KURASA

Thursday, May 22, 2008

MBEGU

Mbegu za mitiki lazima zikusanywe kutoka katika miti iliyokomaa, hii itasaidia katika uotaji kwa sababu mbegu za miti hii ni ngumu kidogo kuota. Unaweza kupata mbegu kutoka kwenye mashmba makubwa ya miti au ukanunua kutoka kwa wakala wa mbegu za miti wa taifa (TTSA) ambao wana matawi yao katika kanda tofauti nchini (Morogoro, Lushoto na Iringa) http://www.ttsa.co.tz/

Mbegu zilizo bora ni zile zilizohifadhiwa mahali pakavu, kabla ya kupanda mbegu inabidi ziloekwe kwenye maji yanayo tembea kama mto kwa siku 3 (masaa 72) au unaweza kuzitia kwenye gunia na kuloweka kwenye chomba chenye maji kwa masaa 72, huku ukibadilisha maji kila baada ya masaa 8 -12. Hakikisha unapoloweka mbegu, lile gunia unalifunga na kitu kizito kama jiwe ili ziweze kuzama kabasa ndani ya maji.

Kila unapobadilisha maji utagundua kwamba maji unayomwaga yanakuwa na rangi nyekundu, hii ni kawaida kwa miti hii huwa inaacha alama ya rangi nyekundu (red dye) kama utakata matawi yake kwa mkono.

Ukisha maliza kuloweka mbegu kwa masaa yasiyopungua 72, mbegu zianikwe kwenye jua ili ziweze kukauka kabisa. Unaweza kuzianika juu ya bati ili kuharakisha ukaukaji, hakikisha unazi tandaza ili zikauke vizuri, hii inaweza kuchukua hata siku mbili kama hamna jua la kutosha. Mara baada ya kukauka mbegu zikusanywe na kuhifadhiwa mahali pakavu na pasipo na joto tayari kwenda kupandwa kwwenye kitalu.

2 comments:

Anonymous said...

uko juu kaka.
mimi napenda sana kufuga samaki,nifanyeje kuhusu kuandaa bwawa na mbegu za samaki zinapatikana wapi?naitwa Arafa

Bennet said...

Arafa nashukuru kwa swali lako, siku nyingine ukitaka kuwasiliana nami kwa haraka nitumie email