KURASA

Wednesday, September 28, 2011

LEO NI SIKU YA KICHAA CHA MBWA DUNIANI -

Wakati leo tunaazimisha siku ya kichaa cha mbwa duniani, ugonjwa huu hapa nchini kwetu bado umekuwa tatizo sugu. Katika wilaya ya Temeke pekee watu 202 waling'atwa na kati ya hao 19 waliugua kichaa cha mbwa. Wilaya hii inajumla ya mbwa 4500, paka 1500 ambapo kati ya hao 3418 walifanikiwa kuchanjwa.

CHANJO YA KICHAA CHA MBWA (RABIES) KWA AJILI YA WANYAMA


Ugonjwa huu huweza kumpata viumbe vingi ikiwemo binadamu, ng'ombe, mbuzi, kondoo na kadhalika, na wasmbazaji wakuu wakiwa mbwa na paka ingwa kuna baadhi ya poo (vampire bats) nao pia husambaza ugonjwa huu kwa kung'ata na kusambaza vimelea vya kichaa cha mbwa.

ugonjwa huu upo kila sehemu ya dunia ambapo kwa mwaka huua jumla ya watu 55,000 kote duniani ambapo Afrika watu 21,000 hufa kila mwana na wengine 34,000 hufa barani Asia na kwingineko

Kauli mbiu ya mwaka huu ni TUSHIRIKIANE KUFANYA KICHAA CHA MBWA KUWA HISTORIA na njia pekee ni kuwachanja wanyama wetu, na pia kuwazuia wasizurure hovyo mitaani, MUONE MTAALAM WA MIFUGO ALIYE KARIBU NAWE ILI MBWA NA PAKA WAKO WAPATE CHANJO KAMILI

WILAYA ZA NGORONGORO NA LONGIDO ZAKUMBWA NA UGONJWA HATARI WA HOMA YA MAPAFU YA NGOMBE



Wilaya za Ngorongoro na Longido ambazo zipo mpakani na Kenya zimekumbwa na ugonjwa wa mapafu wa ng'ombe, hali hii imefanya jumla ya ng'ombe milioni moja (1,000,000) kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huu.

Ugonjwa huu ulitangazwa kama janga la kitaifa mnamo mwaka 2001 kwa sababau ni hatari sana na unaua ng'ombe kwa kasi sana, na unaweza kudhibitiwa kwa kuchanja mifugo mara unapoonyesha dalili za mlipuko.

Kutokana na hilo serekali imechukua hatua za dharura za kuwachanja ng'ombe wote katika wilaya ya Ngorongoro, Longido na zile za jirani kama Karatu na nyinginezo.

Historia ya ugonjwa huu inaanzia enzi za ukoloni mnamo mwaka 1905 na uliweza kudhibitiwa, lakini mnamo mwaka 1964 mwaka ambao ndio wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitokea na Tanzania kuzaliwa, ugonjwa huu ulilipuka tena nchini mwetu. mnamo mwaka 1990 ugonjwa huu ulilipuka tena katika Wilaya ya Loliondo mpakani na Kenya.



Mwaka 1994 ugonjwa huu ulilipuka tena na kusambaa hadi mkoa wa Morogoro katika wilaya za kilosa na Mahenge. na mwaka 1998 ugonjwa huu ulisambaa katika mikoa 11 ya nchi yetu

Ugonjwa huu hujulikana kama contagious bovine pleural pneumonia au CBPP kwa kifupi na kama unataka mifugo yako ichanjwe wasiliana na maofisa ugani waliokaribu nawe au ofisi za wizara ya mifugo