KURASA

Sunday, June 26, 2011

LINDI - MTWARA

NYAMWAGE - MUHORO


MIKINDANI


MABIRIKA YA KUTENGENEZEA CHUMVI - LINDI


BEACH MTWARA


HIKI NDIO KIPANDE AMBACHO HAKINA LAMI KAMA KILOMETA 60

Thursday, June 16, 2011

NDANI YA RUFIJI

CHOMBO KINAKUJAWadau samahanini sana kwa kupotea humu kijiweni, ilikuwa ni lazima nipotee ili vitu vingine viende, lakini sasa nimerudi rasmi kwenye kijiwe changu

Wiki hii nilikuwa wilayani Rufiji nilifika sehemu kama Kibiti, Utete, Ikwiriri, Mkongwa na Nyamwage. Nililala Utete, ni sehemu tulivu na watu wake ni wakarimu kama tulivyo waTanzania wote.

Hali ya utete kwa wakati huu ni joto limepungua sana wala uhitaji kulala na feni kama DSM, kuna mbu wengi sana ni lazima ulalae na chandarua, mji hii uko pembeni ya mto Rufiji
Wakati wa kwenda tulitumia barabara ya Kilwa hadi Kibiti tukakata kulia kama unaelekea hifadhi ya Selous na kufika kijiji cha Mkongwa tukakata kulia na kuelekea kwenye kivuko cha Utete, tukasubiri pantoni baaddae tukavuka na kuingia Utete kama saa 3 asubuhi kwa kupitia njia hii ya mkato tuliokoa mwendo wa kilometa kama 40.

Utete tuliona vitu vingi maana kwanza kuna mto huu wa Rufiji, lakini bado hawajaanza kuutumia kiukamilifu, ila nina imani mambo yatakuwa mazuri maana kuna RUBADA ambayo mamlaka hii imepewa jukumu la kuendeleza bonde la Rufiji.

NAHODHA WA MV UTETE - BWANA ALLI


Wakazi wa Utete ni wakulima wa mazao kama Mpunga, mahindi na shughuli za uvuvi, pia kuna baadhi wanafuga samaki katika mabwawa binafesi ingawa ufugaji wao si mkubwa na si wakitaalam zaidi

TAA ZA BARABARANI - uswazi kwetu hamna hizi


Mji wa Utete una huduma za simu mitandao ya Voda, tigo , Airtel na Zantel, pia kuna umeme na taa mpaka za barabarani ingawa barabara hazina lami, mji una maji ya bomba lakini cha kuchekesha chanzo ni kisima waka mji unapitiwa na mto hapo hapo, maji ni ya chumvi

URITHI WETUUsafiri ni wa mabasi mawili kwa siku moja saa 12 asubuhi na lapili kwenye saa 6 mchana ukiyakosa hayo, omba lifti kwenye magari madogo madogo ya Serekali au Binafsi au sivyo utalala.

WATAALAMU WA USHAURI KWENYE NYANJA ZOTE


Huduma nyingine ni Hospitali ndogo, pia kuna Magereza, kuna BOma lililojengwa na mkoloni linalotumika kama Ofisi ya Wilaya, Kuna posta, Nyumba za kulala wageni, sehemu za vinywaji, soko, na maduka ya bidhaa mbali mbali.

CHEMCHEM YA MAJI MOTO


Ukifika Utete ulizia wakulete huku, kwa pikipiki ni buku tu unalipia, wenyeji wanaamini maji haya ni yamaajabu na yanaweza kuytibu magonjwa, niliogopa kuwaambia hii ni volcanic feature

USAFIRI TOKA VIJIJI VINGINE KUJA UTETE


MAPATO NI MUHIMU


EWURA WAKIJA HUKU NI BALAA- PETROL INAUZWA KWENYE HIVYO VIDUMUNILIUKUTA MTIKI IKABIDI NIUHUGMKONGWA

KILMO KWANZA

Friday, June 10, 2011

KAJUMULO WORLD SOCCER TANZANIA LTD REGIONAL MANAGER - JOB DESCRIPTIONHI FELLOW TANZANIANS,

THANKS FOR THE OVERWHELMING RESPONSE. HERE IS A SHORT DESCRIPTION OF THE DUTIES AND REQUIREMENTS FOR THE REGIONAL MANAGER POSITIONS. I WILL BE HIRING ONE REGIONAL MANAGER FOR EACH OF THE 22 REGIONS IN TANZANIA.

1. YOU MUST BE RESIDENT FOR AT LEAST ONE YEAR IN THAT REGION. YOU MUST KNOW THE REGION AND BE VERY FAMILIAR WITH IT.
2. YOU MUST BE A UNIVERSITY GRADUATE OR HAVE AT LEAST 3 YEARS OF BUSINESS EXPERIENCE WITH EXCELLENT REFERENCES.
3. YOU MUST SPEAK, READ, AND WRITE ENGLISH FLUENTLY.
4. YOU MUST HAVE A VALID TANZANIA PASSPORT.
5. YOU MUST BE AN ACCOMPLISHED COMPUTER USER, ABLE TO USE THE INTERNET, EMAIL, SOCIAL NETWORKING (LIKE FACEBOOK, TWITTER, ETC) AND MICROSOFT WORD AND EXCEL. EXPERIENCE WITH PHOTOSHOP OR ILLUSTRATOR IS BENEFICIAL.

YOU MUST SEND A PAPER APPLICATION TO THE PO BOX ADDRESS.

DO NOT SEND AN EMAIL. I WILL NOT READ APPLICATIONS SENT BY EMAIL.

SELECTED CANDIDATES WILL TRAVEL TO THE U.S. DURING THE FIRST YEAR OF EMPLOYMENT FOR BUSINESS AND SPORTS MARKETING TRAINING.

MAIL COVER LETTER AND RESUME TO:

KAJUMULO WORLD SOCCER TANZANIA, LTD.
ATTN: HUMAN RESOURCES MANAGER
PO BOX 75935
DAR ES SALAAM TANZANIA


ok and you can you the page www.babukaju.com