KURASA

Friday, April 24, 2009

TANGO-Dawa ya kukausha maziwa mbwa anayenyonyeshaHii le nitaongelea tunda la tango na madhumuni zaidi ni katika kumsaidia mbwa jike kukausha maziwa. Inaweza kutokea mbwa watoto wake wamekua na kuacha kunyonya au watoto wakafariki wakati bado wadogo mara baada ya kuzaliwa, na maziwa yake yasikauke yenyewe ingawa ni mara chache sana.

Maziwa yasipokauka yatamsababishia ugonjwa wa chuchu ujulikanao kama (mastitis)ambao husababisha maziwa kuvimba baada ya kushambuliwa na bakteria, tiba yake huwa ghari kiasi sana na mara chache husababisha vifo kwa mbwa.
Sasa basi kwa njia rahisi ukitaka kuepukana na hali hii inatakubidi kumsaidia mbwa wako kukausha maziwa, katika chakula chake msagie tango moja (1)ambalo limeondolewa maganda nusu na nusu kubakia kwa muda wa siku 3 mpaka 5 au mpaka maziwa yakauke.

BINADAMU
Kwa binadamu tango ni dawa la magonjwa mengi na kinga pia, inashauriwe liliwe likiwa na maganda yake kiasi yaani usimenye maganda yote. magonjwa yanayotibiwa na tango ni KUHARISHA magonjwa mengine ni kama presha ya kupanda na kushuka pia husaidia kurekebisha ngozi ya mwili