KURASA

Tuesday, January 26, 2010

SIMBA MWENYE FADHILA



Mwaka 1969 John Rendall na Ace berg walimuona mtoto wa simba (dume) aliyekuwa anauzwa huko Harrods alionekana mpweke ndani ya kibanda chake kidogo na wakaamua kumnunua na kwenda naye nyumbani kwao ambako ni ghorofani na wakampa jina la Christian. Paroko wa kanisa moja aliwaruhusu kucheza naye katika viwanja vya kanisa lakini ndani ya muda mfupi simba alikuwa haraka na kuwa mkubwa ambako kwenye nyumba yao asingeweza kuendelea kuishi zaidi ya hapo.

Wakaamua kumrudisha kwenye mazingira yake ya asili kwenye mbuga za Afrika na baada ya Mwaka walipotaka kumtembelea waliambiwa ya kwamba amekuwa mkubwa na kuwa na milki yake na sasa amegeuka mnyama pori kamili kwa hiyo ni hatari kama simba wengine kwa maana hiyo wasingeweza kumsogelea karibu tena, pamoja na hayo bado waliamua kwenda kumuangalia hivyo hivyo, baada ya kumtafuta kwa masaa kadhaa walifanikiwa kumuona…….. ukiangalia kwenye video hii utaona jinsi alivyo warukia kwa furaha akiruka ruka, kucheza nao huku nao wakimkumbatia na wala hakuwa mkali au hatari kwao kama walivyoambiwa, na mwisho alikuja simba mwingine jike ambaye alikuwa ni mke wake kwenye hiyo milki yake na huyo simba jike naye akabaki akiwaangalia tu na wala hakuwashambulia ( ni kama naye alitambulishwa)

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hakika binadamu tu tofauti. Mmmmhhh kuishi nyumba moja na simba?

mumyhery said...

kumbe kuna wanyama wakumbukao hisani, lakini kuna binaadam wengine hisani inakuwaga nuksani

Yasinta Ngonyani said...

Da M hapo umenine ni kweli afadhali hata ya huyo simba sijui sisi binadamu tupoje?

Anonymous said...

Heri umfadhili mbuzi au mnyama yoyote yule lakini binadamu atakuudhi. Viumbe sie hatuna fadhila wala shukrani nimeyaona kwa macho yangu na nimetendewa wala si ya kusimulia. Bora ningefuga paka au hata mbwa nikamsheheni kwa gharama kuliko kupoteza pesa, na wakati kwa binaadamu. Waswahili wanasema "wafadhilaka wapundaka"!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mbona lawama jamani? kwani nyie mnaolalamika hamlalamikiwi? nyie wazuri?

bora kufuga mnyama kama simba, kwa upendo bila na kuwa na nia mbaya ya kumtafua siku moja, hapo ntakuwa nimetenda wema kuliko kufuga ngombe au mbuzi nikitarajia maziwa au yakigoma nitamtafuna, huo sio wema. au mbwa ili afukuze wezi kama sio paka ili amalize mapanya!