE VITALU
· Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa
· Sia mbegu kwenye kitalu zikiwa nusu sentimeta chini ya udongo
· Baada ya kuchipua, mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani
· Panda miche wakati wa masika
· Panda kwa nafasi ya 2m x2m. Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi. Nafasi kubwa hufanya miti kuwa na matawi mengi pia mashina hayanenepi wala kurefuka

UTUNZAJI
· Acha machipukizi kwenye shina
· Toa matawi kwenye mashina ili kunenepesha mashina
· Weka shamba katika hali ya safi
· Zuia magonjwa kama.
- Vinundu (galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scales na mealbugs kwa kutumia dawa za sumu kama Selecron, Karate nk.

KUVUNA
· Anza kuvuna miaka 3 baada ya kupanda
· Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya miti
· Kata shina la mti,na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya
· Kuwa mwangalifu ili ganda litoke vizuri bila kupasukapasuka
· Seli za nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukaruza kwa kisu
· Kausha vizuri siyo kwenye jua kali Mavuno
· 0.25 kg – 10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja. Kiasi cha mazao hutegemea ukubwa na umri wa mti
· Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na umri wa mti. Mti wa umri mkubwa hutoa mganda yenye ubora wa chini

MATUMIZI
Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa umesagwa au bila kusagwa hutumika kama:
· Kiungo kwenye chakula na vitafunwa kama keki, mandazi,vitumbua
· Vikolezo kwenye vinjwaji km. chai, kahawa
· Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya chakula
· Dawa ya ngozi

JINSI YA KUTUMIA
· kiungo kwenye chakula
Tumia maganda au saga magada yaliyokauka. Tumia ili kuongeza ladha kwenye vyakula kama pilau, ndizi, mchuzi nk
· Kutengenezea kinywaji
Weka vipanda vichache 2-3 (30gm) vya maganda kwenye kikombe ongeza maji yanayochemka, funika kwa dakika 15, ongeza vipande vya limao. Kunywa kila baada ya kula

MANUFAA
· Miti hudumu shambani zaidi ya miaka 20. Miti huchipua na kutoa machipukizi mengine kila baada ya kuvuna
· Gharama ndogo ya uzalishaji
· Mazao yaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu
· Magonjwa na wadudu ni kidogo
· Rahisi kuchanganya na mazao mengine
· Nguvu kidogo, kipato kikubwa.