KURASA

Tuesday, September 29, 2009

SEHEMU YA 4 - MATUNZO YA WATOTO WA NGURUWE
Kwa kawaida hunyonya kwa wiki 5 -8, na baada ya hapo hutengwa na mama yao na kuanza kupewa chakula chenye protini 25% kwa muda wa wiki 6 za mwanzo

KUKATA MENO
Mara baada ya kuzaliwa watoto wakatwe meno kwa kutumia mkasi mkubwa au kifaa cha kukatia waya (wire cutter) umuhimu wa zoezi hili ni kwa sababu nguruwe huzaliwa na meno na mara wanapoanza kunyonya huumiza chuchu za mama yao na kumsababishia ugonjwa wa chuchu (mastitis)

MADINI CHUMA
Wakizaliwa tu wanahitaji madini ya chuma kwa wingi, maziwa ya mama yanatoa kiasi cha 10% tu, huwa wanapigwa sindano (Iron Injection) kiasi cha 155mg kwa kitoto kimoja ili kuwaongezea madini ya chuma ya ziada, muone mtaalamu wa mifugo akusaidie kwa hiliKUHASI
Madume ambayo yatakuzwa kwa ajili ya nyama ni vizuri yakahasiwa, hii husaidia ukuaji wa haraka na pia huondoa harufu ya balehe, Zoezi hili lifanyike wakati wakiwa na wiki 2-3 inapofika wiki ya 5 zoezi huanza kuwa gumu kwa sababu watoto wanakuwa wakubwa na litahitaji sindano za ganzi, zoezi hili linahitaji mtaalamu wa mifugo.

MINYOO
Mzazi anapokaribia kujifungua wiki ya mwisho achomwe sindano ya kuondoa minyoo na magonjwa ya ngozi ijulikanayo kama IVOMEC SUPER au IVERMECTIN zinazopatikana kote nchini, dawa hii husaidia kuwalinda watoto na minyoo hadi wanapoacha kunyonya ndio na wao wapigwe sindano hii ambayo pia itasaidia kuua minyoo ya mapafu, minyoo ya macho, viroboto na kuondoa ukurutu.CHAKULA
Baada ya wili chache vitoto vitaanza kula chakula kidogo kidogo kwa kuanzia na kile anachopewa mzazi, hakikisha mzazi anapewa chakula kingi na chakutosha kwa sababu atakuwa anakula yeye na watoto wake

KITIMOTO SEHEMU YA 3 - NGURUWE JIKE (MZAZI)

UCHAGUZI
Yawe na chuchu zisizopungua 18 na chuchu ziwe nene na ndefu, chuchu fupi na ndogo huleta matatizo wakati wa kunyonya , kumbuka mtoto wa nguruwe chuchu atakayo nyonya siku ya kwanza ndiyo hiyo hiyo atakayonyinya mpaka atakapoacha kunyonya
Awe na miguu ya wastani yenye nguvu na isiwe na kasoro kama matege au kukaa upande na kucheche mea, hii humsaidia kuhimili madume makubwa
Uke uwe na ukubwa wa kutosha na umbo la kawaida, pia upimwe na mtaalamu kwa kuingiza vidole na kuangalia kama wakati wa kuvitoa vina kwama kwama, hii huwa dalili ya majike dume (hermaphrodites)CHAKULA
Maji yalishwe chakula cha kunenepesha mpaka yakifikisha uzito wa kilo 80, baada ya hapa yapewe chakula maalum cha wazazi ambacho kitasaidia wasinenepeane na kuwa na mafuta mengi kwenye njia ya uzazi

BANDA
Majike hukaa moja moja au mengi kwenye banda moja muda wote (kipimo ni 2.5m *1.5m ) kwa kila nguruwe kasoro tu yanapokaribia kuzaa ndio huhamishiwa kwenye banda la kuzalia

NGURUWE AKIWA KWENYE BANDA LA KUZALIA


UPANDISHAJI
Majike yapandishwe yakifikisha umri wa wiki 28 na uzito wa kati ya kilo 120 – 140, nguruwe aachwe mpaka aingie joto kwa mara ya 3 ndio apelekwe kwa dume ambapo kila baadda ya siku 21 nguruwe huingia kwenye joto

KUINGIA KWENYE JOTO
Dalili za joto ni guruwe kupiga kelele hovyona kuhangaika lakini ukimkandamiza kiunoni na mikono yako hutulia, uke huwa na rangi nyekundu na hutoa ute mweupe. Baada ya dalili za mwanzo nguruwe huwa tayari kupandwa baada ya masaa 38 – 42 na hudumu kwa masaa kama manne (4) inashauriwa ukiona tu dalili za mwanzo umpeleke jike kwenye banda la dume

MIMBA
Mimba huchukua siku 114 mpaka watoto kuzaliwa (miezi 3 wiki 3 siku 3) kipindi cha ujauzito nguruwe jike hula sana mpaka kiasi cha kilo 5 -7 kwa siku apewe mlo kamili lakini kuwe na umakini asinenepe sana na ikifika wiki ya mwisho ahamishiwe kwenye banda la kuzalia (furrowing pen)

BANDA LA KUZALIA


Liwe na ukubwa usiopungua 3m * 2m, liwe na sehemu ya watoto ambayo mama mtu hawezi kufika watoto waingie huko kwa kupenya, hii husaidia nguruwe asiweze kuwalalia watoto wake. Sehemu ya watoto iwe na chanzo cha joto kama vile jiko, hii husaidia kufundisha watoto wakimbilie kule muda wote