KURASA

Sunday, August 30, 2009

MIKARATUSI NA UKWAJU - TIBA YA KIFUA

Mikaratusi na ukwaju ni tiba yenye nguvu dhidi ya kifua na kukohoa, tiba hii ni rahisi kuandaa na haina gharama.UAANDAAJI
Chukua jani moja au zaidi ya mkaratusi lililokomaa kutoka katika matawi machanga/mapya ya mti, ponda ponda na uchuje kwenye maji kiasi cha mililita 100-200, unaweza kutumia blender pia kusagia dawa hii, kisha changanya na juisi ya ukwaju, pia unaweza kuongezea tangawizi kidogo ukipenda.


MATUMIZI
Kunywa mchanganyiko huu mara 3 kwa siku kwa siku 3-5
Ukitumia mchanganyiko huu mara moja kwa wiki ni kinga tosha kwa magonjwa ya njia ya hewaMUHIMU Ukichemsha majani ya mkaratusi chumbani na kuacha mvuke usambae chumbani ni kinga tosha juu ya mafua, pia huleta harufu nzuri chumbani (air freshener)