KURASA

Thursday, December 19, 2013

NDIKANA KALI - EAST COAST FEVER

Ugonjwa huu hushambulia wanyama kama ng'ombe, mbuzi na kondoo na husababishwa na vimelea vijulikanavyo kama Theileria parva ambavyo vusambazwa na kupe wekundu wa kwenye masikio wajulikanavyo kama Rhepicephalus Appendiculatus, ugonjwa huu usipodhibitiwa unaweza kusababisha vifo vya wanyama wengi sana na pia ni aghali kuutibu kulinganisha na magonjwa mengine


KUPE WEKUNDU KWENYE MASIKIO YA NG'OMBE

DALILI ZA UGONJWA HUU
Homa kali, mnyama kushindwa kupumua vizuri,  kukohoa pamoja na kutoa makamasi, kuharisha na kuvimba matezi

MATIBABU
Mnyama inabidi apigwe sindano ya dawa za  PARVAQUONE au BUTALEX kiasi cha ml 20 (soma kimbatanisho cha dawa kwa maelezo zaidi) na kurudia baada  ya siku moja kupita, yaani ukuchoma leo unarudia dozi kesho kutwa, pia mnyama achomwe dawa ya OTC20% kipindi chote cha matibabu



KINGA
Kinga kubwa ya ugonjwa huu ni kuhakikisha kwamba mifugo yako inaoga mara kwa mara kwenye majosho au kwa kuwanyunyuzia dawa za kuua wadudu wa mifugo

NG'OMBE WAKIOGESHWA KWENYE DAWA

KUPUNGUZIA MATAWI MITI YA MITIKI - PRUNING TEAK TREES

 

Umuhimu wa zoezi hili ni kuhakkisha miti yako inanyooka, kukua kwa haraka na kuwa na mbao bora, miti inapokuwa na matawi haikui kwa haraka maana chakula kinagawanywa pamoja na matawi, lakini kama mti hauna matawi mengi basi hunenepa na kurefuka kwa haraka, pia kwa kuondoa matawi yakiwa machanga unoaongeza ubora wa mbao maana hazitakuwa na vidonda vinavyo sababishwa na matawi