KURASA

Wednesday, February 18, 2009

MBILIMBI

MTI WA MBILIMBI (M-MBILIMBI)
Huu ni mmea unaopatikana sana sehemu za pwani kama Zanzibar, Tanga, Dar es salaam, Kibaha n.k Ni mmea ambao hauwezi kuhimili ukame wala baridi kali na unastawi zaidi kwenye mvua za kutosha na udongo usiotuamisha maji kabisa.


MATUMIZI


Miaka mingi mbilimbi zimekuwa zikijulikana kwa matumizi ya achali ndio maana sehemu nyingine mbilimbi zilitungwa jina la PICKLE FRUIT. Utengenezaji wa achali uko wa kuchanganya vitu tofauti tofauti kama nyanya, vitunguu, pilipili, ndimu, malimao, chumvi, maembe n.k ambavyo vinankuwa katika vipande vidogo vidigo, unaweka kwenye chupa na kuanika juani kwa siku kadhaa (ingawa baadhi huupika mchanganyiko huu)

Mbilimbi pia hutumika kutengenezea siki (vinegar) na mvinyo, hii mara nyingi hufanyika viwandani na sio majumbani kama ilivyo achali.

Mbilimbi pia ni dawa kwa magonjwa kama chunusi, kifua na kukohoa na mengineyo mengi. Ili kutibu kukohoa unatakiwa utafune mbilimbi kama tunda mara mbili mpaka tatu kwa siku ukichanganya na chumvi kupunguza ukali wake au unaweza kula mbilimbi zilizoiva ambazo ndio zina vitamin C zaidi ya mbichi. Majani na maua yake ni dawa ya vidonda, unaponda ponda na kufunga kwenye kidonda kwa siku kadhaa, pia yanapunguza uvimbe.

MAUA YA MBILIMBIMbilimbi mbichi ambazo ni kali huwa na acid ijulikanayo kama OXALIC kwa kiasi kingi hivyo huweza kutumika kungarishia vitu vilivyotengenezwa na chuma, shaba na aluminium kwa kusugulia na kisha kusafisha na maji safi

6 comments:

Subi said...

Bennet,
Kazi nzuri sana. Elimu haina mwisho na kwa kweli unafanya PUGU nzuri sana hapa. Huwa ninakutembelea mara kwa mara kuchota maarifa.
Narudia kusema tena, Kazi nzuri sana!

Bwaya said...

Kazi nzuri sana Bennet. Unaiwezea elimu hii, bila shaka tutaendelea kujifunza mengi kwa lugha nyepesi kuliko ile ya kwenye kumbi za mihadhara.
Kwa kusoma hapa bila shaka kwa lugha hii rafiki tutajifunza kirafiki.

Bennet said...

Wadau nilikuwa ziarani Tanga sehemu za kilindi kuna mdau mmoja anataka kufungua shamba la mitiki kama ekari 200 alinichukua kwa ajili ya surveying and land planning kabla ya kilimo chenyewe, pia nili msaidia kuandaa kitalu cha miche, maana jamaa kachimba na kisima kabisa, kwa kweli jamaa amejiandaa vizuri.

Nakuja na somo lingine hivi karibuni kwa sababu kila ninachoandika lazima nikijaribu kwanza na sio kuhadithiwa tu.

Pia nina wazo la kuigeuza website kabisa mungu akinijaalia, hii itasaidia kila kitu kikae mahala pake kwa kujitegemea na sio mara miti mara samaki halafu dawa vuruguvurugu mchanganyiko

Subi said...

Bennet, pole kwa shughuli na hongera kwa elimu kwa vitendo.
Kuhusu suala lako la kuwa na tovuti, ni jambo zuri ila, nina hakika kuwa tovuti utakayoiandaa ili iendane na mtindo wa kisasa, itakuwa ya fomati ya blogu, yaani kuweza kuwapa wananchi fursa ya kuchangia, ukitizama tovuti nyingi kubwa kama vile CNN, BBC, TIME nk iliwabidi kubadili fomati ya tovuti zao na kuchukua mfumo wa blogu.
Kwa hivi, utapata tu jina lisilokuwa na .blogspot lakini utakachokifanya hakitatofautiana na hapa.
Ubaya wa kuwa na tovuti zisizoshirikishi ni kuwa lazima kila unapoanza kuandika jambo, basi itakubidi kufungua ukurasa mpya na kuutafutia nafasi kwenye menu, sasa Ben, utafungua kurasa elfu ngapi kwa masomo haya yaliyo lukuki?
Jawabu langu: Endelea kubaki na hizi blogu huru kwa kuwa unapata nafasi bure, ikijaa unaeweza kununua mpya, vile vile nunua jina ikiwa unataka .blogspot iondoke lakini ukikubali kubaki na blogu hii hii, basi weka LABELS ambazo ni sawa na Categories ambazo zitakusaidia kupanga posti zako za aina fulani ziwe na jina laki na za aina nyingine ziwe na jina kulingana na maudhui yanayohusiana, ukitaka kuona mfano jaribu kuperuzi blogu yangu au ya Bwaya, Chemi, Mzee wa Changamoto nk, zile lebo ndizo kurasa/pages zinazomsaidia msomaji kuperuzi masuala kadhaa anayopendelea.
Samahani kwa kuandika kireeeeefu!

SHEMIHASHA HUSEIN said...

Natarajia kuanzisha shamba la nyuki maeneo ya Chekerei Mombo,je,miti ya mbilimbi maua yake yanawavutia nyuki?naomba msaada wa kitaalam kuhusu aina za miti ya matunda inayo wavutia nyuki na inayo stawi maeneo ya joto.

lost no step ent said...

nawezaje kupata mbegu kwaajili ya mbilimbi? email yangu ni simplytheent@gmail.com plz msaada kaka