KURASA

Thursday, November 12, 2009

KASUKU - DONDOO ZA KUMFUNDISHA KUONGEAWatu wengi wamekuwa wakipenda kufuga kasuku lakini utakuta wanalalamika kwamba kasuku wake haongei, nimeamua kuweka vidokezo muhimu ili mfugaji aweze kuzingatia wakati wa kumfundisha
Kuna aina nyingi za kasuku duniani wengine wakiwa na rangi za kawaida na wengine wakivutia sana, kwa kawaida huwa hawaishi sehemu zenye baridi kali kwani hupendelea hali ya joto wastani

UCHAGUZI WA KASUKU
Mbegu kubwa ni waongeaji wazuri, mbegu ndogo ni wavivu kujifunza,
Akiwa mdogo anajifunza vizuri zaidi, ukiweza mpate yule anayetoka kulelewa kwenye kiota na ndio anajifunza kuruka/kupaa
Kasuku muoga hawezi kujifunza vizuri.
Kasuku mwenye tabia ya kung'ata anauwezo mkubwa wa kujifunza kungea.
MAZINGIRA
Kumbuka kasuku hujifunza maneno machache tu hawezi kuongea kama mtu.
Sehemu nzuri ya kumuweka nyumbani ni jikoni, kwa sababu kuna shughuli nyingi.
Huanza kuongea katika umri wa miezi 4-6.
UFUNDISHAJI
Wakati wa kumfundisha zima radio na TV (kusiwe na kelele)
Muda mzuri wa mafunzo ni asubuhi na jioni.
Mfundishe kupiga miluzi baada ya kuweza kuongea baadhi ya maneno na si kabla ya hapo.
Kumbuka kasuku hujifunza vizuri zaidi kwa vitendo mfano unamtoa nje ya kibanda chake huku unamwambia " toka nje mmmh" ukirudia rudia, jitahidi kutumia Mmmh kila baada ya neno, hii humsaidia kujifunza kwa urahisi.
Hakikisha anapata mlo kamili maji na matibabu

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa habari hii ila nikiwa na kasuku huyu basi tutakuwa akina kasuku waengi:-)

John Mwaipopo said...

kwani na wewe yasinta ngonyani ni kasuku? au sijakuelewa? LOL

chib said...

Kumfundisha mtu tu ni kazi, sasa ije iwe kasuku.....

Bennet said...

Inaonekana kweli Dada Yasinta ni kasuku kama alivyosema mwenyewe, sasa kwake yeye itakuwa kazi kumfundisha maana inatakiwa uwe unatamka maneno taratibu kiasi.
Chib ukiamua inakuwa rahisi mbona we jaribu utaona

SIMON KITURURU said...

Asante kwa hii!

Nilikuwa najiuliza hili kwa kuwa rafiki yangu kumfunza kasuku ilimshinda na sikujua hata ni kwanini.Alim-adapti sehemu na nimepata mwangaza ni kwanini kasuku kikongwe anaweza kukununia.

Bennet said...

Kuna hadithi moja inayosema Mama mmoja wa alikwenda kununua kasuku akamkuta anayejua kuongea tayari, lakini muuzaji akamuonya kwamba kasuku huyo alikuwa anafugwa na machangudoa fulani
Basi yule Mama akang'angania kumnunua sababu alikuwa anaweza kuongea, basi alivyofika naye nyumbani kasuku akawa anasema sema kwa kurudia NYUMBA MPYA na MAMA MPYA,
watoto walivyorudi shule akawa anasema NYUMBA MPYA, MAMA MPYA na WATOTO WAPYA mama akaendelea kufurahia, wakati wote huo mumuwe alikuwa safarini, siku aliporudi Mama akiwa na watoto nyumbani baadas ya kupokea zawadi za safari
akaamua na yeye akamwonyeshe mumuwe kasuku, basi kufika kule kasuku alipomuona tu mumewe akasema AAAHH BWANA JUMA

Ina maana jamaa alikuwa anaenda sana kwenye ile nyumba ya machangudoa mpaka kasuku kamzoea na kumjua jina lake