KURASA

Tuesday, January 19, 2010

MTI MPWEKE ZAIDI DUNIANI

Mti aina ya acacia ulioota kwenye jangwa la sahana nchini Niger ndio mti ulio mpweke zaidi baada ya kuwa umbali wa zaidi ya maili 250 pande zote bila kukutana na mti mwingine. Mti huu uligunduliwa Mwaka 1970 lakini uliota mahala hapo wakati jangwa halijawa kavu kama lilivyo sasa, kwa miaka hiyo ambako mti huu uliota haukuwa peke yake bali kulikuwa na miti mingine ila yenyewe ilikufa baada ya jangwa hili kuendelea kuwa kavu zaidi na kupata kiasi kidogo cha mvua

MTI MPWEKE PICHANIMtii huu Ulikufa baada ya dreva wa lori kutoka Libya alipougonga, inasemekana dreva huyo alikuwa akiendesha lori hilo huku akiwa amelewa pombe. Baada ya mti huu kufa wana sayansi walichimba pembeni yake na kugundua mizizi ilikwenda chini kiasi cha futi 120 (mita 36) mpaka kufikia maji ya chini ya ardhi (water table) Sasa hivi sehemu ulipoota mti huo imejengwa nguzo ya chuma kama kumbukumbu ya mti mpweke zaidi duniani

NGUZO MAHALI ULIPOKUWA MTI MPWEKE

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nanukuu "Mti aina ya acacia ulioota kwenye jangwa la sahana nchini Niger ndio mti ulio mpweke zaidi baada ya kuwa umbali wa zaidi ya maili 250 pande zote bila kukutana na mti mwingine"mwisho wa kunukuu:- Sikujua kama miti naye inakuwa upweke ama kweli duniani hapa duh! kumbe mungu ameumba vitu vingi vipweke.Asante kwa habari hii.

John Mwaipopo said...

yasinta ngonyani :(

chib said...

Aliyeniudhi kabisa ni huyo dereva mlevi aliyeugonga mti huo.

John Mwaipopo said...

hivi jangwa looote hilo huyo dereva akaona aulenge mti tena mti mpweke. jamani watu wana dhambi. wanaugonga hata mti mpweke?

Elyc said...

John mwaipopo umenichekesha sana..eti waugonga hata mti mpweke? Mkuu nice to read the article!!! Ila ninaomba msaada wako tafadhali..naomba unisaidie tafsiri ya mimea hii kwa kiswahili..Thyme tree and Oregano.Na je yapatikana hapa Tanzania? Nimejaribu kugoogle ila sijapata jibu la kuniridhisha!!!