KURASA

Tuesday, January 12, 2010

KAMBALE ANAYETEMBEA

Hii ni aina ya kambale inayopatikana sana bara la Asia na Africa, amepewa jina la kambale anayetembea sababu ya uwezo wake wa kujikongoja na kuhama toka sehemo moja hadi nyingine kupitia nchi kavu kwa dhumuni la kutafuta chakula au mazingira mazuri, sio kwamba anatembea bali hujinyanyua juu kwa kutumia mapezi yake na kujinyonga nyonga kama nyoka na ii humuwezesha kusogea mbele, ana uwezo wa kuka muda mrefu nje ya maji madhali ardhi isiwe kavu bali iwe na unyevu

Hupendelea kwenye maji yenye kina kifupi au yasiyotembea, kama kwenye vijito na mito, mabwawa, majaluba ya mpunga na sehemu yoyote ambayo maji hujikusanya. Hukua hadi sentimeta 30 (urefu wa rula ya mwanafunzi) hana magamba kama kambale wengine bali ngozi yake huwa na ulenda ulenda unaomsaidia atembeapo nchi kavu, ana rangi ya kijivu mpaka kahawia iliyokolea kabisa. Tofauti na yake na kambale wengine yeye hana mapezi ya kwanza juu ya mgongo bali pezi lake la pili huwa refu mpaka karibu na mwisho wa mkia, unapomvua kambale huyu usimshike akiwa hai au hata kama kafa mshike kwa umakini sababu ana miiba iliyojificha kwenye mapezi ya chini karibu na mkiaHupendela halijoto kati ya 10c mpaka 28c, chakula chao kikuu ni samaki wadogo, wadudu, konokono wasio na magamba na mimea ya kwenye maji, kambale hawa wanatabia ya ulafi inayowafanya wawe hatari kwa viumbe wengine wa kweye maji

5 comments:

Upepo Mwanana said...

Habari nzuri, lakini hao samaki mbona wanatisha!!

John Mwaipopo said...

Upepo mwanana hujawahi kuwaonja tu. hasa ukute waliokaushwa wa kutoka ifakara huko, na mpunga mpya. utaacha michips hiyo. usisahau nazi kwenye wali.

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahaaa John. No wonder profile photo yako unacheka.
Asante kwa mara ya tena Kaka Benett lwa uelimishaji huu.
Kwa hiyo huyu ndiye apendaye na awezaye kuishi kwenye tope zaidi?

Bennet said...

Upepo mwanana ni kweli samaki huyu anatisha lakini sio sana
JM hawa samaki kwa kweli ni watamu sana kwa wasafiri wa kuja DSM wanaweza kuwanunua pale Ruvu darajani
Mzee wa changamoto kambale wote huweza kuishi kwenye tope pale ambako maji hukauka kwa ukame, lakini huyu ninaye mwongelea yeye anaweza kuhamia bwawa au dimbwi lolote lili karibu na alipo kama maji yatakauka

Anonymous said...

kaka leo nimeanza kuchimba bwawa la kufuga samaki.naomba unishauri pa kupata mbegu bora za samaki. pia nna shamba langu mkuranga ningependa kufuga huko samaki pia bila kusakafia bwawa any advice?