KURASA

Monday, August 10, 2009

KICHAA CHA MBWA

KUSAMBAA

Kichaa cha mbwa kinaweza kusambazwa na mate ya wanyama, wengi tumezoea kwamba mbwa ndiye anasambaza kichaa, lakini wanyama wengine kama paka, popo, ng'ombe, mbweha, fisi na wengine wanaweza kukisambaza




DALILI ZA MBWA MWENYE KICHAA

siku 1-3 mbwa hubadilika zile tabia ulizozizoea hapa ni ngumu kidogo kugundua

siku 3-4 mbwa huwa na aibu na pia huwa anakwepa mwanga (photophorbia), anajifichaficha na kung'ata kila kitu kinachopita karibu yake hata kama karatasi limepeperushwa na upepo

siku 5 mbwa huanza kulemaa akianzia miguu ya nyuma (hind quarter paralysis) kisha kufuatia miguu ya mbele, baada ya siku saba mbwa hufariki




CHANJO
Mbwa wachanjwe dhidi ya kichaa angalau mara moja kwa mwaka, watoto wanaozaliwa na mama aliyechanjwa wachanjwe baada ya miezi mitatu baada ya kuzaliwa, unaweza kuwachanja kabla kama kuna mlipuko wa kichaa cha mbwa

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nilikumiss maana ulipotea kidogo na pia nilimiss elimu yako. Karibu sana tena.

Bennet said...

Nashukuru Dada Yasinta, nilikuwa nje ya mji kidogo, kisha huko nikapata matatizo kilap top changu kikapigwa na virusi nikapoteza vitu vingi muhimu kwa hiyo sasa hivi hata net ni mpaka niende cafe na kikamera changu nacho kiliharibika ingawa nishanunua nyingine

Nicky Mwangoka said...

Nimefurahi kupata elimu hii maana ,duh mie naogopa sana mbwa ndugu yangu.