KURASA

Tuesday, August 28, 2012

CANINE PARVOVIRUS

Kama jina lake lilivyo ungonjwa huu husababishwa na virusi ambavyo huwaathiri mbwa ka kiasi kikubwa, ugonjwa huu uligundulika miaka ya 1970 na hushambulia zaid seli za kwenye mfumo wa chakula na hewa. virusi vya ugonjwa huu huwa vingi sana kwenye kinyesi cha mbwa mgonjwa na  husambaa baada ya mbwa kugusa kinyesi che nye vidudu kwa mdomo wake, huweza pia kubeba virusi hivi kama atavilalia au kukanyaga kinyesi cha mbwa mwenye ugonjwa huu, na mbwa anaweza pia kuambukizwa ikiwa atagusa kitu chochote ambacho kiligusana na kinyesi chenye vidudu vya parvo.


DOBERMAN PINSCHER

Ugonjwa hushambulia mbwa wa umri wowote lakini watoto wenye umri kati ya wiki 6 - 20 hushambuliwa zaidi na pia mbwa aina ya Doberman Pinschers and Rottweilers hushambuliwa zaidi ya mbwa wengine ha dalili za ugonjwa huu huonekana kirahisi kwao.


ROTTWEILER

Dalili za kwanza huonekana baada ya siku kama 5 ambazo ni kuharisha, kutapika na joto kupanda sana ingawa si mbwa wote ambao watapandisha joto, watoto wataonyesha dalili za kusumbuliwa na maumivu ya tumbo, pia kinyesi hutoka na malenda malenda ambayo wakati mwingine huwa na damu damu kiasi na kwa wataalamu wa mifugo kipimo cha ELISA huweza kutumika kupima na kugundua virusi vya ugnjwa huu

MATIBABU
Hakuna matibabu ya ugonjwa huu ila drip za maji husaidia kurudisha maji yaliyopotea na kumpa nafuu mgonjwa, dawa za kuzuia kuharisha na kutapika ni muhimu na pia wakati mwingine mbwa anaweza kuhitaji kuongezewa damu, antibaiotiks pia ni muhimu kuzuia maambukizi ya bakteria

Kupona kwa mbwa kutategemea vitu vingi kama ukoo wa virusi vya ugonjwa, hatua za maambukizi, uwezo wa mwili wa mbwa kupambana na magonjwa na umri wa mbwa hata uharaka wa kuapata tiba kwa mbwa

KINGA
Kinga kubwa ni chanjo ya DHPP (distemper, hepatitis, parvovirus, and parainfluenza combination)ambayo hupigwa katika umri wa wiki 8 tangu kuzaliwa na kurudiwa baada ya wiki 16 lakini kama wazazi hawakuchanjwa basi ni muhimu kuchanja katika wiki ya 4, usafi wa mabanda pia ni muhimu lakini ukitumia blichi kiasi cha 1:30 katika uchanganyaji na maji ukisafisha na kuiacha kwa zaidi ya dakika 20 kabla ya kuiosha na maji

CANINE DISTEMPER - UGONJWA HATARI WA MBWA

Huu  ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyofanana sana na vile vinavyosababisha surua kwa binandamu, distemper hushambulia wanyama jamii ya mbwa (canine) kana simba, mbwa mwitu, fisi, mbweha na mbwa wa kawaida tunaowafua majumbani mwetu. Huu no ugonjwa unaoua zaidi mbwa duniani ingawa hapa nchini haujasababisha madhara makubwa kama kichaa cha mbwa (rabies)


Mbwa aliambukizwa ugonjwa huu hutoa virusi hivi kwa njia ya kinyesi, mkojo, mafua na chafya na njia ya hewa ndio njia kuu ya kusambaza ugonjwa huu kwenda kwa mbwa wengine. Maabukizi makubwa zaidi ni kwenye watoto wasiochanjwa ambao wenye umri kati ya wiki 6 - 12 ambapo kinga toka kwa mama waliyozaliwa nayo hupungua sana na kuwa katika hatari zaidi ya maambukizi.

Mbwa walioambukizwa ugonjwa huu nusu yao wataonyesha dalili kidogo sana au wasionyeshe dalili za ugonjwa huu kabisa na wanaoathirika zaidi ni mbwa ambao hawapati lishe bora na kuwekwa kwenye mazingira mazuri na afya kwa ujumla.Virusi vya ugonjwa huu hushambulia ubongo, sehemu za ndani ya ngozi, macho na utando wa mfumo wa hewa na chakula na dalili za wazi huweza kuonekana baada ya siku 6 - 9 tangu kupata maambukizi

Hatua ya kwanza ya ugonjwa huu joto hupanda kufikia sentigredi 39.4 - 40.5 mbwa hupoteza hamu ya kula, hutoa machozi na majimaji puani, lakini dalili hizi ni kama za ugonjwa wa kawaida wa mafua (colds) kwenye mbwa kwa hiyo zinaweza kukuchanganya kidogo. baada ya siku chache macho huwa na matongo tongo na sio machozi tena na puani atatoa makamasi mazito na sio majimaji tena, mbwa huwa na kikohozi kikavu, hutapika, kuharisha na hii husababisha upungufu wa maji mwilini. ndani ya wiki moja au zaidi mbwa ataonekana kupata nafuu na hii hutokea zaidi kwa mbwa waliotibiwa na dawa za antibaiotiki kama OTC  na Gentamycin, lakini hali hubadilika baada ya mashambulizi ya juu kutokea kwenye njia ya hewa na mfumo wa chakula

Hatua ya pili ni baada ya wiki mbili au tatu mbwa wengi wataonyesha dalili za magonjwa ya akili, kushambulia ghafla, kutingisha kichwa, kutafuna kama vile anatafuna bazoka/chewing gum, kukimbia kwa kujizungusha mduara na kuanguka chini, kupiga mateke miguu yote minne, kuona aibu na wakati mwingine anakua haoni vitu vizuri sababu ya kushambuliwa macho. Dalili nyingine ni kuvimba kwa pua na nyayo za mbwa ingawa hii haitokei sana

MATIBABU
Matibabu yanakuwa ya uhakika zaidi kama mbwa atatibiwa mapema wakati wa dalili za mwanzo kabisa, antibaiotiks husaidia sana kupunguza mashambulizi ya juu (secondary infections) ingawa hazitaua virusi vinavyosababisha ugonjwa huu, Mbwa pia watahitaji drip ya maji ili kufidia upungufu mkubwa wa maji uliosababishwa na kutapika/kuharisha, pia apewe dawa za kuzuia kuharisha na kutapika pamoja na dawa za usingizi ili apumzishe ubongo wake vya kutoshaKINGA
Hii ndio njia sahihi ya kupambana na ugonjwa huu, siku hizi kuna chanjo moja kwa ajili ya magonjwa manne DHPP (distemper, hepatitis, parvovirus, and parainfluenza combination) ambapo chanjo hii wapigwe watoto wa mbwa kabla ya kufikisha wiki 8 toka wazaliwe au wapigwe kabla kama mama yao hakuchanjwa kabisa