KURASA

Monday, August 17, 2009

MBAAZI- cajanus cajan

Pamoja na kuwa ni chakula tulichokizoea sana, lakini mmea huu pia ni dawa ya magonjwa mbali mbali

MAANDALIZI

Chukua majani, maua au mizizi kiasi cha nusu kilo (ni vizuri kama utachanganya vyote) pondaponda na uloweke kwenye maji safi kiasi cha lita 2 kwa muda wa masaa 24.


Chuja na uweke dawa hii mbali na jua/joto, ni vizuri kama ataweka kwenye friji, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 kwa siku 3




TIBA

Dawa hii inaweza kutibu magonjwa yafuatayo

1-Inauwezo mkubwa wa kushusha homa

2-Husaidia kuponesha vidonda.

3-Husaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa wanawake.

4-Husaidia kupunguza uvimbe

5-Huponyesha kifua na kukohoa.

6-Husafisha kibofu/njia ya mkojo.

7- Huongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbali mbali

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Katika kibaraza hiki tunapata kujua mambo mengi ambayo hatukuyajua. Mi nilijua ni chakula tu kumbe ni dawa pia. Ahsante sana kaka Bennet.

chib said...

Dozi yake ni vipi? Glasi moja kutwa mara 2 au.......

Anonymous said...

je unajua dawa yoyote mbadala kwa malaria sugu?
nitashukuru kwa msaada!

Bennet said...

Aksante sana kwa swali lako anony aug 22 12:06am
Kwa ajili ya tiba mbadala naomba urejee makala yangu ya aloe vera

Mzee wa Changamoto said...

Hapa ni tiba m'badala na inanufaisha saana. Asante Kaka

John Mwaipopo said...

Mie kanikumbusha muda mrefu kidogo. sijala mbaazi nina miaka mingi tu.