KURASA

Friday, December 11, 2009

TANGAWIZI

1.0 UTANGULIZI:
Jina la kitaalamu ni Zingiber officinale
Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome) ambalo huonekana kama mizizi ya mmea. Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China. Zao hili linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi ya Jamaica. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro.Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji (kama chai, soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, achari n.k. Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k. pia hutumika katika vipodozi kama poda n.k).

2.0 AINA ZA TANGAWIZI
Hakuna uthibitisho wa aina za tangawizi ambazo hulimwa hapa nchini ila kuna dalili ya kuwa na aina za White Africa (Jamaica) na Cochin (flint); hii huwa na tunguu ngumu zenye nyuzi.

3.0 TABIA YA MMEA
Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati Cochin ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu. Mmea una urefu wa futi mbili na majani yake ni membamba marefu ambayo hufa kila mwaka yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua ya mmea huu yana rangi nyeupe au manjano.

4.0 HALI YA HEWA NA UDONGO
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji mvua kiasi cha mm.1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigredi 20-25. Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji.

MMEA WA TANGAWIZI


5.0 UPANDAJI
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm.2.5-5. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 840-1700 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekta moja. Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana.

Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekta na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana. Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, dawa ya kuua magugu, kama simazine au round up hutumika.

MKATE WA TANGAWIZI NA LIMAO


6.0 Magonjwa na wadudu:
• Madoa ya majani yanayosababishwa na viini vya magonjwa viitwavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta zingiberi.
• Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na viini viitwavyo Pithium spp
• Mizizi fundo; inasababishwa na Meloidegyne spp.

7.0 UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana.

8.0 USINDIKAJI
Tangawizi ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa mafuta. Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa zimechanganywa na sukari na/au chumvi au bila kuweka kitu chochote. Hata hivyo tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha 16.0-18.0%.9.0 SOKO LA TANGAWIZI
Soko la tangawizi lipo ndani na nje ya nchi, kiasi kikubwa kinauzwa nchini. Bei yake ni kati sh. 300-1,500/- kutegemeana na msimu.

10.0 GHARAMA ZA UZALISHAJI NA MAPATO
GHARAMA YA HEKTA MOJA:
Mbegu Tshs. 240,000/-
Vibarua 250,000/-
Mbolea(mboji/samadi) 150,000/-
Jumla 640,000/-
MAPATO:
Kilo 20,000 X300 =6,000,000/-

25 comments:

Anonymous said...

Hili zao kumbe lina hela hongera sana blog nzuri ila wasomaji hamna

Anonymous said...

Wasomaji tupo na tunafuatilia kila siku sema huwa hatuchangii kwa sababu mambo haya ni yakitaalam zaidi humu hamna siasa

Halil Mnzava said...

wasomaji tupo,tena sana tu!

Bennet said...

Aksante H. Mnzava ni kweli wasomaji ni wengi lakini sio lazima wote wachangie, anony wa kwanza endelea kunitembelea natumai na wewe siku moja utajitambulisha

Mija Shija Sayi said...

Bennet, unajua tangawizi inasaidia sana concentration na kupunguza kupaniki, jaribu chai ya tangawizi kali nusu saa kabla ya kufanya mtihani au kuprizenti mada au kwenye testi ya uendeshaji gari utaona inavyotuliza.

Anonymous said...

Nakupa hongera kwa blog hii ambayo ni useful. Mimi sikujua kuwa tangawizi inalipa namna hii. Sasa kwa mfano mtu uko Dar na unataka kuanziasha hii, utaaanzaje? Vile vile nilikuwa ninakusudia kufuga ng'ombe wa maziwa, labda nianze na mmoja au wawili. Hao breeders wako wapi na bei inaanzaje. Unaweza kuniwasilia kama itawezekena hapa; naomba usichapishe hii email. ennakili@yahoo.com

Na

kapondo said...

Ni blog nzuri sana. inahabarisha vema kabisa. nikitaka kununua tangawizi kiasi cha kilo 1000 iliyosagwa nitapata wapi? please you may contact me thru dmuwowo@gmail.com

canute Temu said...

Mimi nieanza kuotesha tangawizi vuli ya mwaka 2013. Natarajia mavuno ya kwanza 2014 vuli ! Nakusudia kuuza tangawizi yangu kwa jina la "GINGTANG" yaani GINnger from TANGanyika. Naomba mtu yeyote mwenye taarifa za uhakika kuhusu faida za kiafya [health benefits] za Tangawizi aniletee ili niweze kuziingiza katika kipeperushi kitakachosambazwa na tangawizi zangu. Kwa sasa nauza pia ILIKI [cardamom] na nimeotesha vanila.
Canute Temu, cwtemu@gmail.com , 0754282101, Moshi Vijijini, Masaera , Kilema Kusini, Kilimanjaro. P O Box 270 HIMO, Kilimanjaro.

jina lanug said...

Mhabarishaji nashukuru kwa taarifa hii muhimu. Nimekuwa nikitamani kujua jinsi ya kulima tangawizi kwa muda mrefu ili kuepuka hasara zinazoweza kuepukika na nafurahi kwamba leo nimekutana na blog hii.

Unaweza kuniambia mvuno wa kg 20,000 ni kwenye ukubwa gani wa shamba (kama ni robo eka, nusu eka au eka moja) na bei uliyoiweka ya shs 300 ndivyo unavyouza? Nitashukuru ukinipa majibu haya.

Hii blog ni muhimu mno na asante kwa mchango wako muhimu.

REHEMA KOPAKOPA said...

asante kaka BEN kwa elimu unayotupa,mm n muhitimu wa chuo kikuu cha sua nmesoma FOOD SCIENCE AND TECHNOLOGY. NMEVUTIWA NA KLIMO CHA TANGAWIZI. NAOMBA UNIPATIE NAMBA ZAKO TUWASILIANE NATAKA KULIMA ZAO HILI,naitwa REHEMA 0657038277/0684300312. NIPO DAR ES SALAAM

Prosbry Yalinder said...

nilijaribu kutafta blog kama hii..asanten sana

GADAU FRANK said...

Nashukuru kwa elimu nzuri ya ulimaji wa mazao ya tangawiz lakini naomba ushauri na elimue zaidi kuhusu kilimo cha iliki

Angel Benedict said...

Habari ndugu zangu hongereni kwa Elimu nzuri

Abu Ismail said...

Enter your comment...wadau naomba kufahamu, hyo bei ya tshs 300,ni ukiwa shambani au,coz masokoni bei za jumla ni kati ya 1500 hadi 2500,kutegemeana na msimu

Furaha Ndabila said...

naomba mwenye soko la uhakika la tangawizi anijuze kupitia fnexhibitor@gmail.com

viwanja kwetu Geita( VKG) said...

Nzuri nisaidie namna ya kuotesha


Unknown said...

Kama unahitaji soko la tangawizi nichek xalehemfinanga@gmail.com

Unknown said...

Jamani nimelima tangawizi ekari 3 .msaada maana mda ndo huu wakuuza .nafanyaje kupata soko

Unknown said...

Unapatikana mkoa gani ?

Unknown said...

Nipatie namba yako tafadhali

Unknown said...

Nipatie namba yako tafadhali

Unknown said...

Unapatikana mkoa gani ?

Unknown said...

Au nipigie 0713210020

Unknown said...

Natafuta wauzaji wa jimla wa zao la tangawizi walioko mikoani ...tuwasiliane mapema kwa 0713210020

Unknown said...

Natafuta wauzaji wa jimla wa zao la tangawizi walioko mikoani ...tuwasiliane mapema kwa 0713210020