KURASA

Sunday, February 21, 2010

MAKAKARA - PASSION FRUITS

Ni mimea inyotambaa na kuhimili hali nyingi za hewa (sio ukame) mme huu hustawi zaidi ukanda usio na baridi wastani wa 20c – 30c na kiasi cha mvua 1500mm za ujazo kwa Mwaka, tunda huwa na ukubwa wa sentimeta 10 kwa kipenyo na uzito gramu 90, kuna aina kadhaa za matunda haya lakini yale ya kijani/manjano hustawi zaidi ukanda wa pwani na yale yenye wekundu Fulani hustawi zaidi maeneo ya misitu, hupendelea udongo wa kichanga wenye mbolea na usiotuamisha maji, pia udongo usiwe na chumvi nyingi na pia kusiwe na mwamba chini kasi cha mita moja tu.UPANDAJI
Mbegu zipandwe kwanza kwenye mifuko ya plastiki yenye udongo wenye rutuba ya kutosha , kiasi cha Mbegu 3 kwa kila mfuko na mara zinapoota mimea ikingwe na jua kali na ikifikia urefu wa sentimeta 30, huweza kuhamishiwa shambani
Kwenye shamba lako hakikisha kuna nguzo zenye waya mmoja kwa ajili ya mimea kutambaa juu yake, sehemu ya juu baada ya nguzo kuzikwa chini ibakie kama mita mbili na kati ya msatari na mstari iwe ni mita 2 (ukanda wa pwani ) na mita 3 ukanda wa juu kiasi, na umbali kati ya nguzo na nguzo kwenye mstari ni mita 6, na mimea ipandwe umbali wa mita 3 kati ya nguzo na nguzo kufuata mstari.UANGALIZI
MBOLEA

Mbolea za viwandani ziwekwe kutokana na hali ya udongo, muone afisa ugani kilimo ili afanye vipimo kujua mahitaji na upungufu wa udongo,

MAGONJWA WADUDU
Wadudu kama chawa wa mimea na mchwa wekundu ndio adui wa makakara, pia fangasi husshambulia sana maua ya makakara. Dawa za jamii ya kopa zitumike mara dalili za magonjwa au wadudu kuonekana, kiasi cha kilo 2.8 – 3 hutosha kwa hekta moja au gramu 225 kwa ajili ya dumu moja la lita 20

MAGUGU
Makakara yanatakiwa yawe kwenye shamba safi lisilo na majani na magugu, jembe la Mkono au madawa kama ROUND-UP na GRAMOXONE ynaweza kutumika mimea ikishaefuka na kuwa juu kwenye waya

KUFUNDISHA MIMEA
Ni lazima kuyafundisha matawi mawili ya kwanza kwa kuyaelekeza kutambaa kwenye waya kila moja likielekea upande wake na matawi yatakayoota kutokana na matawi makuu nayo yaelekezwe juu kwenye waya yakifikia ukubwa wa sentimeta 30 – 40KUPUNGUZA MATAWI
Silazima kupunguza matawi kwa sababu mmea mkubwa zaidi ndio hutoa matunda mengi zaidi, labda kama kuna matatizo katika uchumaji ndio unaweza kupunguza baadhi ya matawi kiasi.

UVUNAJI

Uvunaji huanza baada ya miezi 8 – 9 baada yam mea kupandwa na matunda hukusanywa baada ya kudondoka yenyewe chini baada ya kuiva kila baada ya wiki moja, matunda yahifadhiwe sehemu kavu na isiyo na joto , kiasi cha tani 5 – 10 huweza kupatikana katika hakta moja kwa msimu

15 comments:

SIMON KITURURU said...

Napenda sana hili tunda ingawa sikujua linanakotokea.

Asante kwa shule hii Mkuu!

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana kwa darasa hili, mwaka jana nilipanda haya matunda ila sidhani kama nilifuata sheria hizi. ntaprint hapa na kuhifadhi, labda yamekufa itabidi nianza upya.Ahsante tena.

Candy1 said...

Nayapenda kweli haya matunda! Nilivyokuwa mdogo nilikuwa naogopa kula na kuzimeza zile mbegu ila siku moja tu nikaamua kuyala, ndio yes! nikiyapenda kweli.

Emmanuel Kisanga said...

hivi mkuu unaposema hekta unamaanisha sqm ngapi? zinanchanganya sana kati ya heka na hekta

Gloria Mahinya said...

Ahsante kwa darasa nimelifurahia. Ninashughulika na vitalu vya mikakara rangi nyekundu. Napenda kujua zaidi dawa ya asilia ya kutibu magonjwa ya kujikunja majani.

Ahsante

Frank Mbele said...

NAPENDA KUJUA AINA ZAKE KIUNDANI ZAIDI (SPECIES) LOCAL PAMOJA NA ZA KIGENI

Suitbert Maro said...

Heka 2.5 mkuu

Edward Lupembe said...

VP kaka we huna group wattsup maana elim unayotupa inatufaa sana

Unknown said...

Mche mmoja wa passion unaweza kuvuna mara ngapi hadi kufikia kuzeeka kwa mche huo

hertu farms said...

NAWEZA KUPATA MCHANGANUO WA GHARAMA

Leo_Farmer said...

Habari zenu ndugu, ningependa kujua hasa kuhusu soko la hili zao,nina shamba langu na ninataka kupanda hili zao sasa shida ni! sijui wapi ntayauza baada yakupanda na kuvuna.

Ferdinand Kweka said...

Nashukuru kwa somo hili. Mimi nilipanda miche 5 mwaka huu mwezi wa 5 na sasa ndio yamezaa bado hayajaiva. Nimekuwa nikijifunza kupitia miche hii michache. Kwa upande wa upandaji ukiweka mita 3 kutoka mche na mche unakuwa karibu maana yanafungamana sana. Ningependekeza umbali wa mita 4 - 5. Kwa matokeo ya miche hii michache imenivutia kuongeza idadi zaidi na sasa nimeandaa Shamba na leo nakwenda kupanda miche isiyopungua 60 kwa eneo nililonalo. Nitaendelea kujifunza zaidi kupitia ukurasa huu na Shamba hilo nililoliandaa.

Unknown said...

Ekari moja naweza pata gunia ngapi za kilo 100? msaada jamani kwa anaye tambua anijuze

Lucas Michael said...

Thanks to the Blog host, it is a good topic. I have four plants bearing fruits after 10 months, i planted them locally but i can now do better after this lesson . thanks again

Awiscofarmstz.blogspot.com said...

Real nice